Hii inamhusu mama mwenye nyumba!!!

Hii inamhusu mama mwenye nyumba!!!

sakapal

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Posts
1,804
Reaction score
1,425
Habari yako wewe mama uliyefungua uzi huu kutaka kujua nini kilichojiri. Na wengine pia habari zenu :behindsofa: !!
Ni hivi msimu wa likizo na sikukuu ya kumaliza mwaka umewadia na muda huu mambo mengi huwa yanatokea kwenye familia. Wakati huu wa likizo wanafunzi walioko bording wanarudi majumbani na ndugui na jamaa wa vijijini wanataka kuja mjini kusalimia mjomba na shangazi. Wakati huohuo wakazi wa mjini wamepanga kwenda kula sikukuu kijijini ili watoto wale wanaosoma academy schools wajue walikotokea mababu zao. Basi mwezi huu unakuwa busy watu wakisafiri huku na kule wengine hata kusafiri nje ya nchi na familia nzima. Kutokana na purukushani hizi za hapa na pale matumizi huwa mengi na makubwa kwa mwezi wote huu wa 12 na hivyo mwezi unaoanza na mwaka mpya ada zinatakiwa kwa watoto kurudi mashuleni na hivyo matumizi kuendelea, nimeona mama kama msimamizi wa familia anawajibu wa kuhakikisha yafuatayo,
  • Chakula kinakuwepo kwa msimu wote huu wa likizo hadi kufikia mwaka mpya.
  • Kujua idadi ya watu wanaolala nyumbani kwake au kujua wageni atakaowapokea kipindi hiki
  • Kuhakikisha watu wote walio nyumbani kwake wanakula na kupata mahali pa kulala
  • Kama kunasafari ya familia hakikisha unabook ticket mapema au kuhakikisha usafiri mtakao tumia wakati wa kusafiri uko salama na wa uhakika
  • Kuzingatia usafi maana kipindupindu huwa kinaanza msimu huu wa mwisho wa mwaka ambapo matunda ni mengi.
  • Mama punguza matumizi yote ambayo siyo ya lazima kwa familia yako
  • Kila hela unayopata mwezi huu weka asilimia 5 kama akiba ya mwakani kama si asilimia 10
  • Hakikisha ada za watoto january ziko kibindoni kabla hamjaanza kusheherekea sikukuu za mwisho wa mwaka
  • Kufurahia msimu huu wa likizo pamoja na watoto wako na mumeo na ndugu zako wa karibu.

ANGALIZO: SI LAZIMA KUKARIBISHA WAGENI AMBAO HUTAWEZA KUWAHUDUMUA USIJEAIBIKA.

Huu ni mtazamo wangu, nmawe weka wa kwako kwa msimu huu wa sikukuu na likizo ambapo dunia nzima iko kwenye kusheherekea. Najua wajibu wa wababa pia upo ruksa kuwakumbusha wakina baba nini wanatakiwa kufanya msimu huu.
Nawakilisha.
 
sisi masingle ni full kujiachia,!
hakuna cha ada wala nepi ya mtoto mwakani
hapa nafikiria niende nchi gani kujiliwaza na maswahibu yalonikuta mwaka huu

Wacha nikupe mji mamiiii...

Tokelezea Jerusalem israel for a cristmass.... Tuna mpango wa kutokelezea huko kuondoa stress... Almost 2.5m inakutosha for roundtrip ticket and a week expenditure around there...

Kama vipi unga tela safari around 19 december... Pale st joseph church wanafanya taratibu zote na maelekezo...
 
Sasa leta ushauri kwa wale wanaokuja mjini na jogoo kwenye kwapa kipindi hiki wafanyaje hasa.
 
Hivi umeniona???

Yaani Sakapal, you must be a witch!

Watu wanakuja, wanataka na nauli uwalipie, na hela za kulipa madeni huko waliko uwatumie
Na wakija kwako maisha yaendelee kama kawaida bila kusahau vi-outing vya hapa na pale.

Kweli situmii mtu hata senti tano, anayeweza na ajilipie, Shabashhh!
 
I wish . . . . .

aisee poa mkuu nitakupm ngoja nikashuhudie alikozaliwa mfalme wetu alietuweka mjini hapa JESUS
 
Mie Tangaaaa mara hii naona kama siku yangu yalikizo iko mbali nnavyo tamani maembe tanga na nguru kwa muhogo
asubuhiii hadi rahaaaaaaaaaaaaaaaa........
 
hivi umeniona???

