HESLB na uzembe wa kujibu mail na kupokea simu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

HESLB na uzembe wa kujibu mail na kupokea simu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Things Fall Apart, Aug 29, 2017.

 1. Things Fall Apart

  Things Fall Apart Senior Member

  #1
  Aug 29, 2017
  Joined: Jun 26, 2012
  Messages: 177
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Habari wanajamvi,
  Leo ninaleta kero hii kuhusu hiki kitu kinachoitwa HESLB, naam namaanisha Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini Tanzania.

  Ni majuzi tu mheshimiwa Rais JPM alitengua uteuzi wa bwana mmoja aliyekuwa mkurugenzi mtendaji kwa muda mrefu sana ndugu George Nyatega ili kuhuisha utendaji wa taasisi hii nyeti kwa mustakabali wa elimu hapa nchini. Baada ya hapo tukaletewa ndugu Abdul Razaq Badru kurithi mikoba ya bwana Nyatega.

  Mara baada ya kuchukua kiti, bwana Badru alionesha makeke na kuapa kuwasaka wale wote walionufaika na mikopo lakini hawajarejesha mikopo yao. Bwana Badru alienda mbali zaidi na kusema atawafuata wadaiwa sugu hadi siku wanapofunga ndoa kuwadai fedha walizokopa walipokuwa wakisoma. Hii ilikuwa sawa kabisa kwa bwana Badru ukizingatia tupo serikali ya awamu ya tano "Hapa Kazi Tu".

  Cha kushangaza ni kwamba baada ya hapo mambo ya Bodi ya Mikopo (HESLB) hayaendi kama bwana Badru alivyotuaminisha kwenye media. Kwa nini nasema hivi?: Mimi ni mnufaika wa mkopo wa elimu ya juu alimaarufu kama "BOOM". Nimepiga hela zao, nimemaliza na sasa ni muajiriwa kwa miaka kadhaa na salary napiga kama kawaida ila nipo private firm. Sasa baada ya bwana Badru kutangaza mikakati yake na namna atakavyotusaka, nikaingiwa na kahofu nikasema wacha nijitokeze ili nijulikane na nipewe statement yangu nianze kukatwa 15% mara moja nisijeaibishwa bure siku nachukua "jiko". Sasa picha ndio linaanzia hapa. Niliandika email miezi zaidi ya sita iliyopita kwenda bodi kwenye email yao kama iliyvo katika website ya HESLB
  info@heslb.go.tz lakini hadi naenda mitamboni leo hii karibia tumalize mwaka hakuna majibu. Nimejaribu kupiga namba zao walizoweka kwenye website yao kwa muda mrefu +255-22-2772432/3 lakini simu inaita tuu haipokelewi au ipo bize.

  Sasa ninachojiuliza ni hiki; ikiwa mimi ni mnufaika niliyejitokeza kwa hiari yangu mwenye nia ya kulipa siwezi kupata statement ya deni langu ili nianze kulipa, je itakuwaje kwa mnufaika ambaye amejificha na hataki kujitokeza? Je, Bodi itaweza kumfikia? Sanasana itaishia kwa watumishi wa uma kama waalimu na wenzao wenye cheki namba japo kimshahara chao kiduchu masikini ndio wanafyekwa bila huruma hilo li 15%. Kwa sisi tuliopo private itawachukua muda sana tena sana.

  My take: Bwana Abdul Razaq Badru jitahidi kufanyia kazi kile unachohubiri. Haina maana kutangaza msako wa wadaiwa sugu kwenye media ilihali kuna wadaiwa waliokwisha kujitokeza wanaulizia statement ili waanze kulipa hawapatiwi huduma. Kama hizo e-mail hakuna mtu wa kuzisoma na ku-respond ziondoeni kwenye website yenu maana hazina maana. Hizo namba za simu mnaweka hapo simu inaita tu haipokelewi maana yake nini? nazo mzifute. Na kwa staili hii sahauni kuwapata wadaiwa sugu. Naamini meseji hii pia itasomwa na wale vijana wa suti nyeusi pale MAGOGONI naam zifikisheni kwa mukulu.

