Hii imekaaje wadau?

ankol

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2012
Posts
2,724
Reaction score
5,291
Habari zenu wadau.
Hivi ni kwa nini mara nyingi inatokea endapo utamwacha yule mwenza wako ambaye mmesota sanaa kimaisha then baada ya mambo kukuendea vizuri ukaamua kumuacha na kwenda kuanza relationship na mtu mwingine basi maisha yako yataporomoka sana?
Nina mifano mingi ya watu mbalimbali hapa mtaani kwetu amabo imewatokea hali hii.
unafikiri ni kwa nini?
 
yule anayeachwa anaumia sana anakuwa na uchungu mwingi moyoni, ogopa mtu unayemtendea ubaya anakwambia anamwachia Mungu! hukumu itakayotoka ni stahiki!
 
kinyongo kibaya sana,hasa mtu akikuwekea bila wewe kujua
 
Wala hamna lolote. Ujingaa huo huo unaopelekea umuache mwenza wako ndo ujingaa huo huo unaokupelekea kufilisika
 
Inawezekana tu kama unayemuacha ndio mtunza vitabu...mpanga mipango na ndo mwenye mtaji
 
Wengine hua na mikosiiii baki njia kuuu
 
yule anayeachwa anaumia sana anakuwa na uchungu mwingi moyoni, ogopa mtu unayemtendea ubaya anakwambia anamwachia Mungu! hukumu itakayotoka ni stahiki!

haisee!
 
Kwani kabla hujawa naye si ulikuwa mchovu tu kimaisha.Baada ya kuwa naye mkasota mka-win maisha.Sasa ukimuacha unapaswa kurudi kulekule kwenye msoto kwa kuwa si akili yako peke yako iliyokufanya u-win.Huwezi kutumia wenzako kama ngazi halafu nature ikuache hivihivi ebo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…