Kada Mzalendo
Senior Member
- Oct 9, 2024
- 182
- 128
Katika kipindi cha miaka mitatu, sekta ya afya nchini Tanzania imepambwa na mabadiliko makubwa yanayoakisi dhamira thabiti ya Rais Samia Suluhu Hassan kuboresha maisha ya wananchi.
Hii ni safari ya matumaini, ambapo idadi ya vituo vya afya imeongezeka kutoka 8,549 mwaka 2021 hadi 9,693 mwaka 2024, sawa na ongezeko la vituo 1,144.
Aidha Vituo vya huduma za dharura za uzazi (CEmONC) vimeongezeka kutoka 388 mwaka 2021 hadi 523 mwaka 2024.
Maendeleo haya yanaonekana katika upatikanaji wa hospitali na vituo vya afya vipya 570 vilivyoongezwa nchini.
Sasa huduma za afya ziko karibu zaidi na wananchi, hasa katika vijiji vilivyokuwa vikikumbwa na changamoto za miundombinu duni.
Picha halisi inayojitokeza ni ya miundombinu imara, majengo mapya, na huduma bora za matibabu ambazo zimesogezwa karibu na kila Mtanzania, ikiondoa vikwazo vya awali na kutengeneza nafasi za upatikanaji wa huduma za afya bila tabu.
Kuongezeka kwa vifaa tiba vya kisasa vya uchunguzi, kama vile MRI kutoka 7 hadi 13, CT-Scan kutoka 12 hadi 45, Digital X-Ray kutoka 147 hadi 346, Ultrasound kutoka 476 hadi 668, Echocardiogram kutoka 95 hadi 102, Cathlab kutoka 1 hadi 4, na Pet Scan 1, ambayo awali haikuwepo nchini, ni ushahidi wa hatua kubwa zilizopigwa katika sekta ya afya.
Maendeleo haya yanaangaza kama nyota angavu usiku wa giza, yakileta matumaini mapya kwa wananchi.
Tangu Rais Samia alipochukua usukani Machi 19, 2021, ameongeza vitanda vya hospitali kutoka 86,131 mwaka 2021 hadi 145,374 mwaka 2024.
Pia amesaidia katika uwekezaji mkubwa wa ununuzi wa dawa, ambapo upatikanaji umeongezeka kutoka asilimia 58 mwaka 2021 hadi asilimia 79 kufikia Machi 2024.
Tafsiri ya "pesa hazihesabiwi kwa wingi bali kwa thamani" ni kwamba wananchi sasa wanaweza kupata huduma bora zaidi na vifaa vya kisasa hospitalini, tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Zaidi ya hayo, Rais Samia amejenga mazingira bora kwa wahudumu wa afya kwa kuajiri zaidi ya watumishi 15,000 na kutoa mafunzo ya kuongeza ujuzi wao, hatua inayolenga kuimarisha uwiano wa daktari kwa mgonjwa.
Kampeni za kinga na elimu kwa umma, ikiwemo chanjo za magonjwa kama polio, surua, na COVID-19, zimeimarishwa ili kuongeza mwamko wa wananchi kuhusu umuhimu wa afya, na vifo vitokanavyo na UKIMWI vimepungua kutoka 29,000 mwaka 2022 hadi 22,000 Machi 2024, kuashiria juhudi hizi zenye matokeo chanya.
Kwa ujumla, juhudi za Rais Samia zimeleta matokeo chanya katika sekta ya afya, kulinda nguvu kazi ya taifa, na kutekeleza ilani ya CCM.
Ndimi Jackson Jonathan