Heri ya siku ya Baba Duniani 2017 (Happy Fathers Day)

Joseverest

JF-Expert Member
Sep 25, 2013
51,993
69,391
Habari za muda huu wana JF! Natumai mko poa sana..

Leo Jumapili June 18 2017 ni siku ya Baba duniani.

Karibuni tujumuike katika kuwapongeza Baba zetu popote walipo..

Salamu zangu za leo

Baba yangu mzazi popote ulipo nakushukuru sana kwa malezi uliyonipatia hadi leo, umekuwa msaada mkubwa sana kwenye maisha yangu... Naahidi kukupenda, kukuthamini na kukulinda kadiri niwezavyo..

Kwa wale ndugu zangu ambao Baba zao wametangulia mbele ya haki nipende kuwapa pole na Mungu awape heri na vilevile awarehemu Baba zetu huko walipo..


Tunaotarajia kuwa Baba tujiandae kwa majukumu ya kuitwa Baba..Tusinyanyase familia zetu, tuzipende na tuzithamini kwa ustawi wa jamii..


Wadau karibuni tuonyeshe upendo kwa Baba,Dad, (Dingi) zetu!!


[HASHTAG]#MsimsahauNaMamaPia[/HASHTAG]
[HASHTAG]#HappyFathersDay2017[/HASHTAG]







 
hakika najivunia kuwa na BABA
Sijawahi kujuta kuwa mwanawe
asante mshua wewe ndo kamanda wangu mwenyewe wa maisha
mengi ninayokabiliana nayo leo ni muongozo wako mkuu mdingi wangu
NAKUKUBALI KICHIZI YANI WE MWENYEWE UNAELEWA JEMBE LANGU LA TREKTA
 
kuna wengine wangekuwa wanasherehekea siku ya leo
ila wakalazimisha toa toa hiyo sijajiandaa sijui walifikiri ni ngumi hizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…