HESLB bado hawajatoa VRF kwenye salary slip

baiser

JF-Expert Member
Dec 29, 2014
1,267
2,000
Mimi nashangaa sanaaa haya mambo ya kimfumo tu kinachofanyika ni kupunguza deni automatic kama walivyoliweka .masuala ya kwansa sijui kwa mwajiri n.k ni kupoteza mda ...inabd njia waliotumia kuingiza deni kwenye s.slip ni ile ile itumike kuliondoa au kulipunguza
 
Culminate

Member
Jul 24, 2019
69
125
Huo utofauti ukoje?unajua Sisi wengine tupo mikoani kufika makao makuu ni mbali kidogo

Kumbuka sasa hivi VRF na penalty zimefutwa.

Hivyo, automatically kiwango cha pesa unachodaiwa kitabadilika. Hapo ndio inconsistency inapotokea. Kuna watu madeni yao ni makubwa lakini si kwa sababu ya riba au penalty bali uingizaji mbaya wa taarifa za madeni.

Verified loan statement inaonesha mchanganuo uliokamilika kama ifuatavyo

i) Ulikopeshwa shilingi ngapi.

Hapa utapewa taarifa kwa mchanganuo. Kwa mfano kiasi cha tuition fee, meals and accommodation, research fund, practical training n.k ulichokopeshwa.

ii) Umerejesha kiasi gani hadi sasa.

Hapa utaoneshwa marejesho yako ya kila mwezi. Kuna watu wanadaiwa pesa nyingi kumbe kosa ni la muajiri kuna miezi hakuwa anapeleka pesa.

Na hii inatokea hata kwa waajiriwa wa serikali pia. Kwa hiyo usijipe moyo wewe ni mwajiriwa wa serikali.

Wewe nenda tu kapate statement yako ujue hali ya mkopo wako.
 
goodlif1600

JF-Expert Member
Jun 1, 2016
441
500
Sio kazi kubwa ni mifumo tu ya kitehama inaweza kumaliza hiyo kazi. Au watoe utaratibu kila wadaiwa ktk halmashaur fulani waende kwa ofisi za utumishi kubadilishiwa au ku uodate taarifa zao. Mbona kwenye kuingiza makato mapya haikuwa kazi ngumu? Ila kwenye ku update taarifa inakuwaje kazi ngumu
Umemjibu vyema uyu jamaa atakua bodi ndo maana anatetea uzembe wanaoufanya
 
Culminate

Member
Jul 24, 2019
69
125
Sasa hili ni kosa la nani? Mtumishi au loan board?

Mkuu kwani wewe unahitaji kumjua mwenye kosa ni nani au unataka deni lako liishe?

Collective justice ni ngumu sana, hasa kwenye kesi kama hizi. Wewe nenda bodi kaweke mambo sawa, otherwise watakukata deni litaisha na wataendelea tu kukukata.

Kitakachofata ni wewe kuanza kudai pesa waliyozidisha kukukata kimakosa.

Hapo sasa ndio utajua kuwa viatu huwa kweli vinaisha ukivitembelea sana.

Ila ni kama alivyosema mkuu hapo juu. Kupanga ni Kuchagua. The ball is in your court.
 
Mpelu

Senior Member
Jul 10, 2021
128
225
Kumbuka sasa hivi VRF na penalty zimefutwa.

Hivyo, automatically kiwango cha pesa unachodaiwa kitabadilika. Hapo ndio inconsistency inapotokea. Kuna watu madeni yao ni makubwa lakini si kwa sababu ya riba au penalty bali uingizaji mbaya wa taarifa za madeni.

Verified loan statement inaonesha mchanganuo uliokamilika kama ifuatavyo

i) Ulikopeshwa shilingi ngapi.

Hapa utapewa taarifa kwa mchanganuo. Kwa mfano kiasi cha tuition fee, meals and accommodation, research fund, practical training n.k ulichokopeshwa.

ii) Umerejesha kiasi gani hadi sasa.

Hapa utaoneshwa marejesho yako ya kila mwezi. Kuna watu wanadaiwa pesa nyingi kumbe kosa ni la muajiri kuna miezi hakuwa anapeleka pesa.

Na hii inatokea hata kwa waajiriwa wa serikali pia. Kwa hiyo usijipe moyo wewe ni mwajiriwa wa serikali.

Wewe nenda tu kapate statement yako ujue hali ya mkopo wako.

Na nilisikia kwamba kuna value retention fee before 1 May 2021 kwamba nayo imeesabiwa je hili ni kweli?
 
