HESLB wanatoa wapi pesa za kudhamini vipindi vya redio?

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
3,062
2,000
HESLB ni wadhamini wa kipindi cha Powerbreakfast cha Clouds FM, swali ninalojiuliza hapa ni kwamba inakuwaje taasisi ya serikali ambayo ni non-profit institution inajigeuza kuwa profit-based institution?

Sielewi lengo lao la kujitangaza ni nini. Hawana ushindani wowote, hawana mtu wanayeshindana naye, sheria iliyounda taasisi haisemi taasisi itajihusisha na uwekezaji bali kuwakopesha wanafunzi wasio na uwezo wa kulipia gharama za masomo ya elimu ya juu.

Sasa HESLB tuambiane pesa za kudhamini vipindi vya redio mnazitoa wapi, au ndo ile 6% mnayotukata kila mwezi?

HESLB haipaswi kujitangaza la sivyo mruhusu kuwe na taasisi shindani zinazotoa mikopo ya elimu kwa wanafunzi wa elimu ya juu pia.
 
Mkumbwa Jr

JF-Expert Member
Mar 23, 2016
1,465
2,000
Yaani kila nikiona huo msamiati HESLB naiona dhuluma, unyang'anyi, ubabe na uswahili mwingi

Hawasaidii maskini wanajisaidia wao,familia zao na jamaa zao.

Kama kweli wamefikia hatua ya kudhamini vipindi hiyo ni balaa

Kuna Uzi nilishaandika na kumshauri Mh. Rais afumue menejimenti yote.

Ikiwezekana aondoe hadi walinzi pale maana rushwa ni nje nje
 
Mkumbwa Jr

JF-Expert Member
Mar 23, 2016
1,465
2,000
Yaani Mh.Rais asipoondoa hii menejimenti bado ataacha kundi kubwa la maskini linyanyasike na watumishi kudhulumiwa.
 
Mkumbwa Jr

JF-Expert Member
Mar 23, 2016
1,465
2,000
Pale walinzi, wafagiaji ndio wanapewa rushwa na wenye hela zao wawapelekee watumishi wa bodi ili wapewe Mikopo.

Maskini, yatima hawapewi na watumishi tunakatwa makato makubwa.

Yaani HESLB rushwa nisehem ya utumishi wao. Tunawajua kwa majina
 
Sage_

Member
May 20, 2019
51
125
Acha wajitangaze, wanatangaza na kutoa elimu kwa wateja wao (Wakopaji). Mbona mashirika mengi ya serikali yasiyokuwa na washindani wanajitangaza kama TANESCO, Mamlaka za maji nk.

Mikopo ndo biashara yao maana mwisho wa siku kuna riba.
 
Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
3,062
2,000
Acha wajitangaze, wanatangaza na kutoa elimu kwa wateja wao (Wakopaji). Mbona mashirika mengi ya serikali yasiyokuwa na washindani wanajitangaza kama TANESCO, Mamlaka za maji nk.
Mikopo ndo biashara yao maana mwisho wa siku kuna riba.
Acha ujinga mkuu, ile ni nonprofit government institution, imeundwa kwa sheria ambayo inazuia taasisi kujigeuza kuwa ya kibiashara, ipo pale kuwezesha watanzania wasio na uwezo wa kujilipia gharama za masomo ya elimu ya juu.

Wanapokengeuka na kuanza kufanya hiyo huduma kama biashara basi waruhusu kuwe na soko huria la kutoa mikopo ya elimu ya juu, waruhusu watu au makampuni mengine nayo yajiingize kwenye hiyo biashara.
 
Sage_

Member
May 20, 2019
51
125
Acha ujinga mkuu, ile ni nonprofit government institution, imeundwa kwa sheria ambayo inazuia taasisi kujigeuza kuwa ya kibiashara, ipo pale kuwezesha watanzania wasio na uwezo wa kujilipia gharama za masomo ya elimu ya juu...
Ukiniita mjinga wewe ndo utakuwa mjinga zaidi, theoretically ni sawa non profit lakini practically ni financial instution inayokopesha wanafuzi. Ndo maana wameweka na riba, vinginevyo wakiondoa riba ndo itakuwa sawa na malengo ya uundwaji wake na ndipo utaiita nonprofit.
 
Makanyaga

JF-Expert Member
Sep 28, 2007
6,374
2,000
HESLB ni wadhamini wa kipindi cha Powerbreakfast cha Clouds FM, swali ninalojiuliza hapa ni kwamba inakuwaje taasisi ya serikali ambayo ni non-profit institution inajigeuza kuwa profit-based institution?

Sielewi lengo lao la kujitangaza ni nini. Hawana ushindani wowote, hawana mtu wanayeshindana naye, sheria iliyounda taasisi haisemi taasisi itajihusisha na uwekezaji bali kuwakopesha wanafunzi wasio na uwezo wa kulipia gharama za masomo ya elimu ya juu.

Sasa HESLB tuambiane pesa za kudhamini vipindi vya redio mnazitoa wapi, au ndo ile 6% mnayotukata kila mwezi?

HESLB haipaswi kujitangaza la sivyo mruhusu kuwe na taasisi shindani zinazotoa mikopo ya elimu kwa wanafunzi wa elimu ya juu pia.
Inawezekana labda kuna kitu faida wanayopata kutoka kwenye tangazo hilo.
 
Darmian

JF-Expert Member
Oct 1, 2017
11,596
2,000
Wanatangaza namna watu wanavyopaswa kurejesha mkopo(kwa njia ya mtandao) baada ya kupata kazi ili fedha zipatikane za kuweza kukopesha vijana wengine wengi na kupunguza mzigo wa serikali kuwatengea fungu kubwa..hii sio faida?

Hawajitangazi kwa ile ya kusema " Heslb ni babalao,hatuna mpinzani Tanzania,mikopo yetu ni chapuchapu".

Think critically.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom