Bigbootylover
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 2,847
- 1,826
Nakumbuka wakati nikiwa mdogo, tulikuwa mimi na mdogo wangu tukaokota shilingi hamsini, ilikuwa inakutukutu hivi ila hatukujali sana, tukaenda kununua big G au jojo wengine huziita. Mimi ndio niliikota ile hela, dogo alikula jojo tu, ila cha ajabu kesho yake tulitokwa na vidonda hasa mimi niliyeokota ile hela, dogo vilikaa kidogo vikapona ila mimi nilihangaika sana, nakumbuka MAMA YANGU alihangaika sana kunitafutia dawa mahospitalini, nilichomwa sindano sana ila vidonda au majipu yale yalikuwa yakikauka kidogo then yanarudi tena. Ilifikia kipindi nikavaa nguo wakati wa kuvua nguo inagandana na yale madonda yenye usaa, ilikuwa shida sana kuvua nguo. Mama hakukata tamaa alizidi kunitafutia dawa bila mafanikio, hadi ikafikia tukahamia sehemu nyingine ambapo mama alizoeana na bibi mmoja na alimueleza pia kuhusu tatizo langu, basi yule bibi akamwambia mama, nichukue pia hela yoyote kichele kama ambavyo mimi nilivyoiokota ile shilingi hamsini ya shilingi, kisha nikamue jipu au donda moja, ule usaha na damu ya kile kidonda niupakae katika ile shilingi then nikaitupe njiapanda. Basi nikafanya hivyo, haikupita hata wiki moja vile vidonda vikaanza kukauka na hatimae nikapona kabisa. Aiseeee, mpaka kufa kwangu sintokuja kulisahau hili swala japo mpaka leo huwa najiuliza maswali mengi sana, TUWACHUNGE NA KUWAONYA WANETU KUHUSU KUOKOTA OKOTA HELA HASA SHILINGI HIZI HOVYOHOVYO. Mpk leo huwa nikitembelea yale maeneo nikikaa sana, nikijikuna upele, unaweza kutengeneza jipu tena, hii sijui inakuwaje. DUNIA INA MAMBO