Omusolopogasi

JF-Expert Member
Aug 31, 2017
5,515
2,000
Swali linajibiwaje na swali, ndugu? Katika wote waliochangia hapa, yaani umeona mimi ndio naweza kuwa na taarifa hiyo! Uliona na mimi niliuliza swali - maanake sina taarifa.
Je vrf wameifuta yote au wamebakiza kiasi?
 
Kimbori

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
4,494
2,000
Hii bodi ina mauzauza sana. Kuna cases zinatafarisha kwelikweli!
1. Mdau 1 alikuwa na deni la 5m (alikopeshwa 11m, na kuanza kulipa 2016), ghafla kwenye system inasoma laki 6. Sijui kama kuna formula yenye kuweza kufafanua hilo.
2. Mdau 2 alikopeshwa 8 m, akaanza kulipa 2014, mpaka sasa bodi inatambua kuwa HAJAWAHI KULIPA HATA SENTI, slip inasomeka 1.5m Kama deni.
NB. Niishie hapo kwa sasa
 
MZEE RAZA

JF-Expert Member
Feb 19, 2015
2,734
2,000
Mnajichanganya ninyi tu bodi wapo vema na hawana shida. Saizi unajisajili kwenye web yao na unaona deni lako halisi. Hawawezi kwenda kwa waajiri wote kufanya update ya makato kwenye salary slip ni kazi kubwa sana. Wewe chukua statement yako online jua deni lako, au fika bodi jua deni halisi baada ya msamaha.

Kwa mfano mimi kwenye statement ya bodi nadaiwa laki 8 tu. Lakini salary slip inaonesha nadaiwa mil 2.5

Kuna jamaa yangu salary slip inasoma mil 1.8 lakini statement ya bodi ilimwambia kamaliza deni. Alipowasiliana nao wakamwambia akachukue clearance certificate. Unapeleka utumishi wanaondoa Deni.

Wanaoshughulika na salary slip na kuingiza na kutoa makato ni utumishi/mwajiri. Ndio maana hata bank wakikulipia deni haliondoki automatically ila wanapeleka uthibitisho utumishi au kwa mwajiri kuwa ume clear wanaliondoa kwenye makato ya mshahara, maana ni hao hao utumishi waliweka hayo makato walipoletewa orodha na bodi.

Bodi kupata waajiriwa ilikuwa inawatafuta kupitia waajiri sio system za serikali kukunasa juu kwa juu. Hii ina maana mwajiri ndiye anaweza kutoa au kupunguza makato pale anapoambiwa na bodi. Sasa bodi haiwezi fanya hii kazi kubwa hivi, wewe unaedaiwa nenda ujue deni lako. Kwanza saizi wamerahisisha ni kuingia kwa web yao unajisajili unaona kila kitu, wanakupa na control number hapo hapo ya kulipia. Wanakupa option yakulipia mpk tigopesa. Mnalalamika hata bila kuwa well informed.

Wapo ambao wameajiriwa baada ya makato kupanda kuwa 15% hao deni lao halipo mbali na ukweli uliopo kwenye salary slip kwa uzoefu wangu na pengine yanalingana kabisa.
Umefanya udadavuzi mzuri mno na ndivyo ilivyo!
 
babaellen

Member
Aug 24, 2015
8
45

body wanatakiwa wataarifu utumishi warekebishe madeni kwenye salary slip sababu hizi slip tunazitumia bank na maeneo mengine kama kupata mikopo ya maendeleo nk., pia unaweza wauzia bank huo mkopo mf mimi slip inaonyesha nadaiwa 16.7m , board statement baada ya kuondoa tozo zao nadaiwa 8.5m, hii 8.5m ikitokea kwenye salary slip ni ahueni kubwa kwan itarahisisha kukopa zaid ie pesa kubwa zaid kwa ajir ya maendeleo na bank kuchukua huo mkopo wa heslb
 
Leverage

JF-Expert Member
Jan 25, 2021
1,356
2,000
Mkuu benki huwa hawanunui madeni ya bodi kwa kuangalia salary slip. Ni lazima upate verified loan statement. Hiyo ndio huwa na control number ambayo wao wanaitumia kulipa.

Kwa hiyo bado kwenda bodi ni swala la msingi tu kama unaitaka haki yako kwa haraka.
Hivi mtu ukishindwa kuafikiana na bodi kuna chombo cha juu unaweza kwenda au ndio mahakamani tu?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom