hekimatele
JF-Expert Member
- May 31, 2011
- 9,889
- 2,799
hii inanikumbusha enzi zile niko praimari pale msimbazi mseto nagonga hogo la haja saa nne asubuhi. Maisha enzi zile za Mwinyi yalikua mdebwedooooooooo
Paloma nasikia eti makungu ukila lazima genye zipande kwa wadada, hivi zile zilikua story za mtaani au ni uhalisia mpaka leo inatokea? Nadadisi tuhahahaaa makungu.....yanajaa mfuko wa addidas madaftari yanashikwa mkononi
Bujibuji kwli wa kale. Umenikumbusha mbali sana. Mabumunda.....Ukotoka kwenye vibama, unaenda kwenye vitindi na masasati, na baada ya hapo unaenda kwenye mabumunda.
SokoineIlianzaga hivi kipindi hicho cha miaka ya 80 na mwanzoni mwa 90. "Kariakoo nauli shilingi TANO", baadaye ikawa Kariakoo nauli "Dala", na hatimaye Kariakoo nauli "dala dala", hatimaye tena Kariakoo "dala dala", mwishowe DALADALA mpaka leo! Hiyo ndiyo inayoitwa "Dala" na ndiyo imeleta jina la dala dala!
Sokoine
Paloma nasikia eti makungu ukila lazima genye zipande kwa wadada, hivi zile zilikua story za mtaani au ni uhalisia mpaka leo inatokea? Nadadisi tu
Yaani, nilikuwa naizungushia lile ganda la sigara la kama aluminium vile halafu naisugua kichwani, hizo picha zote zinatokea kwenye hilo ganda, halafu narudia na upande wa pili, na mwisho naibandika kwenye kiubao kilichokatwa kama shilingi tano... baada ya hapo ni kuwadanganya watoto wenzangu kuwa nina shilingi tano..
hahahaa........unasikia.....huna uhakika!!!
we mtafutie wifi hayo makungu umpe ale afu uje utapata jibu!
kisha nitafute nikwambie zaidi!
Kwa nini nisianze na kukutafuta halafu ndo niingie step one?
tehe tehe tehe tehe.......
ukiwa na hiyo unapata banzoka shi1, mihogo na juice sh2 na icecream za kumwaga, yani full kujichana siku hiyo, kwani wenzio wanakuomba nawe unawaringishia vitu vyako
Yaani, nilikuwa naizungushia lile ganda la sigara la kama aluminium vile halafu naisugua kichwani, hizo picha zote zinatokea kwenye hilo ganda, halafu narudia na upande wa pili, na mwisho naibandika kwenye kiubao kilichokatwa kama shilingi tano... baada ya hapo ni kuwadanganya watoto wenzangu kuwa nina shilingi tano..
Mbute za mihogo au kuna mbute nyingine?????nakumbuka "VIBARAGARA" na "MBUTE"........