Hesabu za gizani za Membe

Oct 7, 2019
51
156
Nimemsikiliza Membe Sana Wiki hii, inaonyesha kapania kweli kweli kugombea. Analalamika Sana kuhusu kanuni za CCM, kuhusu Adhabu yake, kuhusu katiba ya nchi nakadhalika.

Huyu jamaa anaweza akawa na plan B ya Siasa na tunaweza kukutana na Surprise huko mbeleni.

Kuna uwezekano Membe akaangukia ACT wazalendo na sio Chadema Kama wengi wanavyomtabiria. Huyu Kuna asilimia zaidi ya 80 katika hesabu zangu za Ramli akahamia ACT Wazalendo.

Kwa nini ACT na Sio Chadema

Kwa haraka haraka ACT niliwaambia watauzika zaidi Zanzibar kuliko bara hii ni kutokana na uwepo wa Maalim Seif kule Zanzibar. Hili halina ubishi Vita ya Zanzibar inawahusu CCM na ACT.

Kwa maana hiyo ACT wanatafuta mtu Strong huku bara wa kuwasaidia kuitikisa CCM na kwa hesabu zilizopo Membe anaonekana Kama mtu Sahihi na huenda wameshakubaliana.

Kwa Nini ACT watamchukua Membe na sio mwingine?
Watamchukua Membe kwa sababu kuu mbili kwanza ni mtu anayekuja na utamaduni usio Rasmi wa CCM wa kuachiana kijiti kwa miaka kumi. Watu wanataka kumsikia kabeba agenda gani.

Pili ACT wanamuona dili kutokana na eneo analotokea la mikoa ya Kusini. Kiashiria kikubwa Cha hili Ni Mbunge Suleiman Bungara kuhamia ACT kwa haraka na ameshawahi Siti. Bungara ni Mbunge ambaye anajua kusoma alama za Nyakati kwa Siasa za Kusini. Kama akihamia ACT, CCM itakuwa inakutana na Hali isiyoeleweka ukanda huu wa Kusini. Tukumbuke kwa miaka ya hivi karibuni Mikoa hii imekuwa na Siasa zisizoeleweka.

Hesabu zetu CCM zilienda vibaya kumtimua Membe?
Kama akihamia ACT Basi tutakuwa tulipiga hesabu vibaya. Nilitamani reconciliation mapema Sana. Wakati fukuto la udikuzi wa simu lilipoibuka ndani ya CCM solution yangu ilikuwa kufanya reconciliation. Ila niliambulia wazee wawili na Vijana wawili kwenye fukuto lile. Niliambulia wazee Kinana na Yusuph Makamba na Vijana Nape na January Makamba Membe tukamtosa.

Kuna msemo wa kiingereza unasema "an intelligent person knows how to solve any problem. A wise person knows how to avoid that problem.

Hapa tulikataa kata kata kutumia Busara (Wisdom) kumaliza tatizo mapema. Narudia a wise person knows how to avoid that problem hapa baada ya kuona kimbelembele Cha Membe tungetumia Wisdom (Busara) kummaliza tungemtafutia ubalozi kule Somalia au Syria, ni saa ngapi angelitoka njee aite press? Akitaka kuja nchini ni mpaka aombe kibali wizara ya Mambo ya njee.

Kwa Nini Membe anataka Urais Sasa?
Ndani ya CCM kuna utaratibu mwingine ambao Ni mzuri Sana wa kuachiana kwa awamu kijiti Cha kugombea Urais kwa kufuata misingi Fulani hivi ambayo sitaitaja hapa. Kwa maana hiyo ili Membe aje agombee ndani ya CCM atahitaji kusubiri miaka 15 ijayo toka Sasa kwa Sasa ana miaka 67 ukijumkisha na miaka 15 ijayo atafikisha miaka 82. Kiuahalisia atakuwa ameshapoteza Ramani ya Siasa na atakuwa kazeeka Sana.

Nani mwingine atapiteza Kusini?
CUF ya Prof Lipumba ilikuwa inafaidika na Siasa za Kusini lakini kwa Sasa ACT wanazipigia hesabu na nafasi ya Cuf Wanaitaka huko Kusini kama hesabu hizi za Membe na Ramli yangu itakaa sawa.

