Hii Imekaaje Wakuu?

Hii Imekaaje Wakuu?

Marco Polo

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2014
Posts
13,594
Reaction score
21,793
Mzee wangu ananiambia alinunua kiwanja huko Kibaha, sasa juzi kati wakapewa taarifa kwamba kwa yyte ambaye hajaliendeleza hilo eneo serikali italichukua , hivyo imemlazimu kuanza ujenzi wa haraka haraka, ninachotaka kujua hivi inawezekana mtu ukajenga sehemu ambayo huna hati miliki yake? Maana anasema alilipia wilayan lakin hawakumpa hati miliki isipokuwa wakimwambia wanalifuatilia suala lake maana mkuregenz aliyekuwepo wakati analipia hayupo tena.


Mm Niko mbali na Dar nataka kujua tu kuhusu haya mambo maana usije mtu ukatuma fedha mwisho wa siku mnakuja aambiwa mmevamia eneo.
 
Majibu yapo huko upimaji na ramani/Kibaha,hapa tutakuletea porojo tu,mwambie mzee aende na vielelezo vyake vyote vya malipo na umiliki wake wa halali wa hilo eneo,atasaidiwa..
 
Fatilieni hatimiliki kwanza tafadhali,msije lia kilio cha mtu mzima...na hiyo shughuli mnayoifanya iacheni mara moja...

Mali bila daftari hupotea bila habari.
 
Fatilieni hatimiliki kwanza tafadhali,msije lia kilio cha mtu mzima...na hiyo shughuli mnayoifanya iacheni mara moja...

Mali bila daftari hupotea bila habari.
Hich ndicho nilichomshaur mzee, ila naona ni mgumu kunielewa na pia nimesita kumtumia pesa
 
Ninawajua watu zaidi ya elfu 1 waliojenga maeneo yasiyo na hati

Ninachojua mimi kibongobongo ni maeneo machache sana yaliyopimwa, sembuse yenye hati

Kwa kawaida (Watanzania wengi)tumezoe kujenga sehemu isiyopimwa, kisha mradi wa upimaji ukija katika eneo husika ndio tunapima kisha tunatafuta hati

Kama maeneo jirani na eneo la mzee yana hati lakini eneo la mzee halina hati, hapo shtuka...... Vinginevyo hilo eneo ni salama cha msingi awe na nyaraka za ununuzi wa eneo husika
 
Back
Top Bottom