Hii inatupeleka wapi?

Hii inatupeleka wapi?

Eliphaz the Temanite

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2010
Posts
3,017
Reaction score
1,154
Siku hizi mapenzi ni pesa, utajiri, ana gari gani, ana nyumba ama kapanga, na kama huna vitu hivyo utaitwa mwanaume suruali. Na kwa vile wigo wa kujua nani kafanya nini na wapi umepanuka sana utaona kwenye Facebook, Instagram, tweet Google+ nk,....nk jinsi watu wanavyokula bata. Maadili ya kijamii yanaporomoka. Hatufikiri tena jinsi gani tutatengeza famila zenye maadili, kujituma katika kazi, na uadilifu. Kibaya zaidi tumemsahau Mungu. Hii sio dalili njema kabisa

Mara nyingi nimesoma humu jinsi wanawake wanavyolalamikia wapenzi waio na pesa, imefika hatua hata ukiomba/kukopa pesa kwa mwenzi wako anakuona wewe ni hookworm tena anakupiga chini! Akili zimekuwa polluted, tunataka mafanikio na utajiri wa haraka haraka. Matokeo yake ni udanganyifu, ubabaishaji na ubadhilifu.

Hii trend sio dalili njema, Kama taifa vijana tunataikwa ku engage katika national dialogue zitakazo turudisha katika misingi ya uadilifu.
 
Elea vizuri bas!
Nini kifanyike ili kuwe na hali kama uitakayo!!!!
 
Nadhani uko sahihi sana. Nimekuelewa sana mkuu inabidi tubadilike.
 
Elea vizuri bas!
Nini kifanyike ili kuwe na hali kama uitakayo!!!!

Jikubali vile ulivyo.
Jiamini kwamba hata mwenza wako hana kazi, hana pesa, wewe unazo unaweza kumboost akafika pale mnapotaka.
Amini kwamba maisha siyo fedha, nyumba, gari, ni vile ulivyopanga
Amini kwamba Mungu ndiye anayepanga. Mambo ya kuchomana mikuki ya hela, demanding za kipuuzi tuzifute.
 
wewe mleta uzi nataka ufaham kuwa kuna kitu kinaitwa UTANDAWAZI ndo maana unapelekwa shule!
kwa sasa mke na mume wote wanahusika kufanya kazi!
hizo picha uzionazo kwenye facebook,twitter n.k zinakuhamasisha na wewe ufanye kazi kwa bidii ili ufanikiwe!
haikatazwi kumkopa mwenza ila isizidi kikomo si unajua TOO MUCH IS HARMFUL na mungu hatujamsahau bhana ila wewe mwenyewe ni shaidi viongozi wa dini hawaelewani vipi upande wetu!
 
Unadhani watakuelewaaa?? Tulishahama analogia tupo digitali Wenye akili zao wataishi kwa raha,wenye kufata mfumo lazma waumie!!btw-u a right watu wabadilike.
 
Sio vibaya kwenda na utandawazi sio vibaya kwenda ki-digitali ni vitu vizuri vinavyoharakisha maendeleo lakini hatupaswi kuyaparamia haya mambo na kutuondolea uadilifu
Kinachoniumiza kichwa ni mabadiliko ya kimitazamo kwamba usipokuwa na pesa, nyumba, au gari hufai kwa watu mwanaume au mke wa mtu fulani. Hii inaondoa uadilifu, uaminifu na Misingi ya kazi. Principal za maisha ni fanya kazi kwa bidii, ukitumia maarifa na elimu yako. Mafanikio hayaji kwa haraka kama wengi tunavyodhani leo
 
Back
Top Bottom