Hitimisho.
Kama hesabu zikienda hivi bila kubadilika ACT itakuwa ni chama kinachotaka kuongoza Siasa za Upinzani nyuma ya NCCR Mageuzi ambayo hesabu zake Ni kushika usukani wa Siasa za Upinzani. Vita ya kuongoza Siasa za Upinzani itahamia kwa ACT VS NCCR Mageuzi.
Tunaweza kuzirudia hizi Hesabu zikakaa sawa kabla ya uchaguzi mkuu. Bado tunaweza kuepuka kutumia nguvu kubwa na fedha nyingi 2020.

All in All ningepewa nafasi ya kukutana na Membe ningemshauri afungue Kampuni la Korosho huko Kusini awasaidie Wana kuchele... Atapoteza zaidi akiziamini hesabu zake hizi.
MEMB.jpg
 
ZABURI 130

1 Ee BWANA, toka vilindini nimekulilia.

2 Bwana, uisikie sauti yangu, masikio yako na yaisikilize sauti ya dua zangu.

3 BWANA, kama Wewe ungehesabu maovu, Ee Bwana, nani angesimama?
 
Hakuna plan B hapo jamaa hajasoma alamaza nyakati. Hakuna mtu alikuwa na nguvu kama Lowassa ila yuko wapi? Alikuja soma alama akiwa kachelewa lakini afadhari alijua kuwa ni muda wa kupumzika.

Membe hakuwahi kuwa na mvuto kihivyo kwa watanzania yani ni sawa na Sumaye.
 
Hivi NCCR mageuzi ya mbatia ina nguvu gani kiasi icho? mbona mnaikuza sana

Kimsingi NCCR haina nguvu yoyote kutoka kwa wapiga kura, na Magufuli ana nongwa na chuki ya wazi kwa cdm. Ukiangalia sasa hivi hakuna tume huru ya uchaguzi, na rais kwa kutumia madaraka yake vibaya, anaweza kuagiza tume imtangaze amtakaye. Hivyo amepanga kuwapa NCCR viti kadhaa maana wamekubali kumsujudia, kwani hawana uwezo wa kushinda chochote kwenye uchaguzi halali. Hivyo watapewa viti kadhaa vya mbeleko ili kuuhadaa umma, na dunia kuwa kulikuwa na uchaguzi huru, ndio maana wapinzani pia wameshinda.

Kwahiyo NCCR wameahidiwa kupewa viti kadhaa ili wawe chama kikuu cha upinzani, kwa sharti la kufanya siasa zinazotakiwa na ccm. Lengo hasa la kubebwa huko ni ili agenda ya kumuongezea Magufuli muda wa kukaa madarakani zaidi ya miaka 10, wawepo wapinzani wa kuunga mkono. Hivyo hawa wapambe wanacholeta hapa, ni mpango wa nyuma ya pazia unaosubiri kutekelezwa.
 
Siwezi kumpa Membe kura yangu, eti kwa sababu simtaki Magufuri.

Ila aendelee kuwepo tuu, ili anogeshe uchaguzi.
 
Wewe unajaribu kumjenga membe ok.

Ila elewa kitu kimoja anachoifanyia mageuzi JPM kwa sasa ni kuifanya CCM kuwa taasisi yenye nguvu kuliko mwanachama mmoja mmoja kama ilivyokuwa hapo awali, na hilo limefanyika kila sehemu ya nchi.

CCM ile ya kina Membe walivyokuwa wana nguvu kuliko chama na kuzaa neno vigogo.
Membe angeweza kuwa na nguvu akiwa ndani ya CCM, lakini akiwa nje ya chama yeye anabaki kuwa yeye na wale anaowagawia pesa ili my mpambe.

Mimemaliza

Kwa taarifa yako Magufuli haifanyi ccm iwe na nguvu kama taasisi. Bali anaigeuza ccm kuwa chama cha kijeshi zaidi kuliko chama cha siasa. Kwa sasa ccm itageuka kuwa chama kinachofanyiwa maamuzi na watu wanaomsujudia mwenyekiti, na sio wanachoamua wanachama. Kwa mantiki hiyo, haya maono ya mwenyekiti ataigeuza ccm kutoka kuwa chama cha ushawishi, na kuwa cha shuruti, na kitategemea zaidi nguvu za rais, kuliko chama kama chama. Mbinu yoyote yenye nia ovu huwa haina mwisho mzuri. Muda utasema hili.
 
Back
Top Bottom