Sherehe za Mwaka Mpya zimekuwapo kwa muda mrefu. Maandishi ya kale yaliyochongwa yaonyesha kwamba Wababiloni waliadhimisha sherehe hizo katika milenia ya tatu K.W.K. Walifanya sherehe kuu ya mwaka mpya katikati ya mwezi wa Machi. Kitabu cha The World Book Encyclopedia chasema kwamba “wakati huo mungu Marduki aliamua mambo ya mwakauliofuata.” Sherehe za mwaka mpya za Wababiloni ziliendelea kwa siku 11 na zilitia ndani maandamano, kutolewa kwa sadaka, na ibada ya kuomba mvua na mazao.
Mwaka mpya wa Waroma ulianza pia mwezi wa Machi katika kipindi fulani. Lakini mnamo mwaka wa 46 K.W.K., Maliki Juliasi Kaisari aliamua uanze Januari mosi. Hapo mbeleni Januari mosi ilikuwa siku ya Janus mungu wa mianzo na mwaka wa 46 siku hiyo ikawa pia siku ya kwanza ya mwaka wa Waroma. Tarehe hiyo ilibadilika lakini sherehe haikubadilika. Kitabu cha marejeo cha Cyclopedia cha McClintock na Strong kinasema kwamba katika Januari mosi watu “walijiingiza katika sherehe zenye fujo na ulevi, na ushirikina mbalimbali wa kipagani.”
Hata leo, sherehe za Mwaka Mpya zatia ndani ushirikina mbalimbali. Kwa mfano, katika maeneo kadhaa ya Amerika Kusini, wengi hukaribisha Mwaka Mpya huku wakisimama kwa mguu wao wa kulia tu. Wengine hupiga mbiu na kufyatua fataki. Watu wa Jamhuri ya Cheki wana desturi ya kula dengu wakati wa Mkesha wa MwakaMpya, lakini siku hiyo Waslovakia huweka fedha au magamba ya samaki chini ya kitambaa cha meza. Desturi kama hizo ambazo hufanywa ili kukinga bahati mbaya na kuhakikisha ufanisi huendeleza imani ya kale kwamba mambo yatakayokuja huamuliwa siku ya kwanza ya mwaka.
Maoni ya Biblia
Biblia yashauri Wakristo ‘wajiendeshe kwa adabu, si katika sherehe zenye makelele ya ulevi.’* (Waroma 13:12-14; Wagalatia 5:19-21;1 Petro 4:3) Wakristo hawashiriki katika sherehe za Mwaka Mpya kwa sababu mara nyingi sherehe hizo ndizo zenye ulevi na mambo mengine ya kupita kiasi yanayokatazwa na Biblia
Kwa wanaotoka Moshi wanajua mwisho wa mwaka huwa 70%wanenda kufanya nini?
Achilia kufahamiana, kusalimia,kujuana vizuri,kurefresh akili n.k
Una sababu nzuri ya kusherehekea? Iweke hapa.
Chanzo chake umekiona?
Je ni agizo kwenye biblia?