Oktoba 29 hadi 30, walionekana waandamanaji waliokuwa wakipinga zoezi la uchafuzi uliokuwa ukiendelea. Kulikuwa na ushahidi wa watu, hasa vijana waliofanya jambo hilo, picha zipo na mwonekano halisi ulitambuliwa.
Kwa maoni yangu, kwa kukadiria tu kutokana na mwonekano huo toka sehemu mbalimbali nchini, naweza kusema idadi ya washiriki haiwezi kuwa zaidi ya milioni tano tu kwa nchi nzima.
Nimesema hili linatokana tu na kukadiria kwa kutazama ushahidi wa matukio mbali mbali yaliyo onyeshwa kwenye picha.
Tume ya uchaguzi imemtangaza Samia Suluhu Hassan kuwa mshindi kwa nafasi ya urais, kwa kupata kura milioni 31.9 (31,913,866); asili mia 97.66 ya kura zote zilizopigwa siku ya uchafuzi..
Walio jiandikisha na kuwa na sifa ya kupiga kura walikuwa ni waTanzania milioni 37, kwa maana kwamba walioitikia wito wa kupiga kura walikuwa ni asili mia 86.2.
Maana yake ni kwamba palikuwa na mwitikio mkubwa sana wa wapiga kura na kujitokeza kutimiza HAKI yao ya kuwachagua viongozi wao. Takwimu za aina hii ni nadra sana kuzipata katika nchi yoyote humu duniani; siyo kwenye hizo nchi zinazo fahamika kuwa za kidemokrasia, na hata kwenye nchi za mlengo wa kikomunisti.
Hawa waTanzania wenye mwitikio mkubwa namna hii; hawa wametoka sayari gani hawa?
Lakini nirudi kwenye dhumuni la mada hii. Wingi wa watu milioni 30 hauwezi kufichika hata kwa mwonekano tu.
Kwa hiyo basi, naomba wote wenye ushahidi wa waTanzania kupanga misululu nchi nzima ili wamchague Samia Suluhu Hassan kuwa rais wao watuonyeshe tu picha hizo, popote pale walipoona watu wakijipanga mistari kusubiri kupiga kura.
Watu kiasi hiki hawawezi kutoonekana kwa siku hiyo moja ya zoezi hili.