Hii imekaaje, AK Waafrika Hawataki Kiafrikaans lkn wanataka English!


Afrikaner si lugha ya Kiafrika. Ni lugha ya makaburu. Makaburu kwa jina jingine huitwa Afrikaners
 
Mkuu wale wameathirika na ukabila bora lugha ya malkia tu
 
Mkuu...tanzania tulishapata ukombozi...ama kweli Benja hakukosea alivyowaita malofa na wapumbavu
Ukombozi upi kijana??????siye watanganyika tulichokifanya hiyo miaka ya 60 ni kubadili white exploiters(colonialist) master to black exploiters tu and not otherwise......
 



Ndiyo maana nimekwambia jaribu kwanza kujisomea Historia ili uelewe haya mambo na uache kulishwa!
Apartheid AK haijaanza 1948 ila jina Apartheid ndiyo limeanza kutumika mwaka 1948, lkn mfumo wa Ubaguzi wa rangi AK umeanza zamani sana tangu miaka ya 1800 huko kulikuwa na kitu kinaitwa pass law na pass law iliasisiwa na Waingereza chini ya akina Cecil Rhodes na wenzake sasa sijui unachobisha ni nini hapa? Na pass law ndiyo mzao wa Apartheid tofauti ni jina tu!

Na Waingereza ndiyo waliyoipromote Apartheid system siku zote mpaka siku za mwisho Mandela anaachiwa alikuwa kwenye terrorist list ya Uingereza na Marekani, kwa lugha rahisi mandela alikuwa ni gaidi au terrorist kwa Waingereza na Marekani kama vile alivyokuwa Osama Bin laden mpaka siku anaachiwa huru Apartheid imeisha tu baada ya Thatcher (aliyekuwa Kiongozi wa Uingereza) kuondoka vita baridi kuisha na Waingereza na rafiki zake kama Marekani kukubali kuishinikiza AK ya Makaburu kuruhusu demokrasia ya wote!
 
Nikweli kabisa, ni sawa na vile sultan alitawala Zanzibar kwa niaba ya uingereza
 
Issue sio Rhodes alikufa mwaka gani, atuzungumzii mtu,tunazungumzia mfumo, ambapo Uingereza ndio sponsor
 
Kiingereza ni lugha ya dunia.
 
Ndiyo maana nimekwambia jaribu kwanza kujisomea Historia ili uelewe haya mambo na uache kulishwa!
Ni wewe siyo mimi anayepaswa kusoma Historia. Ubaguzi upo wa aina nyingi. Kwa mfano kilichotokea Afrika Kusini Mwaka juzi na kinachotokea huko Ujerumani hivi sasa ni ubaguzi lakini hauitwi "Apartheid" bali "Xenophobia" na kihistoria makaburu hawazaliwi na Waingereza bali wanazaliwa na wadachi!!

Kusema kwamba Apartheid imeanzishwa na Waingereza ni utungaji usio na maana. Apartheid ulifanyika kuwa Mfumo pale sheria ya kuwaweka watu wa Afrika Kusini katika madaraja kwa kuzingatia Rangi zao na kuweka maeneo rasmi kwa ajili ya watu kwa kulingana na rangi zao.
 
Daaahhh....nakumbuka mwalim wangu wa history alinifundish ki2 kama hiki ila kiliitwa "UTOPIAN REVOLUTION" a Mayo ilitokea Uingereza
 
Kiingereza ni lugha ya dunia.
3/4 ya watu wa SA..wanaongea lugha ya kiingereza..sasa linapokuja suala la kuwaforce wajifunze ki Afrikaans..inamaana unawakumpusha machungu ya nyuma..kwanza hiyo lugha ukiiangalia kwa umakini inakuwa sawa tu na lugha za kizulu,khosa na vikabila vingine vidogo..kwa nini ipaishwe hivyo na sio kizulu au khosa??kwanini wasitumie kiingereza ambayo ni international language..yenye faida luluki kuliko hiyo ya afrikaans ambayo ni local language!
 


Nimekwisha kwambia kwamba kabla ya Ubaguzi huko AK kuitwa rasmi apartheid ambalo ni neo la Kiholanzi/afrikaans ambalo maana yake ni kama ,,kutenganisha" kulikuwa na neno lingine au mfumo ulioitwa pass law, na halikuwa na tofauti yoyote ile na Apartheid isipokuwa walibadilisha jina tu ktk pass law kwenda apartheid na pass law ilianzishwa na Waingereza kwa lengo hilo hilo la kubagua watu kwa mujibu wa rangi na asilia yao, yaani Waafrika walikuwa wanabaguliwa na walihitaji pass kama ilivyokuwa baada ya 1948 Apartheid kwenda mahali popote pale kila kitu kilikuwa kimetenganishwa, na Watu weusi wote walikuwa hawaruhusiwi kufanya chochote wala kujichanganya na Wazungu na ndiyo maana ikaitwa pass law yaani walihitaji pass au kibali kufanya chochote kile kama vile ilivyokuwa apartheid!
 
Unawashauri wengine wakati kwenu lugha ya Universities ni hiyo hiyo English!
 
Ni lazima kuelewa kwamba hawa waafrikaans ndiyo waliokuwa wanapewa upendeleo kipindi kile cha ubaguzi..ndiyo waliokuwa wanaruhusiwa kupata elimu bora, walipewa makazi bora na ndiyo walikuwa wanaruhusiwa kwenda beach...there was no beach for black...kwa hyo kuendeleza matumizi ya KIAFRIKAANS bado inaclick kwenye vichwa vya black kwamba wanaendelea kutawaliwa....
 
Humu jf kuna watu wanajikuta wanajua kila kitu utadhani wengine hatujasoma kabisaaaa simple history ya O level mtu inampa shida wote tunajua makaburu ndio walikuwa wazungu wa mwanzo kabisa kufika AK wakaja waingereza ambao nao waliitawala sana AK lakini hatukusikia apartheid wala hakuna sehemu yoyote kwenye historia ikionyesha muingereza akitumia apartheid kama modal ya administration yake baada ya muingereza kuondoka huyu panya ndio akashika hatamu na cha kwanza kabisa ali formulate constitution iliyozaa apartheid system na moja ya mission yake ni kufanya lugha yao kuwa lugha mama huko AK
 
Sasa huyo profesa maji marefu anakuja na magazeti makuubwaa kutumalizia bundle zetu bure kabisa English is an international lingua hakuna nchi yoyote yenye hati miliki na nchi flani kutumia English kama lugha yao haimaanishi nchi hiyo inaifagilia nchi nyingine au imepotoka na wala sio suala la kuzua mjadala mkuu
 
pass law,partheid!
Ndugu yangu "Pass Law" na "Apartheid" ni vitu viwili tofauti kabisa!! Pass law hata hapa kwetu Tanzania zilikuwepo na madaraja pia yalikuwepo, watu walikuwa wanajua Bar za wazungu ziko wapi na za kwao waswahili ziko wapi, na hata Mwalimu Nyerere aliwahi kukataliwa kuuziwa bia kwenye baa iliyokuwa maalum kwa wazungu. Pia kulikuwa na maeneo ya wazungu wahindi na Waafrika, na ndiyo maana maneno kama "Uswahilini" "Uzunguni" na "Uhindini" yaliibuka. Lakini huwezi kuuita huo mfumo kwamba ni Apartheid ingawa ni Ubaguzi.

Inawezekana Pass Law ikawa ni kiashiria cha ubaguzi, lakini kunawezekana kusiwe na Pass Law na bado Apartheid ikawepo. Boston kwenye ule mgomo mkubwa wa wakazi wa mji ule uliotokana na kupinga madaraja kwenye Magari ya usafiri ambayo yalimbagua Mwafrika, lakini kulikuwa hakuna Apartheid!!
 


Embu ngoja twende pole pole kwa maana naona kama labda spidi imekuwa kubwa na kupotezana, ngoja tuanze Apartheid kwako unaielewaje? Yaani maana yake nini wanaposema Apartheid AK
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…