IKULU: Rais Magufuli apokea taarifa ya ripoti ya Pili ya Mchanga. Waliosaini Mikataba Wakaangwa

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,227
5,270
Angalia hapa kupitia Facebook

Angalia hapa kupitia youtube


Soma ripoti ya kwanza ya mchanga wa madini => IKULU: Rais Magufuli apokea ripoti ya uchunguzi wa mchanga wa madini. Amtaka Waziri Muhongo ajiuzulu

Naam, kama tulivyotangaziwa siku ya jumamosi na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu; Leo ndio siku ambayo watanzania wengi wamekuwa wakiisubiri kwa hamu kubwa. Siku ambayo Mh. Rais anatarajia kupokea ripoti ya pili ya uchunguzi wa makontena ya mchanga wa madini, ripoti ambayo itajibu hoja na maswali mengi ambayo tulikuwa nayo miongoni mwetu.

Karibu tupate kujuzana yale yatakayojiri kutoka viwanja vya IKULU jijini Dar es Salaam.

UPDATES

Mh Rais ktk kutekeleza uchunguzi wa kiasi cha madini; tulikuwa na hadidu za rejea zifuatazo;

1. Kufanya tathmini ya makinikia iwapo taratibu zinafuatwa

2. Kupitia mikataba iwapo inazingatia maslahi ya nchi

3. Kuafanya tathmini ya thamani ya makinikia

4. Kupitia ripoti ya utafiti wa wataalamu aina kiasi, kiwango na ubora wa madini yaliyopo ktk maikiniaka hayo

5. Kubaini idadi ya makontena yaliyosafirishwa ktk makontena hayo.

6. Kubaini na kujiridhisha kama kuna sababu za msingi zinazokwamishwa uanzishaji wa kiwanda cha makinikia hapa nchini. Ni gahrama kiasi gani

8. Kubainisha uwepo wa mikataba ya madini

9. Kuangalia mambo yote yenye uhusiano na endapo itafaa; kamati itakuwa na jukumu la kumuita mtu yeyote ili kupata taarifa zinazohitajika.

Mpangokazi
Kutembelea na kupata taarifa kutoka Pangea, Bulyanhulu, Geita na Mamlaka ya bandari,TRA,NBS, wakala wa madini, stamico,BRELA, Mamalaka ya masoko na mitaji kuwaita na kufanya mahojiano na viongozi wa serikali kupata taarifa na kujifunza ktk biashara ya madini kukusanya na kuchambua na makontena yaliyosafirishwa nje ya nchi toka 1998 kufanya utafiti kuhusu ujenzi wa kiwanda kufanya utafiti wa kimaabara

MATOKEO YA UCHUNGUZI
Kuhusu uhalali wa kisheria
1.Kampuni ya ACACIA haikusajiliwa Tanzania na haina hati ya uchambuzi

2.Kampuni haikuwahi kuwasilisha nyaraka kuonyesha ni mmmliki wa makampuni hayo

3.Kutokana na kukosa certificate of compliance haina uhalali wa kuchimba madini.

Biashara ya makininikia nje ya nchi

Kampuni ya Pangea na ACACIA ndo zinahusika katika usafirishaji
Makinikia yanasafirishwa kwenda China, Japani, Ujeruman ktk makontena ya futi..20,40 n.k

Mauzo ya makinikia hufanyika kupitia ofisi ya uhasibu iliyopo Africa ya Kusini. Japo kampuni hizo za uhasibu zilisajiliwa Tanzania.Kisheria kampuni za madini zinatakiwa kutoa taarifa sahihi za serikali kuhusu aina, kiasi na thamani ya madini.

Makampuni ya madini yametenda makosa yafutayo;
1.Ukwepaji wa kodi
2.Kutoa taarifa za uongo
3.Kujipatia mali kwa njia zisizo halali
4.Uhujumu uchumi

Wamevunja sheria kupitia sheria ya usimamizi wa kodi.

Kudanganya kuwa madini yaliyokuwa kwenye makontena 277 ni sh bilioni 279.24 wakati ni sh 829 hadi 1.438
Kitabu cha mrabaha

Vitabu vya ACACIA na pangea vinaonyesha kati ya 1998.2017 kiasi cha milioni 111.3$ wakati vitabu vya serikali vinaonyesha kiasi cha milioni 42.7$

Kutoa taarifa za uongo za uchenjuaji wa makinikia yanayoenda nje ya nchi wakati yanauzwa kabla ya kuchenjuliwa.

