Abul Aaliyah
JF-Expert Member
- Nov 8, 2016
- 7,828
- 5,969
Wapinzani wanaoshinda viti vya Ubunge wanashindaje? Kwa nini hiyo mbinu ya kushinda Ubunge isitumike kushinda kiti cha Uraisi?
Membe hana ushawishi, hata ACT- Wazalendo wanajua hilo. Lakini kuna mambo mawili ya kutafakari: 1. ACT wanataka wamtumie angalau kuwapa mbunge mmoja kule kusini. 2. Wanataka kumtumia ili kuwachokoza Chadema na baadaye kuisaidia CCM ( do not trust both Zitto & Maalim). Kwanza, ACT watahubiri coalition yenye kutaka Chadema na ACT wawe na mgombea mmoja ambaye ni Membe, na Chadema haitakuwa rahisi kuwakubalia, na ndipo wimbo wa kwamba Chadema ni wabinafsi na wapenda madaraka utaachiwa hewani ili kuwapaka matope CDM!Hesabu za Membe hazipo sawa sawa. Lowassa alifanya timing muhimu mno. Mwaka pekee ambao tungeshudia Upinzani ukishika dola ulikua ni 2015. CCM ni chama kinachobadilika kulingana na mazingira. Kinajikosoa na kubadilika.
1. CCM ilikua imechukiwa na raia. Hivyo 2015 ilikua ni karata muhimu kuiondoa CCM madarakani.
2. Lowassa alikua na umaarufu na uwekezaji mkubwa kwenye safari yake kuelekea IKULU. Sioni Membe akifika hata nusu za harakati za Lowassa.
3. Membe anakwenda kupambana na CCM iliyorudisha imani kwa raia. Anakwenda kukutana na siasa za Upinzani zilizogawanyika. Sitegemei ile spirit ya UKAWA kuwa live. Mwaka 2015 kulitokea kusalitiana. Vyama vya upinzani haviaminiani kirahisi.
JPM hana mbadala, anapendwa na watu wengi, Wengi wanamwamini na kwa namna alivyoshughulika na Corona hili limempa credit sana tena sana, Kazi yangu inanikutanisha na watu wengi sana, kuna watu walikuwa wanampinga ambao ni Wapinzani Kinda kinda nimeshangaa sana kwa sasa huwaambii kitu.
Ukiondoa kelele za kwenye mtandao hamna mbadala.
Siasa ni sayansi, hautoamini kinachoenda kutokea!Nabashiri matokeo kuwa hivi:
1. Magufuli 90%
2. Mgombea CDM 09%
3. Vyama vingine 01%
Nakuambia ukweliiii.Endelea kuota
Hesabu za Membe hazipo sawa sawa. Lowassa alifanya timing muhimu mno. Mwaka pekee ambao tungeshudia Upinzani ukishika dola ulikua ni 2015. CCM ni chama kinachobadilika kulingana na mazingira. Kinajikosoa na kubadilika.
1. CCM ilikua imechukiwa na raia. Hivyo 2015 ilikua ni karata muhimu kuiondoa CCM madarakani.
2. Lowassa alikua na umaarufu na uwekezaji mkubwa kwenye safari yake kuelekea IKULU. Sioni Membe akifika hata nusu za harakati za Lowassa.
3. Membe anakwenda kupambana na CCM iliyorudisha imani kwa raia. Anakwenda kukutana na siasa za Upinzani zilizogawanyika. Sitegemei ile spirit ya UKAWA kuwa live. Mwaka 2015 kulitokea kusalitiana. Vyama vya upinzani haviaminiani kirahisi.
Membe hana ushawishi, hata ACT- Wazalendo wanajua hilo. Lakini kuna mambo mawili ya kutafakari: 1. ACT wanataka wamtumie angalau kuwapa mbunge mmoja kule kusini. 2. Wanataka kumtumia ili kuwachokoza Chadema na baadaye kuisaidia CCM ( do not trust both Zitto & Maalim). Kwanza, ACT watahubiri coalition yenye kutaka Chadema na ACT wawe na mgombea mmoja ambaye ni Membe, na Chadema haitakuwa rahisi kuwakubalia, na ndipo wimbo wa kwamba Chadema ni wabinafsi na wapenda madaraka utaachiwa hewani ili kuwapaka matope CDM!
Yes, but pia Tuvuke na mipaka hadi Malawi, Zambia, Kenya... Kisha tulinganishe na hali ya tz. Chochote chawezekana. Even people in rural understand ...Mimi CCM damu damu. Napenda tume huru, napenda mihimili huru inayofanya kazi kwa weledi.
Kwa sasa ni ngumu sana upinzani kutoboa, nasema kushinda hata iwepo tume huru bado ni ndoto.
Hizi siasa zetu za mitandaoni zinazofanywa na wenye mtazamo chanya wanaoweza kung'amua mambo ni sehemu ndogo sana ya wapiga, na mbaya zaidi asilimia kubwa ya hawa waelewa huwa siku kupiga kura hawajitokezi kupiga kura.
Hata kama chama changu tawala kina kasoro zake kitapita tu maana wanaopiga kura ni watu wa kawaida, japo wengi wana maisha magumu ila wataenda kupiga kura kutokana na sifa wanazosikia bila ya hata kufahamu uhalisia wa sifa husika.