Hii Fastjet bora ife tu

Usikute ndege ilishakuwa kwenye runway we unasema dk 1..halafu mara nyingi check in za flight za ndani ni 1 hr..sasa we dhani huko ATCL nako kuna huo ujinga wako
 
Nimechelewa dak 1 tu check in wamenizuia kabisa pamoja na kubembeleza kote kule halafu naenda kusogeza tiketi mbele wanadai 255 Ikabidi nikakate air Tanzania tiketi mpya kwa 230
kumbe ulichelewa?

poa... next time wahi ndugu!
 
hata mabasi ya ubungo ukichelewa asubuhi yanakuacha sembuse ndege!
 
Nimechelewa dak 1 tu check in wamenizuia kabisa pamoja na kubembeleza kote kule halafu naenda kusogeza tiketi mbele wanadai 255 Ikabidi nikakate air Tanzania tiketi mpya kwa 230
Acheni kuharibu biashara za watu, nilishachelewa Muda wa Check in ikawa imebaki dk 15 ndege kuondoka na waliniruhusu, wewe utakuwa umefika muda ushaisha na abiria wameshaingia kwenye ndege na ishajiandaa kuondoka
 
Mm pia nlichelewa miaka 3 ilopita nlikuwa na familia yangu yote just dakika si zaidi ya 10, nikakuta check in ndo inaisha nlivyowambia kusogeza ticket enzi hizo ilikuwa 48000/= nikaambiwa kila ticket niilipie 280000/=na tulikuwa wanne,nikawashit nikachukua precision kwa laki mbili mbili
 
Tena kwa hela ya kukopeshwa, nlichukia balaaaaaa, ila nliendelea kupanda ndege zao sababu ya gharama nafuu, toka air tanzania ianze sina time na fastjet kabisa
 
Wao wanajidai wanajali mda wao wa kuondoka lakini ikitokea wao wamechelewa inabidi uwasubiri ila wewe ukichelewa hawakuelewi
Siku na wao fastjet wakichelewa kuondoka wazuie wasiondoke. Ila nawapongeza kwa kujali muda maana nilisikia abiria wa ATCL wakilalamika siku moja kuchelewa kuondoka kisa kumsubiri Mh.
 
Duh!

Nimetoka kununua tiketi ya Fastjet muda mfupi tu ulopita...nafungua JF nakutana na huu uzi!

Alhamdulillah uzi hauhusu huduma yao [FastJet] bali uzembe wa mwanzisha mada.

La sivyo ningeanzisha zogo
Mzee Mwenzangu, mashirika yote ya ndege ni ovyo tuuu, na hata msimamizi sijui P nini nini hukooo, kwanza wako wawili tuu halafu wanafunzi. Mm nishapata raha na karaha kwa mashirika yote ya hapa nchini, ni kuomba lisikukute na kupunguza uzembe.
 
Mwenye hii ID ni yule kaka angu ninaemjua au mtu tu anatumia jina lake?
Pole mwayaaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom