Hii imekaaje? ukimuhitaji hakuhitaji na usipomuhitaji anakuhitaji

Umenigusa mkuu. Mimi nina 27 yrs nilikuwa natoka na mkaka mmoja ofisini,anakuja kwangu analala na mimi hivyohivyo kwake. Amesubiri nimeenda likizo akamuengage his long time girlfriend bila mimi kijua,nilosema ngoja nimchungulie insta ndo nakutana na mapicha. Aysee nimeumia mnoo nimekata tamaa kwani naona umri ushaenda, nanilikuwa namtegemea tuane. Naumia mno kola nikimuona mbaya zaidi yupe naye ofisi moja. Nimetoka likizo kaja kwangu kaniongelesha wee na sababu zisizoeleweka nikajikuta nafanya nae tena mapenz, naomba mnisaidie jinsi yakujitoa jamni. Kwani nashindwa kumove on,wakati tayati yeye amechumbia.

Masikin!sijui nikwambie maneno gani ya kukutuliza.Ila jitahid ukae mbal na huyo mtu kwan ataendelea kukupotezea muda mamaa
 
Mimi nina principal rahisi sifanyi mchezo kwenye mapenzi nikigundua unacheza game na switch off moyo wangu kimapenzi.
 
upande wangu mtu akishaanza kuzingua tu, aisee simcheleweshi..
anasepa zake coz ckuzaliwa na m2. Heri kuwa alone.
 
Umenigusa mkuu. Mimi nina 27 yrs nilikuwa natoka na mkaka mmoja ofisini,anakuja kwangu analala na mimi hivyohivyo kwake. Amesubiri nimeenda likizo akamuengage his long time girlfriend bila mimi kijua,nilosema ngoja nimchungulie insta ndo nakutana na mapicha. Aysee nimeumia mnoo nimekata tamaa kwani naona umri ushaenda, nanilikuwa namtegemea tuane. Naumia mno kola nikimuona mbaya zaidi yupe naye ofisi moja. Nimetoka likizo kaja kwangu kaniongelesha wee na sababu zisizoeleweka nikajikuta nafanya nae tena mapenz, naomba mnisaidie jinsi yakujitoa jamni. Kwani nashindwa kumove on,wakati tayati yeye amechumbia.

I really wish niku-PM kukuuliza jambo.
 
Mawasiliano yakizidi sana na kupitiliza kiwango cha kawaida yanageuka kero, tena kero hasa. Kuna wakati huwa nahisi ni utoto. Tokea asubuhi ni mwendo wa meseji tu hamna kupumzika, mara "ooh ndo nakunywa chai now" hujamaliza kuisoma inaingia nyingine "bby i mic u" bado hujajibu mara katuma nyingine "honey mbona hujibu text zang" sasa baby nitajibu vipi na wewe unatuma bila mpangilio?
Kutokujibu au kuchelewa kujibu haimaanishi kuwa hunivutii la hasha, ila nina mambo mengi ya msingi kuliko kuchat na kutumiana picha za vyakula.

sasa mwanamke kama huyu anapoona unazembea kumjibu ndo anahisi humpendi, umemchoka na umepata mwingine bila kufikiri anaamua kukupoteza. kwa kuwa bado unamuhitaji sana na huenda una malengo makubwa kwake unaanza kuwa karibu yake zaidi na zaidi kuliko ilivyokuiwa mwanzo kwa kuwa bado unamuhitaji.

la msingi ni kuzungumza kila mmoja amuelewe mwenzake na muweze kuishi kulingana na matwaka yenu.
 
Kuna watu pia kwa makusudi wanapenda kuplay games na hisia za wapenzi wao!!sijui ni kwa vile inawapa excitement au inaleta burudani fulani katika akili zao!!Unaweza ukakuta mpo vizuri tu akaanza kuact kama anapunguza mapenzi au anataka kukuacha kabisa,ni kama anakupa kihoro aua anakutest!Basi na wewe kwa kuogopa kuachwa coz kuachwa kunauma isitoshe ukiwa unampenda mtu ni uchungu zaidi,utajikuta unatunia nguvu,ushawishi na mahaba mazito umrudishe chini ya himaya!!Unfortunately akirudi unafeel safe na unaona ni wakati muafaka wa wewe kumtingisha yeye au ikiwezekana kumwacha kabisa,sasa sijui kama ni mapenzi,kisasi au kamchezo!Ikitokea umekosea sasa,umetikisa kiberiti afu yeye akaitika mazima ndo utalia na Mola!!Ila all in all kuna watu wepesi sana kukinai wenzao...na wanapenda attention na kupendwa sana ukipunguza tuu,Anaona humpendi.
 
Halafu hii dhana ya kusema hupaswi kumuonyesha mapenzi mazito mwandani wako inatoka wapi? Huu ni mtazamo wa wanawake wengi sana na najua hata humu JF wamo (sijasema kuwa wanaume wenye mtazamo kama huu hawapo)

Wana hoja yao kuwa ukimuonyesha mapenzi ya dhati atakusumbua! Hii hoja kwangu ni nyepesi sana. Inakuaje mtu aanze kukusumubua eti kwa kuwa umeonyesha kumpenda sana? na hakika akifanya hivyo basi huyo hakufai na ni bora ukachech ustaarabu mwingine kabla hujapoteza muda wako.

