Hii hapa Dawa ya Panya Road

Hii hapa Dawa ya Panya Road

good idea
Nikikuteua katika wadhafa fulani,siku nakuapisha nakwambia mapema.

"SIKU IKIBAINIKA UMEHUJUMU UCHUMI WA NCHI AU UMEFANYA UBADHILIFU WA MALI YA UMMA, ADHABU ZAKO NI TATU.
i) NITATENGUA UTEUZI WAKO.
ii) NITAKUFILISI MALI ZAKO ZOTE, HATA ULIZOKUWA NAZO KABLA.
iii) NAKUFUNGA JELA.

maana upuuzi wa wanasiasa unatia hasira wakuu
 
Ila tatizo jingine la dar ni life style ya wananchi wake.
Hawana ushirikiano kabisa, chako chako changu changu. Hii ni mbaya sana yani nyumba ya jirani inaweza kua inaungua na jirani mwingine yuko zake ndani tu wala hatoki kusaidia.

Ndo kama hiyo ya panya road, mtu anakatwa ngebe mchana kweupe na watu wanapita na hamsini zao kama hakitokei kitu vile.
 
Waanze na hao wachanika wapotezwe wote adabu itarudi na wazazi wataacha kuwatetea watoto wao kwenye uhalifu au kula nao
 
Hakuna kitu chechote chenye ukweli kuhusu neno PANYA ROAD Rodi Roda.

Neno hilo ni muendelezo wa Wezi na Waandamanaji wa Kibeberu,Kibepari, na wa Kimbari kutoka bara la Ulaya, ambao ni kama mbwa mwitu.
 
Swala lingine ni swala la kodi, nikiwa raisi (day dreaming) nitapunguza kodi zote za kila aina to the lowest minimum,ila kila mtu LAZIMA ALIPE KODI.

Nikitaka kwenda ziara ya eneo fulani, natanguliza wapelelezi , nikikuta kuna watu hawalipi kodi, meneja tra wa eneo hilo atavuta pumzi ya moto
 
nasikia juzi kati wamepiga tukio kunduchi yani mi nawatamani nikutane nao bastola yangu toka ninunue haijapata tukio la ku test mitambo
 
nasikia juzi kati wamepiga tukio kunduchi yani mi nawatamani nikutane nao bastola yangu toka ninunue haijapata tukio la ku test mitambo
Mkuu njoo keko,uitest vibaka wapo wa majaribuo
 
Mkuu njoo keko,uitest vibaka wapo wa majaribuo
mkuu hapo keko nna bifu nao kuna siku waliniwekea kisu shingoni walikua na bodaboda ila natamani lile tukio lijiludie tuoneshane makali
 
Hivi hao panya road katika mizunguruko yao mbona hawakatizi katika mageti ya Jeshi?
Kuna tukio moja niliwahi kusikia mtu alifanya makosa akapitia kituo cha Polisi halafu akawauliza kuwa bangi inauzwa wapi maeneo yale! Police hawakumchukulia hatua walijua kuwa ni chizi; kumbe hapana alikuwa na akili timamu isipokuwa alikosea tu kwa sababu waliokuwepo kituoni hawakuwa wamevaa sare.

Panya road wakipita maeneo ya jeshini, kama hawatafanya tukio, possibly wanajeshi wanaweza kudhani kuwa ni vijana tu wa kawaida wamefurahia amani ndani ya nchi yao. Ni sehemu ambayo panya road hawezi kufanya tukio, hata kama kuna mamillion ya fedha yameachwa nje ya geti, hawawezi kuyachukua, na kama watayachukua, basi watayapeleka kwenda kuyasalimisha mahali salama panapohusika
 
Huyajui mageti ya Jeshi wewe!
 
Huyajui mageti ya Jeshi wewe!
Unamaanisha nini? Unamaanisha kuwa panya road wanao uwezo wa kuya-access mageti ya jeshi? Basi kama ni hivyo wasogee na huko halafu tusubiri kusikia ni nini kitatokea kwa sababu masikikio tunayo
 
Hili ndilo kosa kubwa sana Hayati JPM aliwahi kufanya, kama ni kweli. Ukiruhusu hivyo huwezi kujua watu wengine wabaya wanaweza kuutumia mwanya huo kufanya mauaji; na ndiyo maana kuna maiti zilikuwa zinasemekana kuokotwa sehemu mbalimbali ikiwemo mtoni. Serikali huwa haishindwi na hivyo haiwezi kuwashindwa panya road. Njia zipo nyingi tu za kuwadhibiti
Basi nenda kituoni kawaeleze hzo njia za kuwadhibiti
 
Huwezi waamini polisi kiasi hicho.
Sio kila anayekamatwa na kutuhumiwa kuwa ni mhalifu, ni kweli ni mhalifu.
Hata wengine wanaweza mpaka kutiwa hatiani na mahakama kwa ushahidi wa magumashi lakini kiukweli hawana hatia.

Sasa ukiua watu wa hivyo halafu baadaye ukaja fahamu kuwa walikuwa sio wahalifu, utajiskiaje?
Umemwelewa lakini au ndio watetezi wa Wahalifu na kuwachukia Polisi? Ni wanasiasa TU ndio hua wanaonewa na Polisi lakini sio vibaka. Vibaka na Majambazi wanajulijana ndio maana wakikamatwa na kufungwa mitaa inakua salama.Wakiachiwa Hali ya uhalifu inarudi.

Wewe hujiulizi ni Kwa ni ni kipindi Cha Magufuli uhalifu ulipotea mpaka ule wa kuvamia Mabenki na kuteka mabasi.

Bado nchi hizi maskini Zina watu washenzi wasiotii hata Sheria za asili. Yaani watoto wadogo wanakata watu mapanga na kubaka watu halafu Wapelekwe gerezani kufanya Nini. Watafungwa miaka kumi watatoka wakiwa Bado Vijana halafu watakua katili zaidi.

Dawa yao ni Moja tu kuuawa aukukatwa mikono yote miwili. Watoto Wenzao wakiona wataogopa. Ili Polisi Wabaki kuwasaka wezi wa kujificha na kuiba kistarabu sio kukata watu mapanga.
Mtu achukue Mali ya mtu halafu ampe ulemavu Tena. Hapana jamii iamke Sasa ikatae Wahalifu Kwa nguvu zote. Hata kupata viongozi wezi ni Kwa sababu ya kulea watoto wezi na wanaishi kihalifu matokeo yake jamii inatamani kuishi maisha yasiyoendana na maisha halali.
Tusilinganishe Huko Ulaya na Afrika Waafrika Kwa Sasa ndio kunakucha watu wanaishi Kwa uhalifu inabidi Sheria iwe Kali mana Dunia kila mtu anakimbizana na pesa usipoweka Sheria Kali wanyonge watageuka kuwa mawindo ya wenye nguvu . Na Kwa sababu wameshakupora pesa zako ni rahisi pia kuhonga Polisi au kuweka mawakili na kushinda kesi.
 
Huwezi waamini polisi kiasi hicho.
Sio kila anayekamatwa na kutuhumiwa kuwa ni mhalifu, ni kweli ni mhalifu.
Hata wengine wanaweza mpaka kutiwa hatiani na mahakama kwa ushahidi wa magumashi lakini kiukweli hawana hatia.

Sasa ukiua watu wa hivyo halafu baadaye ukaja fahamu kuwa walikuwa sio wahalifu, utajiskiaje?
huu ujinga wenu ndio unawachelewesha.

huwaamini,na unalalamika hali mbaya mtaani kiusalama,fanya kitu basi jamii ijue upo na umechukua hatua.
 
Unamaanisha nini? Unamaanisha kuwa panya road wanao uwezo wa kuya-access mageti ya jeshi? Basi kama ni hivyo wasogee na huko halafu tusubiri kusikia ni nini kitatokea kwa sababu masikikio tunayo
Soma na comments nyingine sio unakurupuka tu!
 
huu ujinga wenu ndio unawachelewesha.

huwaamini,na unalalamika hali mbaya mtaani kiusalama,fanya kitu basi jamii ijue upo na umechukua hatua.
Sawa mwerevu.
Siku utakapobambikwa kosa na polisi wa bongo, ndio utakumbuka hiki ulichoandika.
 
Back
Top Bottom