Yaani sakapal, you must be a witch!

Watu wanakuja, wanataka na nauli uwalipie, na hela za kulipa madeni huko waliko uwatumie
na wakija kwako maisha yaendelee kama kawaida bila kusahau vi-outing vya hapa na pale.

Kweli situmii mtu hata senti tano, anayeweza na ajilipie, shabashhh!
mimi sio mchoyo lakini huwa nashangaa kwanini watu wengine wanapenda kula raha kupitia migongo ya wengine
by the way kongosho tuwe serias mi i wanti to sipend the holidayi withi yuuu! Eizer in yua pulace or mine mmmh!
 
At my place tafadhali

Ila uje na mchele kilo 3, jogoo 2, soda kreti moja, fanta ziwe nyingi zaidi, hoho kilo 1, karoti kilo 2, vitunguu maji kilo 1, nyanya kiko 2, kabechi na vitunguu swaumu ntanunua

mimi sio mchoyo lakini huwa nashangaa kwanini watu wengine wanapenda kula raha kupitia migongo ya wengine
by the way kongosho tuwe serias mi i wanti to sipend the holidayi withi yuuu! Eizer in yua pulace or mine mmmh!
 
at my place tafadhali

ila uje na mchele kilo 3, jogoo 2, soda kreti moja, fanta ziwe nyingi zaidi, hoho kilo 1, karoti kilo 2, vitunguu maji kilo 1, nyanya kiko 2, kabechi na vitunguu swaumu ntanunua
hayo usijali mimi sio parasite bwana nitakuja na zaidi ya hayo mbona.
Mi nataka tu niwe na wewe msimu huu wa sikukuu
 
Hivi umeniona???

Yaani Sakapal, you must be a witch!

Watu wanakuja, wanataka na nauli uwalipie, na hela za kulipa madeni huko waliko uwatumie
Na wakija kwako maisha yaendelee kama kawaida bila kusahau vi-outing vya hapa na pale.

Kweli situmii mtu hata senti tano, anayeweza na ajilipie, Shabashhh!

mi nakwambia Kongosho kwa umri wangu huu na uzoefu nilionao msimu wa likizo hasa wa mwisho wa mwaka kwa wengine ni msala. Tena wengine hawasubiri uwatumie nauli anakuja anakwambia nimnekopa na kwasababu hataweza kuondoka kwako bila wewe kumpa nauli utajikuta na madeni yake umemlipia nakwambia sjui dawa ya tatizo hili ni nini? Labda mkuu Mtambuzi aka baba Ngina aje atueleze cha kufanya usijekuta lile kabila wanaloenda kwqao kuhesabiwa kila ifikapo mwisho wa mwaka wanakwepa wa kijijini wasije mjini na sikukuu kijijini haina gharama kama ukifanyia mjini, hii nina uzoefu nayo. Nahisi kwa baadhi ya familia msimu huu ni tatizo kwa watu wengi ndo maana wizi hauishi na ufisadi ili uweze kukirimu wageni wako na familia kwa ujumla.
 
Sasa leta ushauri kwa wale wanaokuja mjini na jogoo kwenye kwapa kipindi hiki wafanyaje hasa.

ni kujipigia mahesabu ya chakula utakachokula msimu mzima utakako fikia ndo uje nacho huyo kuku kama utamla kipindi chote utakachokuwa mjini haya, namna hii watu wa mjini hawawezi kuacha ufisadi na wizi ili kukidhi mahitaji ya pembeni kama haya..., we utoke kwako uje kukaa kwa mtu na familia yako mwezi mzima halafu uje na kuku mmoja tu???? huo ukarimu au kutafutana ubaya? Kama unayemtembelea yuko mambo safi basi shaka ondoa hata huyo kuku usibebe ila ujiandae kusaidia kazi za hapo nyumbani tuu.
 
Tabu sana

mi nakwambia Kongosho kwa umri wangu huu na uzoefu nilionao msimu wa likizo hasa wa mwisho wa mwaka kwa wengine ni msala. Tena wengine hawasubiri uwatumie nauli anakuja anakwambia nimnekopa na kwasababu hataweza kuondoka kwako bila wewe kumpa nauli utajikuta na madeni yake umemlipia nakwambia sjui dawa ya tatizo hili ni nini? Labda mkuu Mtambuzi aka baba Ngina aje atueleze cha kufanya usijekuta lile kabila wanaloenda kwqao kuhesabiwa kila ifikapo mwisho wa mwaka wanakwepa wa kijijini wasije mjini na sikukuu kijijini haina gharama kama ukifanyia mjini, hii nina uzoefu nayo. Nahisi kwa baadhi ya familia msimu huu ni tatizo kwa watu wengi ndo maana wizi hauishi na ufisadi ili uweze kukirimu wageni wako na familia kwa ujumla.
 
sisi masingle ni full kujiachia,!
hakuna cha ada wala nepi ya mtoto mwakani
hapa nafikiria niende nchi gani kujiliwaza na maswahibu yalonikuta mwaka huu

kunamasingle mjini hapa wabaya kwa timing yaani yeye ananyumba kama kumi tofauti anatime ile saa saba mchana kila kitu mezani huyu hapa halafu ile umesema karibu tuu ya kuingia ndani yeye keshakaa mezani na sahani keshashika chezea kilo ya unga now 1,300= na mchele mzuri kilo 2,000= na usiku bachelor huyu saa mbili sharp yuko nyumba ingine wanatime mida ya misosi tuu akishapakia anaanza kuwa busy na simu hata vyombo hasaidii kuosha wala kuondoa anakaa kwenye kochi na kusikilizia shibe mara anajifanya simu haisikiki vizuri mara anaaga anasepa. Kuna bachelor wabaya mjini ahapa wanalipia kodi ya kulala tuu kula kwa akili.
 
sisi masingle ni full kujiachia,!
hakuna cha ada wala nepi ya mtoto mwakani
hapa nafikiria niende nchi gani kujiliwaza na maswahibu yalonikuta mwaka huu

Wewe shangilia tu wakati ni wako
Ipo siku jambo kama hilo litakukabili ndipo utaanza kuutafuta huu uzi wa Sakapal...tuombe maisha marefu tu......!:becky:
 
Hivi umeniona???

Yaani Sakapal, you must be a witch!

Watu wanakuja, wanataka na nauli uwalipie, na hela za kulipa madeni huko waliko uwatumie
Na wakija kwako maisha yaendelee kama kawaida bila kusahau vi-outing vya hapa na pale.

Kweli situmii mtu hata senti tano, anayeweza na ajilipie, Shabashhh!

dah pole mwaya..........

Mie ndo maana nimepiga biti wageni wa mwisho wa mwaka.....

Hata wakisema nina roho mbaya poa tu
 
mi nakwambia Kongosho kwa umri wangu huu na uzoefu nilionao msimu wa likizo hasa wa mwisho wa mwaka kwa wengine ni msala. Tena wengine hawasubiri uwatumie nauli anakuja anakwambia nimnekopa na kwasababu hataweza kuondoka kwako bila wewe kumpa nauli utajikuta na madeni yake umemlipia nakwambia sjui dawa ya tatizo hili ni nini? Labda mkuu Mtambuzi aka baba Ngina aje atueleze cha kufanya usijekuta lile kabila wanaloenda kwqao kuhesabiwa kila ifikapo mwisho wa mwaka wanakwepa wa kijijini wasije mjini na sikukuu kijijini haina gharama kama ukifanyia mjini, hii nina uzoefu nayo. Nahisi kwa baadhi ya familia msimu huu ni tatizo kwa watu wengi ndo maana wizi hauishi na ufisadi ili uweze kukirimu wageni wako na familia kwa ujumla.

tatizo hao wageni mnawakirimu sana.....

Asubuhi wanywe uji, mchana upite wima na usiku wapige dona na mchicha mwezi mzima...... No outings, wafanye kazi sanaaaaaaaaa.......Akiondoka unamkatia tiketi, unampa nauli alokopa na sha 3000 ya kula njiani uone kama atarudi....
 
Christmas is a time for me to relax, put my feet up and spend my hard sweaty bloody money. Sasa tena wageni kwani yerusalemu hapa? Encourage people to spend christmas with their loved ones jamani, sio kwa watu!
 
Back
Top Bottom