Kama upo kwenye mapenzi yanayokunyima uhuru wa kuonyesha hisia zako basi upo katika utumwa, ndio kinyume cha uhuru ni utumwa. Kwanini ukubali kuwa mtumwa? kwanini umpende mtu ambaye unahofia kumdhihirishia ipendo wako? sasa kuna faida gani ya kuwa kwenye mahusiano ya mtindo huo?

mapenzi ni kuwa huru kwa yule umpendaye na uhuru huo unapokosekana inakuwa utumwa. KUWA HURU SASA EPUKANA NA UTUMWA
 
Masikin!sijui nikwambie maneno gani ya kukutuliza.Ila jitahid ukae mbal na huyo mtu kwan ataendelea kukupotezea muda mamaa

Asante wangu. Yani sina amani,nimejifunza kitu kikubwa sana kwe maisha. Imagine ninakazi nzuri tu kwe sector nzuri, kwani nilibahatika kupata kazi mqpema tu baada ya kumaliza chuo, yani kwa matazamo wa nnje mtu akiniona atasema mmh huyu dada hana shida kabisa, kumbe mmh nikifika nyumbani kwangu ni kulia tuuu,ninalala saa chache mno,pakikucha najiandaa naenda ofisini hakina mtu anayejua,tatizo ni lazma nimuone ofisini yeye anacheka anafurahi ila mimi moyoni natamani kufa. Daah maisha hayaa. Sina hamu. Nilitaka kwenda kwetu kwajili ya sikukuu ila nimepungua mnoo nahofia nikienda maswali yatakuwa mengi. Maisha ni zaidi ya tunavyofikiria watu wengi.
 
Mawasiliano yakizidi sana na kupitiliza kiwango cha kawaida yanageuka kero, tena kero hasa. Kuna wakati huwa nahisi ni utoto. Tokea asubuhi ni mwendo wa meseji tu hamna kupumzika, mara "ooh ndo nakunywa chai now" hujamaliza kuisoma inaingia nyingine "bby i mic u" bado hujajibu mara katuma nyingine "honey mbona hujibu text zang" sasa baby nitajibu vipi na wewe unatuma bila mpangilio?
Kutokujibu au kuchelewa kujibu haimaanishi kuwa hunivutii la hasha, ila nina mambo mengi ya msingi kuliko kuchat na kutumiana picha za vyakula.

sasa mwanamke kama huyu anapoona unazembea kumjibu ndo anahisi humpendi, umemchoka na umepata mwingine bila kufikiri anaamua kukupoteza. kwa kuwa bado unamuhitaji sana na huenda una malengo makubwa kwake unaanza kuwa karibu yake zaidi na zaidi kuliko ilivyokuiwa mwanzo kwa kuwa bado unamuhitaji.

la msingi ni kuzungumza kila mmoja amuelewe mwenzake na muweze kuishi kulingana na matwaka yenu.
aisee umenichekesha Sana Asante kwa kunifurAhisha simu Yangu
 
Asante wangu. Yani sina amani,nimejifunza kitu kikubwa sana kwe maisha. Imagine ninakazi nzuri tu kwe sector nzuri, kwani nilibahatika kupata kazi mqpema tu baada ya kumaliza chuo, yani kwa matazamo wa nnje mtu akiniona atasema mmh huyu dada hana shida kabisa, kumbe mmh nikifika nyumbani kwangu ni kulia tuuu,ninalala saa chache mno,pakikucha najiandaa naenda ofisini hakina mtu anayejua,tatizo ni lazma nimuone ofisini yeye anacheka anafurahi ila mimi moyoni natamani kufa. Daah maisha hayaa. Sina hamu. Nilitaka kwenda kwetu kwajili ya sikukuu ila nimepungua mnoo nahofia nikienda maswali yatakuwa mengi. Maisha ni zaidi ya tunavyofikiria watu wengi.

pole sana jamani mi nachoweza kukushauri ni kuachana na huyo kaka hana aibu kwanza ni mvurugaji yani tayari ameshamvisha mtu Pete na bado anakuja kwako hana haja na wewe kama angekuwa anakuhitaji angekuvalisha wewe ameshakufanya kama kipoozeo chake cha kutuliza ashki zake za muda cha msingi achana nae kabisa acha kumchekeachekea kuwa serious na msimamo mmoja najua inauma na itachukua muda lakini hilo ndo la kufanya anaweza kukuzibia rizki ukakosa mtu wa kueleweka kwako sababu yake wakati mambo yake yanamuendea vizuri....... pole sana yatapita kuwa mvumilivu ila usikubali tena aje kwako
 
Asante dia. Nitalifanyia kazi hilo.
 
Dont chase people.Be yourself,do your own thing and work hard.The right people-the ones who relly belong in your life-will come to you.And stay.
 
Kheeeee himidini ni ustadh??????? ....ukimaanisha kwamba salamu hizi hazimuhusu au

Unadhani kila mtu ni mgalatia??
ثسففييءث اللسءشتهىي اتتؤيليء اؤيؤنني لباخاختيقهر اتهيينه فبهخنبش نتتبغ.
 
Back
Top Bottom