HESLB yatangaza kupokea maombi 2016/2017

Hili swara linaniumiza kichwa sana ..kuendelea kulipa mamilion ya shilng na hali ya wazaz wetu ilivyo..mbona kama n unyanyasaji..sada hapo ndo ukute nyumban mnasoma watoto 4..ndo utaisoma namba
 
kwan mwaka jana si waliandka hvyo hvyo
hakuna kilichobadlika lakin mbona walipata
achen kupanikisha watu
Una uhakika na unayosema Mkuu soma vizuri guidelines za mwaka jana na za mwaka huu sasa watu walizoea kufanya kazi kwa mazoea subiri mwaka huu hawakutishi ila Ndalichako anasema sheria lazima zifuatwe kama inavyoainishwa
 
Kwa sisi tuliosoma kozi za elimu( education) umuhimu wa elimu unategemea sana hitaji la jamii( social need) kwa muda huo. Kwahyo sasa hivi hitaji la jamii ni wataalamu wa nyanja za sayansi. Kuliko kusomesha watu ambao hauna mahitaji nao na hata wao wenyewe hizo kozi sio rahisi kuwasaidia maana watamaliza chuo na kuanza kutafuta ajira ambazo ni adimu sana, ni bora hizo fedha zipelekwe kwenye mambo ya msingi zaidi kwenye jamii kama kutengeneza barabara na kuboresha huduma za afya na elimu msingi.

Wewe mhitimu wa masomo ya sanaa kama familia yako haina uwezo wa kukusomesha ni bora kujiajiri mapema kwenye kilimo na ufugaji kwani tayar hiyo elimu ya kidato cha sita imeshakukomboa kifikra. Usijisumbue kwenda chuo kikuu maana ndo utajiharibu kabisa kimtazamo wa maisha kwa sababu utapenda kuishi maisha standard zaidi wakati uwezo hautakuwa nao, na utaona aibu kurudi kijijini kuendelea na kilimo na kujikuta unaishi mjini kwa ndugu na jamaa huku ukiwa na stress za maisha kibao.

Naomba msinielewe vibaya au kuniona nawaonea wivu, ninaongea kutokana na uzoefu.Karibu chato tulime pamba na mpunga.
Kama masomo hayana umuhimu bas yafutwe kwenye mitaala ya utoaji elimu Tanzania
 
Bodi ya mikopo Tanzania (HESLB) imetangaza kuanza kupokea maombi rasmi ya mikopo kwa kutoa Guidelines kwa mwaka 2016/2017 hivyo wananchi wote mnaombwa kusoma kwa makini masharti kabla ya kufanya application mwisho wa ku apply ni 31st July tembelea www.heslb.go.tz for more information
Means Test Scores ni nini Harnandez. Tafadhali
 
Habari zenu wadau,

Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu, HESLB imewatia vitanzi wahitimu waliomaliza nyuma ya mwaka 2014. Soma guideline uone ukatili huo kwa ambao hawakuweza kupata mikopo kwa njia moja au nyingine.

Kwa mtazamo wangu inakatisha tamaa!
 
Bodi ya mikopo wametaja engineering programs zoooote lkn wameshindwa kuweka aircraft maintenance engineering inayotolewa pale NIT mwenye uelewa na hili anisaidie je mtu atakayekuja kuomba hii course watamuweka ktk category ipi?
 
Back
Top Bottom