Heri ya Siku ya Wanawake 2019 kutoka JamiiForums

Asha D Abinallah

Senior Member
Apr 5, 2015
140
904
31A3779E-34B0-4C83-86EF-3F9D5B27819F.jpeg

Leo, Machi 8, 2019 ni siku kama siku nyingine yoyote ile katika maisha yetu lakini kinachoifanya iwe na tofauti ya kipekee ni sababu kwanza Mwenyezi Mungu katujalia kuiona leo ukifananisha na wengi waliotangulia mbele ya haki, na pili sababu ni siku ya kumsheherekea na kumuenzi mwanamke na nafasi yake katika jamii na maisha yake ya kila siku.

Kwanini tunamsheherekea Mwanamke?

Sababu kubwa ya kumsheherekea na kumuenzi Mwanamke ni kumkumbusha kuwa nafasi yake katika maisha inathaminiwa, inaonekana, ina mafanikio na ni msingi kwa familia na jamii kwa ujumla. Kwamba inawezekana hajafika anapopalenga, inawezekana bado hajapata mafanikio anayotarajia, inawezekana anapata changamoto kubwa ya muda mrefu kama vile kuwa ‘single mother’ au mjane, inawezekana anaumizwa kwa mambo mengine mbalimbali hadi akasahau umuhimu na thamani yake lakini bado anasonga mbele bila kukata tamaa tena kwa bidii zote.

Kusheherekea kunatukumbusha kwamba hata hatua hii tuliyoifikia tayari ni sehemu kubwa ya mafanikio tunayostahili kujipongeza kwa jitihada hizo, haswa ukizingatia umetoka mbali na bado upo unasonga mbele.

Silaha thabiti ni kutokata tamaa na kujifunza kufurahia yale ambayo ni mazuri katika maisha yetu iwe mawasiliano, mahusiano na ushirikiano na pia kujifunza kujenga furaha kwa waliokuzunguka kwa kuwa mtu mwenye furaha na mwenye kusambaza furaha.

Sisi JamiiForums tunajivunia kuwa na Wanawake wanaojielewa, wanaojitambua na kuwa na michango thabiti kwenye jukwaa letu pendwa. Wanawake katika jukwaa hili wamekuwa wakiongoza kwa kuwa na lugha ya staha, matumizi sahihi ya jukwaa na ushiriki wenye manufaa kwa wengi wakiwa katika Majukwaa mbalimbali hapa JamiiForums. Kumekuwa pia na ongezeo kubwa la wanawake kuwa sehemu mbalimbali za uongozi, mipangomikakati na maendeleo ya kijamii ikiwa imechangiwa na ushiriki wao hapa Jukwaani ama moja kwa moja ama kwa jamiiana (social-networking) na wale wanaokutana nao hapa.

Ni kwa misingi hii, tungependa kuwashukuru kwa dhati kwa uwepo wenu hapa na hivyo kujiona wenye bahati ya kuwa nanyi na kuwatakia sikukuu njema ya Wanawake.

Mwaka huu kauli mbiu ni #BalanceForBetter ni matumaini yetu kuwa kauli hii haitaishia kutajwa hivyo bali kila mmoja katika jamii ashiriki katika kujenga jamii inayotoa haki sawa kwa wote.

Happy International Women’s day 2019!

JamiiForums Team
 
Mkuu,

Hamjakwama popote. Hii ni siku yenu pia ya kumuonyesha mwanamke yeyote aliyekuzunguka kwamba wewe si kama wale ambao wameathiriwa na tamaduni kandizi za kumuona mwanamke kutokuwa na tija, kutostahili heshima na kutostahili haki yoyote bali kwa njia ya kumuonea huruma or kumfanyia ‘favors’

Hongera zenu wanaume sijui tunakwama wapi inabidi tuanzishe siku yetu na sisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi JamiiForums tunajivunia kuwa na Wanawake wanaojielewa, wanaojitambua na kuwa na michango thabiti kwenye jukwaa letu pendwa. Wanawake katika jukwaa hili wamekuwa wakiongoza kwa kuwa na lugha ya staha, matumizi sahihi ya jukwaa na ushiriki wenye manufaa kwa wengi wakiwa katika Majukwaa mbalimbali hapa JamiiForums.
Hii point yako imezingatia wale wanaotumia identities zisizokuwa zao? Au hili jambo halipo JF?
 
Back
Top Bottom