  Naomba kuwasilisha.
  Things Fall Apart
   
 2. B

  Babati JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2017
  Joined: Aug 7, 2014
  Messages: 29,303
  Likes Received: 22,413
  Trophy Points: 280
  TCU, NACTE na HESLB
   
 3. K

  Kanyinya JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2017
  Joined: Jul 31, 2017
  Messages: 293
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 80
  Hao ni wahuni hawapokeagi Simu
   
 4. t

  time2ball Senior Member

  #4
  Aug 29, 2017
  Joined: Feb 4, 2014
  Messages: 128
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  Poor Communication or poor correspondence ni jambo la kawaida kwa institutions za serikali. Sasa unajiuliza hizo websites zao huwa hazina web managers au ni nini? Mimi nna experience ya brela nimeingia kwa web yao nimekwama kitu kuna sehemu ya help ni ka click na kutuma msg ya kuomba msaada 3 weeks now no response. Wameweka namba ya simu lakini haipatikani it is a shame. Kuna wakati nilikuwa naistall FIFA game kwenye laptop nikapata shida nilivyoenda kwa website ya watengenezaji wa game nilipata mtu akanielekeza step by step in real time through chatting! That's how serious wenzetu walivyo! Sisi tuna Mark time tu hapa!
   
 5. j

  joseph1989 JF-Expert Member

  #5
  Aug 29, 2017
  Joined: May 4, 2014
  Messages: 896
  Likes Received: 1,900
  Trophy Points: 180
  We acha tu mm tokea jtano wiki iliyopita, nahangaika nayo, namsaidia dogo kujaza wapi, kwanza nikijaza index no IV, naenda ktk link ili nipate control namba, link hairespond, nimekaa baada ya siku moja ikakubali, nikasubiri control no baada ya siku mbili, nikalipa tigo pesa, ni kajaribu kuendeleza ku load wapi, jioni yake nikarudushiwa muamala wangu, jana usiku nikajaribu tena kulipia majibu nimeyapata leo asubuhi hii, ndio naenda kujaza tena,sasa sijui na leo watasemaje manake nimechoka.Jana nimepiga simu mpaka nimechoka, hawajibu alafu cha ajabu, sijui ujinga au dharau au upumbavu, namba ya simu wameiweka moja tu, hawajamaa wa HELSB hawapo serious.
   
 6. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #6
  Aug 29, 2017
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,511
  Likes Received: 3,539
  Trophy Points: 280
  Basi experience ni tofauti. Mimi ni mnufaika wa mkopo/boom. Niliwatumia email kuomba statement yangu ya deni. Nilijibiwa within three days. Nikawalipa deni lao kwa awamu mbili. Mpaka sasa nimeshamalizana nao. Sidaiwi.
  Possibly jaribu kufuatilia physically. Panapowezekana epukana na madeni. Na kwa deni kama hili ambalo limekuwezesha "kutusua" kwa kupata kazi, sidhani kama ni sahihi kusubiri utafutwe. Just pay them and move on.
   
 7. Things Fall Apart

  Things Fall Apart Senior Member

  #7
  Aug 29, 2017
  Joined: Jun 26, 2012
  Messages: 177
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hongera sana mkuu kwa kubahatika kuhudumiwa mapema na bwana Badru. Kufika physically ni mojawapo ya wazo nililo nalo. Tatizo ni kwamba nipo mbali (Mkoa). Kwa hiyo unaweza ona ni jinsi gani ilivyo rahisi kwa bodi kunitumia mail ya statement kuliko mimi ("mdaiwa sugu" japo mkataba niliyosaini unanipa repayment time ni hadi 2020), kukata ticketi ya mkoa ili kusafiri hadi pale opposite na Mlimani City ili kumtafuta anayenidai o_OIt's a bit crazy! :D. Wacha niendelee kutusua hadi siku watakapoamka usingizini na kunitumia hiyo statement.

  'Acha kila mtu apambane na hali yake'
   
Loading...