Makontena 60 yenye makinikia makontena 48 yalioneshwa kwenye hati ya usafirishaji badala 67 yenye urefu wa 20 makontena 65 yalioneshwa kwenye hati ya usafirishaji badala 99 yenye urefu wa futi 20.

Madini yanayouzwa nje ya nchi hayakuwa makinikia hasa yamekuwa ni madini megine ya aina mbalimbali.

Uchunguzi makampuni ya madini yanafanya gharama za uzalishaji kuwa juu sana ili kukwepa kodi kwa serikali.

Makampuni ya madini kwa mwaka 2002 na 2006 yalipata faida ya asilimia 32 lakini haikuoneshwa kwa serikali.

THAMANI YA MADINI YALIYOPO KWENYE MAKINIKIA


Kamati ilitumia kampuni kutoka idara ya forodha, ofisi ya takwimu, n.k
Makontena yaliyosafishwa ni 44,277 kwa kiwango cha chini na 61,320 kwa kiwango cha juu.

Kwa kutumia 47..tani 2010.3..188.32trilioni kwa kiwango cha chini.

Viwango
  1. Silva kilo 6.1 kwa kila kontena sawa na tani 270 yenye thamani ya shilingi 329.66.
  2. copper 5200 kwa.
  3. Sulper 7800 sawa na shilingi bilioni 277.
  4. Iron kilo 524 kwa kontena moja sawa na shilingi bilion 328.2 kwa makontena yote.
  5. Nikel kilo 5400 thamani ni shilingi bilioni 8.42 kwa makontena yote.
  6. Platnum 0.04kg kwa kontena sawa na bilion 105.7 kwa makotena yote.
  7. Heradium 36.24kg sawa na trilion 17.24 kwa makontena yote.
  8. Heribium 67.24kg kwa kontena sawa na trilion 1.9 kwa makontena yote.
  9. Berilium 64kg kwa kila kontena..sawa ni shiling bilioni 959.2 kwa makontena yote.
  10. Lithium 21.5 kwa kontena zote sawa na sh bilion 129.8 kwa makontena yote.

Jumla ya thamani ya madini yaliyosafirishwa toka 1998 hadi 2017 ni trilioni 132.56 kwa kiwango cha chini na trilioni 229.9 kiwango cha juu.

Thamani ya tani 61,320 toka mwaka 1998 hadi 2017 ni sh trilioni 188.59 na trilion 380.29 kwa kiwango cha juu.

Kiasi cha mapato kilichopotea
  • Trilion 57.57-Kodi ya mapato
  • Trilioni 94.Kodi ya zuio(Witholding tax)

Jumla ya mapato kilichopotezwa na serikali ni trilioni 68.59 sawa na bajeti ya miaka miwili mfululizo fedha zingetosha kujenga reli toka Dar hadi Mwanza

Taarifa ya uchenjuaji ya makinikia nje ya nchi.

1.Serikali siyo sehemu ya makinikia hayo.Yaani serikali haina taarifa

Mikataba ya uchenjuaji wa madini

1.Mgodi ya Bulyanhulu; ktk mkataba huu uliosainiwa na waziri wa nishati na madini.Serikali ilimilki 15% ya hisa, mkataba ulifanyiwa marekebisho na kuondoa 10% na kubakiwa na 5% na baadae zikauza zote kwa makubaliano ya kulipa Dola laki 1 kila mwaka.Kamati imebaini marekenisho ya mikataba hiyo hayakuwa na manufaa kwa serikali.

Mikataba ya Pangea ilisainiwa na;
1.Daniel Yona
2.Nazir Karamaji

Serikali haina hisa yoyote na mkataba unatoa nafuu mkubwa kwa kampuni

Mkataba wa North Mara;
1.Ulisainiwa na Daniel Yona na kufanyiwa marekebisho ya Nazir Karamagi

Serikali haina hisa yoyote

GGM=Geita Gold Mine
1.Abdalah Kigoda

Serikali haina hisa na unatoa nafuu kwa wachimbaji.Waziri hawezi kurekebisha masharti ya leseni ya mikataba.

Mikataba ya uchimbaji wa madini inazuia vifungu thabiti na sera inayozuia mabadiliko japo mikataba ya madini ina vifungu vigumu vinavyozuia marekebisho lakini bado Mikataba ya madini inaweza kurekebishwa.

MISAMAHA YA KODI
Mikataba inatoa miasamaha mingi ya kodi; hivyo mikataba hii haina manufaa
Makampuni ya madini hayaweki fedha za mauzo ya madini katka benk za ndani na kukosesha ukuaji wa uchumi.

Kuweka fedha ktk benk za ndani ya nchi kutasaidia kupuzuia ukwepaje kodi
Hakuna utaratibu mathubutu uliowekwa juu ya mafunzo na ajira kwa wazawa.

UWAJIBIKAJI KTK KUTOA HUDUMA KWA JAMII
Mikataba inawataka kutoa uchangiaji wa shughuli za kijamii. Hata hivyo uchangiaji ni mdogo mno.

UHURU WA MADARAKA YA WAZIRI MADINI
Kamati imeona ni vema madaraka yakadhibitiwa kwa kupata idhini ya bunge kama wanavyofanya Ghana

Kamati imeona hakuna haja ya kupeleka migogoro ya madini nje ya nchi kwani mahakama za ndani ya nchi zinaweza kushughulikia hata mahakama kuu.

KIWANDA CHA MAKINIKIA

Tanzania inaweza kuanzisha kiwanda cha kuchenjua makinikia kwa kutumia teknolojia iliyopo ndani ya nchi yetu.
Tuna mitambo inayoweza kutengeneza joto la hadi 3000C

UKOSEFU WA WAKALA WA MELI BANDARINI

Nchi imekuwa inapoteza mapato mengi kukosa mapato mengi kutokana na kukosa wakala wa meli hasa baada ya kuvunja NASACO

MAPENDEKEZO

Kutokana na uchunguzi kamati imebaini kuna ukiukwaji mkubwa wa mikataba na sheria za madini.

Kamati inapendekeza serikali ifanye yafuatayo;

1. Serikali kupitia msajili wa makampuni ichukue hatua za kisheria dhidi ya ACACIA mining PLC kwa kuendesha shughuli zake nchini kinyume na matakwa ya sheria.

2. Serikali idai kodi na mrahaba kutoka kwa makampuni yote ya madini ambayo yamekwepa kulipa kwa mujibu wa sheria.

3. Serikali iendelee kuzuia usafirishaji wa makinikia nje ya nchi mpaka hapo makampuni yanayodaiwa yatakapolipa kodi, mrahaba na tozo stahiki.

4. Serikali ianzishe utaratibu utakaowezesha ujenzi wa kiwanda cha kuchenjua makinikia ili kuondoa upotevu wa mapato na kutengeneza ajira.

5. Serikali ifanye uchunguzi na ichukue hatua za kisheria dhidi ya waliokuwa Mawaziri, Wanasheria wakuu na manaibu wao na wote waliohusika ktk uingiaji wa mikataba na kutoa leseni, waliohusika kuongeza muda wa leseni na kuondoa nyaraka za usafirishaji wa makinikia(Freight forwarders) na makampuni ya upimaji madini.

6. Serikali ifute utaratibu wa kupokea asilimia 90 ya mrahaba na kulipa asilimia 10 baadae.

7. Serikali ifanye uchunguzi kuhusu mwenendo wa watumishi wa idara ya walipa kodi wakubwa ya TRA ktk kushughulikia madai ya kodi ambayo mahakama ya kodi ishatolea uamuzi.

8. BoT ifuatilie malipo ya fedha za kigeni yanayotokana na mrahaba wa mauzo ya madini.

9. Serikali ianzishe udhibiti wa vitendo vya hujuma kama utoroshaji madini katika viwanja vya ndege vilivyopo katika migodi.

10. Serikali iongeze kiwango cha adhabu kwa makampuni ya madini yanayokiuka mikataba ya madini.

11. Serikali kupitia wataalamu ipitie mikataba yote mikubwa ya madini na kuondoa misahama yote ya kodi isiyokuwa na tija.

12. Sheria iweke kiwango maalumu cha asilimia ya hisa itakayomilikiwa na serikali ktk makampuni yote ya madini. Pia Serikali iweze kununua hisa ktk makampuni hayo.

13. Serikali ianzishe wakala wa meli kama ilivyokuwa NASACO.

14. Sheria ya itamke bayana kwamba madini ni maliasili ya watanzania na iwekwe chini ya udhamini na uangalizi wa rais kwa manufaa ya Watanzania.

15. Sheria itamke mikataba isiwe ya siri.

16. Sheria iweke uwazi na kuondoa mamlaka ya waziri wa nishati na madini, Kamishna na Maofisa katika utoaji wa leseni za uchimbaji.

17. Muombaji wa leseni ya madini aonyeshe mchanganuo wa kina wa jinsi atakavyoendesha mafunzo na wataalamu wa ndani.

18. Sheria ielekeze fedha zitokanazo na mauzo ya madini ziwekewe benki ya ndani ya nchi.

19. Serikali ipitie na kufanya marekebisho au ifute kabisa sheria ya madini ili kuondoa masharti yasiyo na tija.

20. Serikali igharamie na kutoa mafunzo kwa watumishi wa serikali ili waelewe kuhusu masuala ya mikataba ya madini.

21. Serikali kupitia kamishna wa madini ifanye kaguzi za mara kwa mara ili kujiridhisha kama kuna kiukwaji za mikataba ya madini.

==========

Rais Magufuli, anasema...


=>Nawapongeza kamati; Nafahamu kwamba mliweza hata kuhatarisha maisha yenu.
Mawaziri hawaendi hata kwa kukosea kukagua

=>Dhahabu inayeyuka katika joto dogo kuliko hata chuma

=>Dhahabu inayeyuka ktk joto la 600C wakati chuma inayeyuka ktk joto la 1500C lakini tunaambiwa smelting haiwezi kuanzishwa nchini.

=>Yupo mmoja anapiga kelele tumefuatilia anaandika meseji kwa Mwanyika akiomba data.
Hizi fedha ni za watanzania

Tumekuwa masikini
=>Prof Kafumu kaenda kumbembeleza Prof Mruma ili afanye forgery.

=>Mapendekezo yote yaliyotolewa na kamati hii nimeyakubali kwa asilimia 100.

=>Wote waliotajwa humu wafuatiliwe, wahojiwe na wafikishwe kwenye vyombo vya dola.

=>Tukiendelea kukaa kimya tutakuja kuulizwa na Mungu.

=>Wizara iwaite idai fedha zetu; kabla ya kuwa registered. Wakikubali kwamba 'watumetubu' walipe walichotuibia. Baada ya hapo ndipo negotiation ya registration zifanyike.

=>Waziri wa sheria kupitia kwa Prof Kabudi, pitieni hii sheria ipelekwe bungeni na ikiwezekana hata kipindi cha bunge kiongezwe.

=>Serikali ilikuwa na share ya 50% imeshushwa mpaka 35% na hiyo 35% hatupati divident viongozi wapo lakini hawafuatilii.

=>Kwa kweli watanzania tubadilike, hii ni kazi ngumu inahitaji msaada wa mwenyezi Mungu

=>Huwezi kuwa na mwekezaji kwaajili ya exploitation

=>Pale BOT kuna Phd 17; This is the result

=>Ripoti hii mmeisikia naomba kila mmoja akaishughulike katika eneo lake

=>Ni lazima tuchukue maamuzi magumu, no matter yanamuhusu nani!

=>Hii ishu inatakiwa tushikamane kwelikweli.

Ninashukuru sana wale wazee walioamka na kutusapoti katika vita hii ya uchumi.
Tumechezewa vya kutosha, ni lazima tufike mahali tuseme imetosha.

Ninakushukuru Mh Spika maana kwa wale wanaoropoka unaenda nao vizuri, endelea hivohivo.

Wakitoka nje ya bunge;Tutadili nao vizuri maana wakiwa ndani hatuwezi kuwashughulikia.

SOMA/PAKUA RIPOTI NZIMA > HAPA
 

Attachments

  • TAARIFA-YA-KAMATI-YA-PILI-YA-MAKINIKIA-12-Juni-2017.pdf
    337 KB · Views: 261
Naam, kama tulivyotangaziwa siku ya jumamosi na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu; Leo ndio siku ambayo watanzania wengi wamekuwa wakiisubiri kwa hamu kubwa. Siku ambayo Mh. Rais anatarajia kupokea ripoti ya pili ya uchunguzi wa makontena ya mchanga wa madini, ripoti ambayo itajibu hoja na maswali mengi ambayo tulikuwa nayo miongoni mwetu.

Karibu tupate kujuzana yale yatakayojiri kutoka viwanja vya IKULU jijini Dar es Salaam.

UPDATES
usisahau pia leo ndio inawasilishwa BAJETI M'BADALA kutoka UPINZANI. hii ndio muhimu zaidi
 
Naam, kama tulivyotangaziwa siku ya jumamosi na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu; Leo ndio siku ambayo watanzania wengi wamekuwa wakiisubiri kwa hamu kubwa. Siku ambayo Mh. Rais anatarajia kupokea ripoti ya pili ya uchunguzi wa makontena ya mchanga wa madini, ripoti ambayo itajibu hoja na maswali mengi ambayo tulikuwa nayo miongoni mwetu.

Karibu tupate kujuzana yale yatakayojiri kutoka viwanja vya IKULU jijini Dar es Salaam.

UPDATES


Wewe umeshafika hapo Ikulu?
 
Back
Top Bottom