Things Fall Apart
Senior Member
- Jun 26, 2012
- 178
- 146
Habari wanajamvi,
Leo ninaleta kero hii kuhusu hiki kitu kinachoitwa HESLB, naam namaanisha Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini Tanzania.
Ni majuzi tu mheshimiwa Rais JPM alitengua uteuzi wa bwana mmoja aliyekuwa mkurugenzi mtendaji kwa muda mrefu sana ndugu George Nyatega ili kuhuisha utendaji wa taasisi hii nyeti kwa mustakabali wa elimu hapa nchini. Baada ya hapo tukaletewa ndugu Abdul Razaq Badru kurithi mikoba ya bwana Nyatega.
Mara baada ya kuchukua kiti, bwana Badru alionesha makeke na kuapa kuwasaka wale wote walionufaika na mikopo lakini hawajarejesha mikopo yao. Bwana Badru alienda mbali zaidi na kusema atawafuata wadaiwa sugu hadi siku wanapofunga ndoa kuwadai fedha walizokopa walipokuwa wakisoma. Hii ilikuwa sawa kabisa kwa bwana Badru ukizingatia tupo serikali ya awamu ya tano "Hapa Kazi Tu".
Cha kushangaza ni kwamba baada ya hapo mambo ya Bodi ya Mikopo (HESLB) hayaendi kama bwana Badru alivyotuaminisha kwenye media. Kwa nini nasema hivi?: Mimi ni mnufaika wa mkopo wa elimu ya juu alimaarufu kama "BOOM". Nimepiga hela zao, nimemaliza na sasa ni muajiriwa kwa miaka kadhaa na salary napiga kama kawaida ila nipo private firm. Sasa baada ya bwana Badru kutangaza mikakati yake na namna atakavyotusaka, nikaingiwa na kahofu nikasema wacha nijitokeze ili nijulikane na nipewe statement yangu nianze kukatwa 15% mara moja nisijeaibishwa bure siku nachukua "jiko". Sasa picha ndio linaanzia hapa. Niliandika email miezi zaidi ya sita iliyopita kwenda bodi kwenye email yao kama iliyvo katika website ya HESLB
info@heslb.go.tz lakini hadi naenda mitamboni leo hii karibia tumalize mwaka hakuna majibu. Nimejaribu kupiga namba zao walizoweka kwenye website yao kwa muda mrefu +255-22-2772432/3 lakini simu inaita tuu haipokelewi au ipo bize.
Sasa ninachojiuliza ni hiki; ikiwa mimi ni mnufaika niliyejitokeza kwa hiari yangu mwenye nia ya kulipa siwezi kupata statement ya deni langu ili nianze kulipa, je itakuwaje kwa mnufaika ambaye amejificha na hataki kujitokeza? Je, Bodi itaweza kumfikia? Sanasana itaishia kwa watumishi wa uma kama waalimu na wenzao wenye cheki namba japo kimshahara chao kiduchu masikini ndio wanafyekwa bila huruma hilo li 15%. Kwa sisi tuliopo private itawachukua muda sana tena sana.
My take: Bwana Abdul Razaq Badru jitahidi kufanyia kazi kile unachohubiri. Haina maana kutangaza msako wa wadaiwa sugu kwenye media ilihali kuna wadaiwa waliokwisha kujitokeza wanaulizia statement ili waanze kulipa hawapatiwi huduma. Kama hizo e-mail hakuna mtu wa kuzisoma na ku-respond ziondoeni kwenye website yenu maana hazina maana. Hizo namba za simu mnaweka hapo simu inaita tu haipokelewi maana yake nini? nazo mzifute. Na kwa staili hii sahauni kuwapata wadaiwa sugu. Naamini meseji hii pia itasomwa na wale vijana wa suti nyeusi pale MAGOGONI naam zifikisheni kwa mukulu.
Naomba kuwasilisha.