Hii imekaaje toka Igunga kusanyiko Dar?

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,882
Wana JF nimeshindwa kuelewa kwamba sherehe kubwa imekuja kufanywa Dar badala ya Igunga.

Pia CCM wana Wabunge 200 plus bado wanazunguka kuandamana juu ya wiz wa Igunga. Can anyone tell me kuna siri gani hapa Mmemsikia Nape akibwabwaja na wajinga wenzake eti Upinzani na kumwaga damu. Jamani hayo mambo yamekaaje? Umemsikia Nchemba anasema Chadema wasingaliweza kupata kura hata 1,000 bila ya kusaidiwa na Tume kweli hao waalimu ni 23,000 hapo Igunga ? Hii imekaaje ?
 

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,666
2,179
Fedha inaongea ie ufujaji wa fedha za walipa kodi kwa mgongo wa chama
Yaani wameona Igunga sio sehemu ya kufanya sherehe ukiona ivyo wanajua hawakubaliki kule as wameforce king
 

measkron

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,782
2,399
wamedanganyika wasubiri ahadi za Maji toka ziwa Victoria na daraja toka kwa Waziri Magufuli, wataendelea kusota walipewa ubwabwa wao kuhongwa so hawahitaji kufanyiwa sherehe....ingawa kura wamepiga wao
 

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
8,173
3,331
Ujue kuwa Igunga ilikuwa ni zaidi ya uchaguzi, lakini jibu lako ni simple kabisa wanataka kuuthibitishia umma kuwa chama bado kina nguvu ya kuweza kushinda hata chaguzi nyingine.
 

kajunju

JF-Expert Member
Jun 30, 2011
999
315
sherehe hii wasingefanyia igunga. wanggezomewa sana.wameleta kwa watu wa dar waliochoka, wanaoshindia chips dume na wakawapa buku mbili hadi tano wakakusanyika.watu wa igunga wametumiwa kama used co...nd..mss
 

mwanapolo

Senior Member
Mar 29, 2011
193
55
Wameifanya hiyo sherehe Dar sababu upelelezi wao umegundua kumbe Igunga hawana sapoti kabisa, pia waliona kuna dalili ya kupopolewa mawe, kwani wanaigunga ndo wamestuka sasa kuwa hata mgao wa chakula cha njaa umekata.
 

MKANDYA

Senior Member
Aug 12, 2009
166
17
Hii ni kukuonyesha kuwa huyo mbunge si wa Igunga, hivyo wana Igunga wameliwa. Watamwona tena wakati wa uchaguzi.
 

TIMING

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
22,825
8,642
ukiona watawala wanaacha shughuli zao na kukutana juani kujipongeza kwa kushinda kwa asilimia sita, kwenye jimbo ambalo ni ngome yao, tena kwa kutumia mabilioni, bunduki na kutia wake za watu, bsi ujue kuna shida kubwa ya kiutawala

Ombwe lililopo linaweza kumalizwa kwa bakora, laikti wangejua mitaani kwetu vijana wana hasira sana, wangekaa kimya tu na kujenga taifa

na mzee wa karolite (Nape) nadhani hajui anachofanya, ana mawili tu, either awe na exit ya nchi iko sawa au ajiandae kuoga mafuta ya taa kwa kauli zake chafu.... he has to learn kwamba internal energy among tanzania youths is unbearable
 

TIMING

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
22,825
8,642
Hii ni kukuonyesha kuwa huyo mbunge si wa Igunga, hivyo wana Igunga wameliwa. Watamwona tena wakati wa uchaguzi.
well said, sasa wanaosha vyombo, pilau limeisha na serikali imerudi kwao
 

MAMA POROJO

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
4,977
775
Hali ya CCM Igunga ni mbaya sana, hadi sasa wajumbe 18 wa ccm wamejiuzulu, wananchi wenye njaa wanasubiri mahindi ya msaada Machemba na watu wake hawaonekani tena, ofisi za ccm zimefungwa wakihofia hasira za wananchi. Igunga siyo salama kabisa kwa mbunge mpya wa ccm.
 

Oxlade-Chamberlain

JF-Expert Member
May 26, 2009
8,635
2,186
Pesa wanazotumia kusheherekea ushindi wa igunga bora wangeenda kuwajengea visima vya maji na mashimo ya choo.

Wana Igunga wenyewe wamerudi kwenye maisha yao ya kila siku ya kutaabika kwani pombe walizobadilishana na kura zao zishawaruka kichwani sasa na nyama walizokula ndio hivyo tena wasubiri uchaguzi ujao.
 

THINKINGBEING

JF-Expert Member
Aug 9, 2010
2,779
1,303
Igunga walishapewa pilau yao na pombe saivi ni zamu ya maeneo mengine.
Kaeni mkao wa kula.Watu wote lazima mpate pilau.
CCM YAJENGA NCHI.
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom