Hii course vipi jamani?

Adm

Senior Member
Sep 19, 2010
149
45
Mi mdogo wenu ndo nimehitimu kidato cha sita na matokeo yangu ni Physics-E,Chem-E,Biology-D,BAM-S and GS-S. Tangu mwanzo nimekuwa nikipendelea kusoma INFORMATION TECHNOLOGY. Swali langu wana jf ni kwamba,kwa matokeo hayo naweza kusoma hiyo kozi(degree level) na bodi inatoa mkopo kwa watu wanaosoma kozi hiyo?
 
kwanza pole kwa matokeo hayo kwani naamini hukutaraji yawe hivyo...ila hapo sio mwisho kwani bado waweza soma chuo.
serikali inatoa mikopo kwa watu waliopata div 3 wanaosoma masomo ya science na ualimu pekee.
kila la kheri kwenye mchakato wako wa shule.
 
asante kwa ushauri wako,serikali inatoa mkopo kwa degree za sayansi na ualimu. Je Bsc in IT nitapata mkopo?
 
asante kwa ushauri wako,serikali inatoa mkopo kwa degree za sayansi na ualimu. Je Bsc in IT nitapata mkopo?

Kwa kiwango hicho cha kufaulu, sidhani kama kuna "creadible University" ambayo watakupa "Admission" ya BSc. (in any field, leave alone IT) ... Unaweza ku-re-seat au tumia njia ya cheti-diploma-degree..
 
jaribu IFM kuna uwezekano mkubwa wa kupata jamaa yangu pale anasomea hiyo na pia bodi wanatoa mkopo kwa IT-degree hiyo div yako sio mbaya mdogo wangu. umesema ni DIV III-14 ?
 
omba ifm kuna jammi zangu pale walipata div-3 pts 17 wakapata hyo BSC-IT na bodi inawapa mkopo 100%....uckate tamaaa mkuuu.....ndo form ilivyo.
 
dogo hapo chuo mbona unapata kabisa kwa IT, jaribu mzumbe,sua,udom,ruico etc kuna jamaa zangu wamepata chance tena kwa points pungufu ya hapo na mkopo walipata. lakini kuwa mwangalifu kuna IT/information systems/IT management ni vitu vyenye tofauti kubwa sana na vyuo vingi vya tz wanatoa IT management ambayo utakuwa mbovu kupindukia ktk maswala ya IT maana hapa utakuwa unatafuta kazi ya umanager
 
Back
Top Bottom