Hii imekaaje?

Hii imekaaje?

Ustaadh

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2009
Posts
413
Reaction score
20
Hivi huu utaratibu wa 'mjeshi' kusimama nyuma ya Rais ni utaratibu 'tuliojiwekea' au ni matokeo ya kurithi kutoka kwa wakoloni? Yaani hata kama anaongea lazima 'mjeshi' asimame nyuma yake?

Kuna ulazima kweli kwa huyu 'mjeshi' kusimama wakati 'wanene' wanaongea kama ilivyo hapo kwenye picha?

10_10_xmrt35.jpg
 
ulazima siuoni kama rais yupo kwenye security zone, labda wana maana nyingine ya uwepo wa huyo bodyguard. Kuna maswali pia huwa najiuliza, huyu jamaa ana familia? na kama anayo huwa anasafiri na mkewe pindi presida anapokuwa nje ya nchi au mikoani maana naona muda mwingi wanakuwa ni watu wa kusafiri tu.
 
Hivi huu utaratibu wa 'mjeshi' kusimama nyuma ya Rais ni utaratibu 'tuliojiwekea' au ni matokeo ya kurithi kutoka kwa wakoloni? Yaani hata kama anaongea lazima 'mjeshi' asimame nyuma yake?

Kuna ulazima kweli kwa huyu 'mjeshi' kusimama wakati 'wanene' wanaongea kama ilivyo hapo kwenye picha?

View attachment 15940

ulazima upo kwa maraisi wagonjwa, ambao muda wowote ataanguka, hivyo jamaa anakuwa na kazi ya kumdaka
 
Ulazima upo mkuu si unajua rais huwa anaanguka sasa asipo simama akianguka nani atamdaka?
 
Ni utaratibu tu waliojiwekea wanene, hapo nyuma ana makabrasha kama 'mnene' atataka ku-desa kidogo.
 
Back
Top Bottom