mamabaraka
Member
- Oct 18, 2011
- 92
- 14
jaman viongozi mtaendekeza huo uozo hadi lini? Jaribuni kujisafisha japo kwa hili la ajira kwa wahitimu vyuoni, unajua sioni mantiki mwalimu na dactari anaajiliwa bila interview wengne interview mbili kuendelea ina maana matutors wa coz nyingine hawafundishi au wanafunzi hawaelewi hadi wajisomee after kumaliza chuo? Tumechoka tunataka haki. Juzi nilitafakari maisha wazazi wangu walivyokuwa wakinisihi nisome sana niwe na maisha mazuri, na jinsi walivyokuwa wanalala njaa wapate ada yangu wakiamini baadae ningewasaidia, leo hii nimeitimu chuo miaka inapita sina kazi naambuliwa kuwaomba wajinyime tena wanipe mtaji au hela yamatumizi. Inauma sana umemaliza chuo huna tofauti na aliyeishia la saba kimaisha. Siku moja nikiwa kwenye daladala alipita dada mmoja mwanasheria, teja akiwa ndani ya daladala akaanza kusema mnamcheck yule ana degree lakin ana miaka mitatu mtaani kazi hakuna kachoka hata si tunamzidi,. iliniuma hadi nikatoa machozi. Mungu atusaidie