Eng. Y. Bihagaze
JF-Expert Member
- Sep 8, 2011
- 1,488
- 908
Tulishakubaliana
Tokea darasani Kwamba hesabu ni maisha, maisha ni hesabu. Lini ikapita siku ukaimaliza pasipo kufanya hesabu? Kama hujanunua kitu, hujahesabu fedha,watu&vitu Bado siku haijaisha. Hata Mtu ambaye hajakanyaga kitu darasa automatic anajikuta akipambana Na mazingira ya hesabu daily.. Lakini nashangaa sana watu hesabu rahisi zinawachanganya..
Neno MUUNGANO linatokana Na neno la lughaflanhivi "UNION" au "U" . Na kuna hesabu rahisi Zake za seti Za vitu au namba. Hebu ona
Ukipewa seti mbili A Na B Kwamba :-
A = {a,c,f}
B = {a,b,d,e}
Ukaulizwa swali tafuta MUUNGANO wa Seti A na Seti B, walituambiaga tunaandika (AUB) utapata kitu hii..
(AUB) = {a,b,c,d,e,f} = (u).
MUUNGANO wa seti hizi mbili unazaa SETI mpya moja (u). Ni Kazi ngumu ya kiendawazimu Kama Mwalimu atauliza akikupatia seti (u) peke yake akakwambia tafuta iliyokuwa SetiA Na SetiB, ni kitu kisichowezekana.
Labda hesabu ngumu twende Kwenye kemia, MUUNGANO ni SOLUTION.. Two soluble compound dissolve to form a single state solution. Mfano sukari na Maji, ukichanganya unapata kimiminika kipya kimoja. Ni Kazi kubwa Na ngumu kutenga tena sukari Na Maji . Wanakemia walitumia mifumo(analysis) (volumetric & qualitative) kujaribu kugundua viasili vya muungano Wa kimiminika flan wakaishia kusema labda(probably) kulikuwa na sukari kiasi flan Na Maji lakini SIO halisia.
Kwanini natumia semi hizi, kuna vitu vya UONGO tumeviamini Na kuviishi kwa miongo takriban mitano sasa Yaani from 1864. Kuna kitu kilichobatizwa Kwa Jina la Muungano wa Tanganyika Na Zanzibar ikazaliwa Tanzania. Ndugu zangu watanzania, nachukua fursa hii kupiga mbiu, tutokeni usingizini. Tusitishe fikra hizi sasa, huo wa 1964 hauwezi kuitwa Muungano. TANZANIA HAKUNA MUUNGANO HILI LIWE WAZI KABISA. Tunaweza kugombana sana, tukatafutana ubaya, tukanyosheana vidole Na kuoneana ubaya bure. Tutazogoana mwanzo-mwisho, tutausema Muungano vibaya au vizuri. Tunapigana Na tusichokiona, tunashambulia hewa, kimsingi HATUNA MUUNGANO. Ni Muungano wa wapi iwapo kipande kimoja Cha Nchi Bado Kina serikali?. Sitaki kuingia Kwenye mamia ya changamoto Za kitu kinachoitwa muungano Maana HAKIPO. Tukiendelea kuamini hivi tutaumizana pasipo Sababu. Kama Muungano ungekuwepo Basi Zanzibar Leo ingekuwa mkoa tu wa Tanzania Kama ilivyo Iringa,Dodoma au Singida. Lakini sintofaham hizi zinatufanya tuabudu tusichokijua..
Mheshimiwa RAIS, mbali Na Changamoto zilizopo embu weka Jambo moja tu la Kihistoria katika UONGOZI wako, TULETEE MUUNGANO TANZANIA. Yaani Tanzania(tanganyika + Zanzibar) Na Zanzibar I mean {[Tanganyika, Zanzibar] + Zanzibar } ziwe kitu KIMOJA sasa. Tuwe Na Tanzania Moja. Hakuna Cha serikali ya mapinduzi Wala serikali ya kipinduzi. Nchi iwe moja, Jina Liwe Moja. Tuacheni Complication zaidi. Umaskini wenyewe umeshatutafuna Bado tutafunwe tena Na zigo la maserikali mengi tutapona kweli??!?. Tuacheni ujinga. Tuundeni Muungano SIO kiinimacho Kama Wazee wetu walivyotulazimisha tuamini. Sisi vijana tuna mustakabali Mkubwa Kwa Taifa letu, Young people MAY die but old one MUST die. We must Protect our people and our nation
Tuwe Taifa Moja, Serikali Moja, Bunge Moja, Jeshi Moja, Sarafu Moja.
Libarikiwe Taifa hili.