Hersi Said: Wadau wa soka tutaendelea kukuunga mkono Rais wa TFF Wallace Karia

Hersi Said: Wadau wa soka tutaendelea kukuunga mkono Rais wa TFF Wallace Karia

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
🎙ENG. HERSI KUHUSU KARIA 👇

🗣"Nikuhakikishie sisi kama wadau wa soka tutaendelea kukuunga mkono Rais wa TFF Wallace Karia na Kamati ya utendaji, nipongeze wazo zuri ambalo kaka angu Mangungu amelitoa na mimi naliunga mkono kwa asilimia 100%, sisi wajumbe wa mkutano mkuu tumelipitisha."- Eng. Hersi Said Rais wa Klabu ya Yanga wakati anazungumza kwenye mkutano mkuu wa TFF uliofanyika Desemba 21 pale Moshi, Kilimanjaro.

🗣"Mafanikio makubwa ambayo Rais Wallace Karia pamoja na kamati yako ya utendaji ya TFF yamekuwa ni sababu ya maendeleo ya mpira wa miguu kwenye taifa letu sisi kama wanamichezo katika taifa hili tunajivunia sana uongozi wako, tunajivunia utendaji wako, tunajivunia uchapa kazi wako."- Eng. Hersi Said Rais wa Klabu ya Yanga wakati anazungumza kwenye mkutano mkuu wa TFF uliofanyika Desemba 21 pale Moshi, Kilimanjaro.

Uchaguzi wa shirikisho la soka nchini TFF utafanyika Agosti 16 katika mji wa Tanga na zoezi linaloendelea kwasasa ni uchukuaji na kurudisha fomu za maombi kwa nafasi mbalimbali.
1750077878826.jpeg
 
Kumuunga mkono Wallace Karia ni kuunga mkono ubadhirifu, rushwa, upigaji, undolanga, ubaguzi, upendeleo, ubabaishaji, ubinafsi, ujinga, nk.

Ni wakati sasa wa kuchagua watu wa mpira, badala ya wanasiasa/mamluki wa ccm.
 
Kumuunga mkono Wallace Karia ni kuunga mkono ubadhirifu, rushwa, upigaji, undolanga, ubaguzi, upendeleo, ubabaishaji, ubinafsi, ujinga, nk.

Ni wakati sasa wa kuchagua watu wa mpira, badala ya wanasiasa/mamluki wa ccm.
Hao ni ndugu!Wewe shabiki ndo unazugwa.Waangalie vizuri wana asili Moja.Poleni nyie mashabiki.
 
Aliungwa mkono kipindi kile cha uongozi wake. Hakuna kiongozi yeyote ambaye angempinga nje nje kwa kuwa alikuwa madarakani sasa muda wake umeisha na miaka yake ya uongozi imeisha awaachie wengine sasa
 
Chini ya Karia Tz mmefika mbali sehemu nyiingi.....Ajaye asitoke mbali atoke humo humo Mana I'll eneo sio la kumpa Mtu ajipatie uzoefu.
 
Back
Top Bottom