Hii hapa nyumba pekee ya Askofu Kakobe

Haya machuma yote kuzuia waumini wasiende kunywa chai, sitaki kuamini anajikinga na maadui maana kwa mtindo huo atakuwa na mabaunsa ikiwezekana bastola kiunoni wakati wa maombi.
 
Ewe ujiitae UMEOKOKA NA HUNA dhambi.Hayo mamlaka ya kuita binadamu alieumbwa na Mungu 'MASHETANI' Umeyatoa wapi?? Hata hivyo najua nyie ni wasanii tu bali mnatumia jina la Mungu kutapeli watu.

Hapa sijataja binadamu. Uongo hutoka kwa Ibilisi ambaye ndiye baba wa uongo (YOHANA 8:44; UFUNUO 12:9), na Ibilisi huyu anao pepo wengi wa uongo (1WAFALME 22:22-23), ambao kazi yao ni kuwadanganya binadamu. Pepo hawa wa uongo, wanaitwa pia mashetani au roho zidanganyazo (1TIMOTHEO 4:1).
 
siyo dhambi mtumishi wa Mungu kuwa na mali!!

Kwa hiyo mnataka awe maskini ili iweje sasa,.. I don't get the concept!
 
Hapa sijataja binadamu. Uongo hutoka kwa Ibilisi ambaye ndiye baba wa uongo (YOHANA 8:44; UFUNUO 12:9), na Ibilisi huyu anao pepo wengi wa uongo (1WAFALME 22:22-23), ambao kazi yao ni kuwadanganya binadamu. Pepo hawa wa uongo, wanaitwa pia mashetani au roho zidanganyazo (1TIMOTHEO 4:1).

hivi hamna pepo/roho mbaya zilizopo mbinguni?
 
Kama hayo unayosema na kuandika hapa ni kweli basi mimi binafsi natilia shaka huduma ya askofu Kakobe.
Mungu ni tajiri sana, kila kitu anacho, na mtumishi wake yeyote akiomba lolote atapata, leo Askofu kakobe amejenga nymba kabla ya kuwa mchungaji kisha askofu, na tangu apate ufunuo na kumtumikia Mungu wake amempa nini? na je anamtumikia huyu mungu mwenye nguvu mwenye kila kitu? je yeye amemuomba nini huyo mungu wake?
Labda pia unisaidie, kujua hili Je kuna sifa gani kwa mtumishi wa Mungu mwenyewe kuwaombea waumini wake na kupata mafanikio kutoka kwa huyo mungu ili hali yeye hana mafanikio? au ina maana yeye hana uwezo wa kuwaombea waumini/wafuasi wake wakapata mafanikio?

Pengine labda utuambie Askofu kakobe kuishi nyumba hiyo na wewe kuwa muumini wake wa miaka 25, inatufundisha nini?, au wewe umejifunza nini kutoka kwa askofu wako huyo? unaposema hana Hela wala nyumba (hivo hana mali zingine) zaidi ya hiyo nyumba unataka sisi tuelewe nini?, hapokei sadaka kanisani? au ana matumizi mabaya ya fedha za kanisa?, mtu wa anasa asiye penda maendeleo? hebu tuelezee kwa mapana

nakutakia ibada njema mlokole wa FGBF
SP

".......kama maskini, bali tukitajirisha wengi...." (2WAKORINTHO 6:10).
 
Semeni tu ukweli?fedha,dhahabu na vyote viijazavyo dunia ni mali ya bwana,hagai ngapi sijui?kwani ikisema ana vitu kadhaa kuna tatizo gani?sindivyo alivyobarikiwa kwani mtu kuwa na mali ni dhambi?
 
Ww sindio msemaji wake.?

Mimi siijui hiyo nyumba ya Boston, wala sijawahi kuiona. Kifupi ni kwamba hana nyumba Boston, ni maneno ya kusikia tu. Mwambie aliyekwambia juu ya nyumba hiyo ya Boston, yeye mwenyewe aiweke hapa, ili mzizi wa fitna ukatwe!!!!
 
$Billion??

Means Tshs 1,620/$ x 1$Billion?
= Tshs Trillion 1.62??
Au ulikua uinamaanishaje Mkuu??
Mara nyingi hawa watumishi feki wanaweka pesa zao ndani,wanachimba chini kisha wanatunza madola tu.Nadhani Kakobe atakuwa na dola bilioni 1.Msanii Gwajima atakuwa na dola bilioni 2 kwa maana yeye sadaka zote anatia kwapani,hataki hata kununua eneo ajenge.mama rwakatare atakuwa na bilioni 3,Yule mwenye bank atakuwa na bilioni 5,lusekelo nae yuko nyuma yao na anawakimbiza kwa hasira atakuwa na milioni 7.Waacheni wajinga waliwe,hawajazimishwa.
 
Taabu yote hii ya nini, mtumishi wa Mungu hapaswi kutenda kazi kwa kuwa wanadamu wanamnyooshea vidole iwe kwa kashfa au kheri.

Malipo huwa ni kwa Mungu, iwe unamtumikia au uwe muumini.
 
Semeni tu ukweli?fedha,dhahabu na vyote viijazavyo dunia ni mali ya bwana,hagai ngapi sijui?kwani ikisema ana vitu kadhaa kuna tatizo gani?sindivyo alivyobarikiwa kwani mtu kuwa na mali ni dhambi?

Ukweli ndiyo huu, kama siyo ukweli, basi uweke wewe hapa ukweli unaoujua.
 
Mimi siijui hiyo nyumba ya Boston, wala sijawahi kuiona. Kifupi ni kwamba hana nyumba Boston, ni maneno ya kusikia tu. Mwambie aliyekwambia juu ya nyumba hiyo ya Boston, yeye mwenyewe aiweke hapa, ili mzizi wa fitna ukatwe!!!!

Siku zote ukweli ndio huwaweka watu huru.....hakuna haja ya promo...
 
nailazimisha nafsi yangu kuamini inakataa kabisaa yani imekataa.hiyo kweli ni nyumba yake nakubali ila kwa maelezo kua ndio hiyo hiyo huenda ikawa sikweli.
 
Mtumishi wa mungu achafuriki wala kuchafuliwa.. unajua LUSEKELO MZEE WA UPAKO anaaishi wapi na anaendesha gari gani?

Hapa naona mimi ni kuwekana sawa tu.
Yule namfahamu mafanikio yake anayafahamu ye binafsi
 
Back
Top Bottom