Heshimuni Haki ya kusikilizwa kabla ya kuadhibu Art. 13(6)(a) Katiba

Heshimuni Haki ya kusikilizwa kabla ya kuadhibu Art. 13(6)(a) Katiba

Kitchener

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
13,823
Reaction score
27,694
Kuna matukio mengi tangu mwaka 2015 through 2020 hadi sasa ya wateuliwa wa serikali wanaolipwa mishahara ya kodi zetu, wanapotoa maamuzi yanayoathiri hatima ya mtu au kikundi, wanasahau kuwa lazima wazingatie haki ya kusikilizwa ambayo ipo kwenye Ibara ya 13(6)(a) ya Katiba ya nchi yetu. Ibara inasema

13(6)(a) wakati haki na wajibu kwa mtu yeyote
inapohitajika kufanyiwa maamuzi na
mahakama au chombo kingine chochote
kinachohusika, basi mtu huyo atakuwa
na haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa
kwa ukamilifu
, na pia haki ya kukata rufani
au kupata nafuu nyingine ya kisheria
kutokana na maamuzi ya mahakama au
chombo hicho kinginecho kinachohusika;

Wasichojua ni kwamba:

1. Wameteuliwa kwa Mujibu wa sheria iliyotungwa subject to Katiba, hivyo Katiba inawalazimisha kuzingatia ibara hiyo.

2. Kama wakivunja haki hiyo, wanavunja kibinafsi, sio kiofisi, na kama kushtakiwa watashtakiwa kibinafsi sio kiofisi. Why? kwa sababu mteule aliyewateua aliwateua kisheria, sheria inayowataka wazingatie katiba, wasivunje katiba, hivyo wakivunja wanavunja kibinafsi sio kiofisi na kushtakiwa watashtakiwa kibinafsi, haitashtakiwa serikali/ofisi.

3. Hajatokea tu mtu mwelewa, nchi zingine ukivunja haki za watu, watakupeleka mahakamani na utalipa fidia ya kutosha pengine ufilisike kabisa. hayo pia kuna siku yatatokea hapa nchini.

4. Hakuna aliye salama katika hili, kama leo wamevunja haki ya A, jua kesho watavunja ya B na keshokutwa watavunja yako. Ili kujenga jamii inayoheshimu utawala wa sheria, lazima tuungane kukemea vitendo hivyo kwa nguvu zote.

5. Sheria imekupatia mamlaka kufanya maamuzi yanayoathiri hatima ya watu, cha kwanza watamkie tuhuma yako wajue wanatuhumiwa kwa kosa fulani, halafu wapatie nafasi wajieleze kwa nini wasiadhibiwe. Hautakiwi kuamka asubuhi, unafika Ofisini, unaamua tu leo naadhibu fulani, and you proceed to do it, huo utakua sio utawala wa sheria, ni utawala wa wanyama wa porini. why? simba huwa anaamua tu leo mnyama yeyote atakayetokea hapa kama analika, nakamata na kuua, sihitaji kumpa nafasi ya kusikilizwa, hakunaga kupeana nafasi ya kusikilizwa why swala asiliwe porini huko, ni survival for the fittest, sasa sisi ni wanadamu sio wanyama wa porini, hatutakiwi kuishi kwa survival for the fittest, wewe mwenye mamlaka na upanga na rungu, unaamua kufanya chochote kwa wasio na mamlaka, ndio maana Katiba ikawepo na sheria, ili kuweka utaratibu wa kuishi na kuadhibiana ili tujitofautishe na wanyama. lazima utawala wa sheria uzingatiwe.

Zaidi sana, jueni hayo mamlaka mliyopewa mmepewa na wananchi (waliomchagua mteule wenu) na ndio mnaotakiwa kuwaheshimu na kuwatendea kazi mkijua mshahara mnaoupata ni kodi zao, wamewaweka hapo ili muendeshe nchi yao tu sio kwa sababu wanawapenda sana.
 
kinachotofautisha utawala wa hayawani/wanyama na utawala wa wanadamu ni kwamba, utawala wa wanadamu unafuata misingi ya sheria, rule of law. mojawapo ya kanuni hizo za utawala wa sheria ambazo ni za asili kabisa ni kwamba usitoe adhabu kwa mtu au kikundi kabla ya kuwapa nafasi ya kusikilizwa/kujitetea. hivo ninyi wateuliwa wa serikali ishini mkijua hilo au la kuna siku mtaashitakiwa kibinafsi na kulipa mamilioni kwani serikali haitashitakiwa kwa makosa yenu ya kibinafsi yaliyo nje ya sheria zilizowapa wenye mamlaka kuwateua. mnateuliwa kwa mujibu wa sheria, lazima mtii sheria na katiba (mama wa sheria zote) au la mtakuja mlipe watu fidia.
 
wateule wengi wakishikishwa rungu huwa wanakuwa na kiburi sana, hata misingi ya sheria huwa hawafuati. mmepewa rungu kwa mujibu wa sheria na katiba, fuateni utawala wa sheria. wapeni watu haki ya kusikilizwa vya kutosha kabla ya kutoa maamuzi yatakayowaathiri, au la mtasababisha athari kwao wakati wana haki tu, na wakiamua wanaweza kuwafungulia kesi ninyi binafsi kwa sababu serikali haiwatumi mfanye kazi bila kufuata sheria zilizotumika kuwateua.
 
Back
Top Bottom