Slim5
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 28,440
- 38,437
Morning wana JF!
Mwenzenu kuna kitu kinanipa shida akilini! Naamini wengi wa members humu hawafahamiani kwa sura! Humu JF mimi kila siku najihisi kama nawasiliana na watu ambao tunafahamiana vizuri, yaani akili yangu inawaza kwamba watu wa humu tunajuana, haitaki kukubali kuwa wana-JF hawajuani kwa sura! Bahati mimi nilikutana na Mwana-JF mmoja tu, tena mara 1 tu, kuna biashara ilikuwa tufanye lakini hatukufikia muafaka! Kuna baadhi ya posts huwa zinafurahisha, zingine zinahuzunisha, mimi hizi huwa zinanipa hisia kuwa hawa watu wapo karibu sana! Hata michango ya members pia, kuna wakati nacheka, kuna wkt naumia, naamini kabisa kuna ukaribu, japo kwa macho nakataa!
Zaidi ya huyo, sijawai kukutana na member yeyote yule wa JF!
Hii hali inaniathiri hata ninapotaka ku-post uzi wwt ule, najikuta natumia muda mwingi sana wa kufikiria kuwa nitume ama nisitume! Kwa mfano last week nilipost kuhusu uhusiano wangu na mzee, unaweza usiamini, ule uzi niliuandika na kukaa nao kwa muda wa wiki 3, kabla sijaamua kuupost!
Jamani hili kama ni tatizo, tunaliitaje? Ni nini hiki?