Hii Inakuhusu Wewe Mwana Jamii Forums,..

Hii Inakuhusu Wewe Mwana Jamii Forums,..

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
21,369
Reaction score
27,784
Habari wana Jamii Forums,..

Kuna Jambo limenitokea Hii Ni Mara Ya Pili Kama Siyo Ya Tatu.

Kuna Hizi Public Computers Tunazozitumia Internet Cafe Kuingia Au Ku-Login In Kwenye Social Forums Mbalimbali Kama Vile Jamii Forums, Facebook And The Likes,..

Leo Nyakati Za Jioni Nikiwa Katika Shughuli Zangu Internet Niliamua Kuingia Jamii Forums, Ile Ku-google Tu Jamii Forums Ikaja Page Tiyari Ina User Name Na Password.

Alikuwa Ni Mwana-JF Mwenzangu Aliyesahau Ku-Log Out Alipomaliza Shughuli Zake, Kwa Sababu Sikuwa Na Nia Ya Ku-hack Nili-Log Out Then Nikaendelea Na Mambo Yangu Kwa Kutumia Akaunti Yangu,.

Nafahamu Wengi Wanakumbwa Na Hili Hata Katika Forums Nyingine, Na Hii Hutokea Pale Mtu Anapo-Log In Na Ku-tick Ile Sehemu Ya Remain Log-In,.

Mwana-Jf epuka Kuweka Alama Ya Tick Kwani Hata Kama Utamaliza Kutumia Forum Atakapokuja Mtu Mwingine Anaweza Kutumia Akaunti Yako Bila Wewe Kujua Na Akafanya Chochote Atakacho Hata Kama Ni Kibaya,

Ni Hayo Tu Wana-Jf, Tuzingatie Kwa Ajili Ya Privacy Na Usalama Wa Akaunti Zetu Mitandaoni!!
 
Asante chakii a.k.a chalii
 
Last edited by a moderator:
watu wahack hata kwa kutumia ID hizi hizi na tunavunga tu
 
Asante kwa ushauri mzuri jamani kuweni makini na watoto wa kijitonyama watawang'oa meno na makucha bila ganzi.
 
Kuna mwingine huwa anasahau kulog out kwenye cafe iliyopo pale Karibu na Open University Mpanda.

Nishawahi kukuta hivyo kama mara 3.
 
Ushauri mzuri asante

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom