He's back

pisi jacky

Member
Oct 21, 2020
32
150
Bwana Bwana Bwana acheni....
Wahenga wanasema hakuna mkate mgum kwenye chai, na kila kubwa na kubwa yake.....
Nawasilim wakuu ,
Two weeks ago nileleta uzi wangu bout how hard imekua kwangu kuweza kumoove on since niachane na mwanaume ambae kusema ukweli nilimpenda mno mno

Hadithi inaanza tarehe moja jion naona sms new number hey babe!
Nkastuka sinaga Mambo Ayo siku izi nani tena uyu?! kuangalia namba vizuri si ya mwingine ni ya yule yule alienifanya niwe kichaa, maana nimeifuta ila kichwani bado ipo.

Sikujibu,. Ikaingia nyingine hey Jackie mie kimya. akapiga sikupokea... Mida ya sa tatu nkaingia kulala, usingizi hauji nageuka tu.
Nkaskia tena message kusoma ni yeye.. I just wanna talk to you!!

This time ikanibidi nijibu maana nkakuta nakabwa
Nkamjibu huwezi niacha kwa amani ?

Nkajibiwa I can but amani yangu unayo wewe

Nkamjibu ibilisi mkubwa wewe umeachwa uko unaludi kwangu kupozea maumivu hebu niache

He replied; am no longer that man you used to know

I replied you're always who you are nataka kulala niache

He replied nights my queen

Basi Bwana asubui sa kumi nkaona text I can't sleep

Nkajibu unawanga?

He replied stop it hebu acha basi
Can I see you
Me kimya......
Another text Jackie can I see you

Nkamjibu ulisema utaoa mwanamke mzuri sana na utanialika kwenye harusi yako vipi ndo unantafuta unialike au?

He replied you're always that beautiful woman sion kama kuna mzuri Zaid ako in this world

I replied kazana kutafuta wapo kibao

He replied please can I see you

Me kimya
He replied; truly I miss you

Me kimya
Nkaenda kazini the whole day akawa akituma text non stop sio kawaida ake mpaka nkajiuliza au ana cancer anataka kufa maana ameniganda visivyo
Usiku ukafika naomba nkuone nkamwambia niko bize sina muda

He replied najua una muda sema hutaki

Nkamwambia unanimalizia chaji kujibu text zako nina watu wengi muhim wa kuchat nao mwishowe sim izime chaji nishindwe kuwasiliana nao

He replied; I miss you beautiful please let me see you
Kidogo nikaanza kua mpole zile short answers zikaanza kupungua nkamjibu nikipata mda ntakwambia

He replied I can't wait any longer I just wanna see you. najiuliza huyu anataka kufa huyu si bure kabisaaa si bure nkamwambia labda weekend
He replied mbali sana...
Nkajibu utajua wewe.
I don't know how?!! but kesho ake nkawa nimeenda kazini, akawa kimya the whole day....basi kila saa naishika sim kuona kama kuna text ake nilivoona kimya nkasema alikua ananjaribu tu, jion nkaludi nyumbani naishi mwenyewe mida ya sa moja naona message nipo apa nje kwako sikujibu ata maana najua asingeweza pajua kwangu nkaisikia kama honi nje kutoka ivi...
Lahaula macho kwa macho na israel mtoa roho nkafunga geti kwa spidi mno nisiamin ninachokiona.
Nkakuta sim inaita ni yeye
Honestly I was shaking hadi ikakata ikaita tena nkapokea kwa upole sana ambao sijawai kwakweli kuuexpirince akaomba afunguliwe geti nkawa kimya for a minute not knowing what exactly to do, nkakata sim ikaingia text am staying here until you open the door.
Nkawa kimya kiukweli nilikua na maswali mengi amepajuaje kwangu? amefikaje? why is he here? Ilipita nusu saa ikaingia message nasubil unifungulie ikapita lisaa nikaona tena text please niruhusu niingie ndani.

Nkamtext mdogo angu wa kike nikifa ni flan kaja kwangu leo.
Nkatoka nje nkamfungulia sikumkalibisha ndani nkamletea kiti nje ananiangalia usoni utafkili kaona hela sijui mi simuelewi ani simuelewi.

He started hi ,
Nkamjibu hi, kwanza umepajuaje apa
He replied; kwani ugomvi, I just wanna talk
Nikakaa enhe haya ongea

Kama muvi ya kihindi Bwana si akapiga magoti Bwana bwana bwana kimoyo moyo nkasema huyu lazima anakabilia kufa wala sio mwanaume wa kupiga magoti lazima kuna jambo.
Akaanza kuomba msamaha na machozi, hapo ndo nkajua kabisaaa huyu tunazika huyu, kuna shida mahali uyu mwanaume ninaemfaham mim eti apige magoti afu alie hamna io kitu.
Mi nkabaki namshangaa tu Bwana we naona mtu analia adi anashndwa kujieleza ikumbukwe ni miaka minne imepta. Yaan mi namshangaa namshangaa
Nkasema huyu akiingia tu ndani atajiliza we anikule sasa nkamwambia nenda nyumbani tutaongea kesho,
Ha ha kuskia ivo ova kapewa kataarifa za msiba kilio icho hadi nkaogopa majirani wasije sikia.
Ikabidi nimkalibishe ndani, I've never seen him like this miaka yote niliokua nayo.
Basi kumuingiza ndani ndo akaja miguuni kabisa Lia miguuni kwangu omba msamaha kama wote, kiukweli mi nilikua namshangaa tu.. uyu anaigiza kama sio kuigiza uyu anakufa kabisaaa yaan ilinichukua muda kidogo kucopup na tukio yaan mpaka hisia kuja ilinichukua muda kwakweli.
Ikabidi nianze kumbembeleza basi nyamaza maana umelia tangu unafika
Kaiva uso wote na ile rangi ake sasa kawa mwekunduu
Alivonyamaza kajieleza weeeee, apo usiku mkubwa tayari
Kiukweli nilimuhulumia ila sio kivile nkamwambia kama unalala lala apa mi nalala chumbani yaan nilikua napata wakati mgum kuamini kinachoendelea. Akanijibu yes ntalala apa nkaingia nkamtolea mashuka ya kujifunika nkamkuta bado analia.

Basi nkamwambia usiku mwema
Mi nkaingia chumbani bwana wee kumbe dakika inaweza kua lisaa, muda hauendi usingizi hauji akantext njoo sebleni sipati usingizi njoo niwekee ata muvi.
Apo tayari nishavua nguo nipo na night dress, si nkaamka nikawasha tv nkampa remote nkamwachia nkamwambia utachagua mwenyewe.
Ile nampa remote nkadakwa mkono nkasema ukingusa napga kelele. Mwe mwanaume ni mwanaume akanijibu serious hebu piga izo kelele,
He stood and hug me akasema sikufanyi chohochote I just want to tell you u look beautiful,
Akaniachia niende kufika chumbani nkawa nahisi maluwe luwe,
Nkavuta pumzi nsielewe nini kinaendelea.ikabidi niludi sebleni mwenyewe kumuuliza amefata nini au ana lengo gani na mim
Akanijibu niluhusu nkusogelee jaman nimejionea muvi za kihindi akasimama ile zero distance vitu vingi vili ring kwenye akili yangu sielewi hisia zilikotoka nililia mno mno
Nikabembelezwa Bwana kama wazungu afu akanambia nenda kalale kama kweli vile,
ile nasimama nkakumbatiwa kuambiwa good night,
Kilichofwata mi mwenyewe ata sielewi ni nin kiliendelea
I just realized he was always on mind na all this while I couldn't move on because moyo wangu ulimtaka yeye tu
Sijui kaja kuniigizia muvi sijui juzi ulikua birthday yangu nkaona mpesa imethibitisha umepokea million kutoka kwake ikafwata text, happy birthday love nunua unachotaka. nkashangaa nkasema uu muamala atauhailisha huu haya maigizo ya harmonize na kajala haya.. ila sijui labda kweli kabadilika maana hela nilitoa ilikubali
Mwe sijui ntaolewa safari hii labda ntavaa shela maana amerudi wamoto hatari maana nazeeka
Uzi umeisha.
 

Waaai

JF-Expert Member
Jan 14, 2021
1,299
2,000
Hakuna kaorganism kalikolia pia?

Maana ss wanaume ni carrier wa kiorganism cha kansa ya mlango wa kizazi, kirusi HIV japo nasi tunapata, kaspem ka mimba n.k
 

ruhi

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
2,506
2,000
Kwenye ujana kuna mengi sana; kweli wazee wamepitia mengi.
Unadai unazeeka lakini unashindwa kuelewa adi ujanja wa vijana wakitaka kala mzigo?
Pole sana japo ndo njia ya kuelekea uzeeni ili uje uwasimulie wanao na wajukuu siku ukiwasikia wanakuletea stori hizo huku wakitokwa na machozi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom