Hii inakukumbusha nini?

Hii inakukumbusha nini?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,579
Reaction score
161,430
999577_614584258562181_1131377152_n.jpg
 
Nauli ya dala-dala..!! wala sio miaka miingi iliyopita, sasa hivi ni 100 times as much..!!
 
Da! siku ukiwa na hii kitu shule walikuwa wanakukomaje aisee, ashikrimu ilikua sh 1, bagia shilingi pia, kwa hiyo ukiwa na dala kama hivi wewe ni Bakhresa kabisa kabisa. Ila zaidi mimi inanikumbusha mwanzo wa madala dala mjini, madala dala yalianza wakati nauli sh 5 na ndio mwanzo wa neno dala dala, maana sh 5 (Kama ilivyo kwenyepicha hapo) ilikuwa inaitwa Dala!
 
Lo! nakumbuka nauli ya uda ilikuwa sh moja na magari binafsi yakaruhusiwa kutoza sh tano, wakati huo iliitwa dala (sijajua kama ililingana na dola). Makonda wa magari hayo ya binafsi wakawa wanatangaza hiyo bei ya sh tano, kuwa usiingie humu bila dala! Ili kuita abiria wakawa wanatangaza - Dala Dala! Dala Dala!
 
Ushakia kitu inaitwa Kibama au Vibama.

Bagia mkuu....duuu those dayz bana, we acha tu, ukiwa nayo hiyo skonga mihogo inakukoma, enzi za kuweka uketo (bisi) kwenye chupa na kuyaloweka....nakumbuka zamani sana...enzi za chachacha na kodrai...suruali zilikuwa zimeandikwa tokyo....duuuu na masharti yana picha ya dola kwenye mifuko...kitu special hicho...sikukuu haipiti bila DH na Romario then maradona....DO YOU REMEMBER?
 

Ilianzaga hivi kipindi hicho cha miaka ya 80 na mwanzoni mwa 90. "Kariakoo nauli shilingi TANO", baadaye ikawa Kariakoo nauli "Dala", na hatimaye Kariakoo nauli "dala dala", hatimaye tena Kariakoo "dala dala", mwishowe DALADALA mpaka leo! Hiyo ndiyo inayoitwa "Dala" na ndiyo imeleta jina la dala dala!
 
hahahaaa makungu.....yanajaa mfuko wa addidas madaftari yanashikwa mkononi
 
Back
Top Bottom