Popo-
JF-Expert Member
- Jan 21, 2022
- 282
- 575
Igweee...
Ikiwa ni siku ya wababa Duniani,
( Father's Day - Wikipedia ) nimesubiria karibu siku nzima bila kuona shamsham za kupostiwa wa kusherehekewa kama ilivyokuwa siku ya wamama duniani.
Kama mjuavyo, siku hii ina nguvu sana hasa ukizingatia mchango wa akina Baba/ wanaume katika jamii na familia kwa ujumla.
Lakini imekuwa ndivyo sivyo, katika contact list zangu zenye muunganiko wa namba niwezazo kutembea whatsapp karibu 1347, Sijaona hata status moja yenye kutambua mchango wa mwanaume kwenye jamii..
Nimeenda kwenye kurasa zangu za mitandao ya kijamii ikiwapo IG, Twitter na Facebook, hata katika pages kubwa kama JamiiForums Millard ayo hata BBC Swahili sijaona wakiweka post ya kutambua mchango wa mwanaume/Baba kwenye jamii.
Hii inanifanya nifikirie mbali sana kwamba, Baba/Mwanaume mchango wake hautambuliki kwenye jamii kwa sababu labda labda si mtu wa kujionyesha onyesha kwa yale ayafanyayo n.k na yumkini yale yasemwayo kuwa ndiyo maana wanaume hufa mapema, scenario hii ikawa ya ukweli ukizingatia haya ya leo.
Kwa niaba ya Wababa na wanaume wote, niwatakueni siku njema. Mimi mwanaume mwenzenu natambua sana mchango wetu kwenye jamii..
Wanajamiiforum, tuungane kwa pamoja tuwatakie wanaume na wababa wooote "HERI YA SIKU YA WABABA DUNIANI"
Ahsanteni