Hii ishu ya Mchanga kwangu sio Habari, Ishu kwangu Mikataba iliyosainiwa kwa Siri ?

Mahweso

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
1,098
1,501
Kiukweli Tanzania inaonekana kabisa tuna utani na Maendeleo, yaani wenzetu wako siriasi lakini sisi tunatania.

Nakumbuka kunakipindi Fulani Wabunge wa upinzani walipiga Sana kelele kuhusu mikataba ya Madini, Mikataba ya kibiashara kupelekwa Bungeni na kupitiwa kuangalia Kama ina masirahi kwa Taifa Serikali ikajibu Mikataba ni Siri,

Sasa hii ishu ya Makontena ya Mchanga Watanzania tunauhakika gani kama hawakuruhusiwa kusafirisha? Ni Miaka mingapi Mchanga unasafirishwa mpaka leo?

Wapinzani walipiga kelele kuhusu kusafirishwa Mchanga mbona Serikali ilitetea? Wakati Serikali inatetea mikataba ilikuwa inasemaje?
Na kwanini ilikuwa inatetea na Leo inazuia,

Tukisema inchi haina Dira mnakasirika,
Hatuna mipango na vitu vyetu tuvitumie vipi,

Nchi ya maigizo hii, mimi sielewi wapi tunaenda.
 
Hivi bandari yetu nayo imekuwa 'location' maarufu zaidi nowadays!?
 
Badala ya kutumbua mikataba ya hovyo kila siku anarukaruka na kutumbua watumishi wanaosimamia mikataba aliyoshiriki kuipitisha na ile iliyosainiwa sirini sasa anaishi nayo kabatini pale magogoni bila kuifumua. Utatutumbua sana kwa kansa iliyotengenezwa na CCM.
 
Ishu sio siri. Mkataba unaweza kuwa siri,wazi au nusu wazi.
Tuombe bunge wapitishe sheria sijui policy ya lazima mikataba iwe wazi au partially transparent.
Wawekezaji waukweli hapend a maana inawafanya waaminike na wasichukiweke na wananchi wa eneo Lao la kazi na pili hupunguza rushwa na ufisadi.
 
Sikushawishiwa na mtu wala hakuna aliyenichukulia fomu. Sipangiwi cha kupost, Bando ni langu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom