Hii dharau sijapata kuiona!!

Hii dharau sijapata kuiona!!

Ng'wanapagi

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2013
Posts
9,116
Reaction score
8,662
Ndugu zangu nimeonelea siku hii ya kumalizia Xmass nikachomeshe kitimoto kwenye bar flani huku mtaani kwetu. Wakati nikiwa nasubiri ili kuepuka usumbufu wa kuulizwa mara kwa mara kaka tukusaidie nini nimeamua kuagiza soda. Niliofika nao pamoja wameagiza bia (pombe) na kuhudumiwa faster kwa kupewa meza na viti huku mimi nikiambiwa viti vimeisha!! Nimesimama hadi miguu ikaniuma nikaamua kusogea kaunta ili niegemee kaunta ninywe hiyo soda ya kusubiria kiti moto,wakati nikiwa hapo kaunta nimeona viti vitatu vikiwa tupu bila watu (vimewekwa akiba). Sijui niwape faka au nisubiri tu pork yangu nisepe:what:
 

Attachments

  • 1451153740998.jpg
    1451153740998.jpg
    44.8 KB · Views: 2,152
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Vumilia tu best yangu,subiria mdudu wako (shwain wewe,kumbe unatumia hii kitu?)

Kwi kwi kwi kwi kwi kwi!! Ningejua hujalala.................kimya😀😀😀:sly: Nitaiacha kuanzia tarehe 1/1/2016
 
Ndo customer Care za kibongo, Tanzania kwa swala la huduma kwa wateja bado sana, yaani bado mno,
 
nani anataka kung'atwa na nyuki usiku huu... hata hapo counter wasingekuruhusu tu
 
Haaaa, mkuu ungeagiza maji makubwa Kilimanjaro ndo wangekupa kiti, soda hawatoi kiti huu ni msimu wa sikukuu.
 
Wanasubiria wateja wamaowapa tipu ya pesa nyingi.
 
Kwa kweli wahudumu wa Bar wanadharau sana wanywa soda na maji.
 
Mhhhh aisee afadhali yangu mimi nakunywaga Bavaria, au nayo inaleta nzi jamani?
Nilikuwa sijui hili!
[emoji85] [emoji85] [emoji85]

Angalau bavari kidogo. Ila em jaribu siku kunywa ile 8.6 bavaria sio 0.0 jirani
 
Napendaga kweli dharau za namna hii.....

Ningelianzisha timbwili la haja....... wangemleta mmiliki kuja kupozaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom