Heri uchukuliwe na polisi kuliko hao wasiojulikana

Heri uchukuliwe na polisi kuliko hao wasiojulikana

Hivi lini wabongo tutaamka tuyakatae haya au tunasubiri mpaka watumalize wabaki wenyewe, inahuzunisha sana inatia hasira sana
 
lakini pia yule doctor, yule mwandishi wa habari na roma, kipanaya hawa ni baadhi ya watu waliowahi kuchukuliwa na wakaibuka, lakini hawakutuambia hawa wasiojulikana wakoje; wangetusaidia sana kuwaepuka hawa jamaa!!
huwezi sema watasema siku zao za duniani zikibakia chache
 
Wameponea shimo la tewa... Hawawezi kuongea kitu kwa sasa ni kihoro wakikumbuka.. Roma sijui wamemfanya nini keshakuwa teja

Kwamba amekuwa na urahibu wa Madawa ya kulevya ???Mbona kama anaimba tu kawaida? Mh Pole sana Roma.
 
Hicho kikosi cha watu wasio julikana kilikuwepo tangia awamu zilizo pita na wanamafunzo wanayo yapata nje ya nchi, sema awamu zilipo pita walikuwa hawatumiwa lakini sasa hvi wanatumiwa,

Sasa hvi hamna pa kukimbilia ukienda mahakamani hupati haki, ukienda polisi unapotea duh

Kweli kuna umuhimu wa kutembea na kadi ya chama
Afadhali kufa kuliko kubeba ile fedheha ya kijani[emoji15] [emoji15] [emoji15]
 
Nilishawahi kutoa ushuhuda kwenye moja ya nyuzi kuhusu hawa wasiojulikana walivyokamata watu kitaa na wengine kuponea kwenye tundu la sindano chupuchupu

na njugu wamemwagwa sana awamu hii kuweni makini sana kwenye maeneo ya hadhira
 
Hii hali itakoma pale yule chunusi anayekula damu za watu pale magogoni atakapoondolewa
 
Hivi, ni nani ambaye anatoa hayo maagizo ya kuteka watu....??

Sitaki kuamini kama ni Mkulu ndie anaetoa Oda hizo za kukamata kila aenezaye baya kwa serikali...
Anaweza akawa Bashite kweli..!? No..

Hawa viongozi wa utumishi huku chini kwenye ngazi za Mkoa, Wilaya wamepandikizwa SUMU nzito sana...

Tena sumu ambayo wanaona wakiiacha Idle itawarudia wenyewe...

Hii kitu kwamba endapo Mkulu akiiona itakua SOO ndicho ambacho hawa watumishi kwa ngazi zao tofauti tofauti wanafanya...

Sio siri Nidhamu ya uwoga imekua kubwa mno...

Hawa
>Civil Servants ( Regional, District Levels )
>Police

Sijui hawakusoma au ni nini kimewakumba.. kutoa maagizo ambayo yanalenga kuumiza watu...

Halafu huyu Mwakyembe sio huyu ambae tunamjua... Yawezekana kuna mtu after Mkulu, Bashite.... yaani yeye ni integrated.. Ni nani huyo??
 
Mwalimu Christian akiwa Iramba huko Singida akakuta wanafunzi wa shule moja wakiwa wanafanya mtihani uwanjani tena bila madawati... Akiona hii ni habari ya kufaa akapiga picha na kuweka maelezo yake...
Picha ikasambaa Mitandaoni na wahusika wakaiona... Sasa hivi Mwalimu Christian hajulikani alipo na kama yuko hai ama la... Alichukuliwa na wasiojulikana

Tuko kwenye zama ambazo hakuna uhuru wa habari tena.. Na ukosoaji wowote hauvumiliki hata kwa asilimia chache kabisa... Zamani ilikuwa ni ishu kubwa sana kukamatwa na polisi... Siku hizi ni afadhali mara mia ukamatwe na polisi kwakuwa kuna pa kuanzia na at least usalama wako hautakuwa shakani.....
Wengi waliochukuliwa, kutekwa ama kukamatwa na watu wasiojulikana hawakuwahi kuonekana tena na kama walionekana basi aidha watakuwa hoi kwa kipigo mateso na hawajitambui au miili yao wakiwa tayari ni marehemu... Wanakopelekwa hakujulikani, wanachofanywa hakijulikani... Lakini mkifanikiwa kumpata mmoja... Mnajua tu kuwa huyu alikuwa jehanum
Ngoma ikivuma sana hupasuka... Kutekwa kwa mwalimu Christian kunazidi kutoa taswira ya wale wasiojulikana waliokuwa wamejificha kwenye ukuta mnene...
Sasa mabingwa wa kuchora picha habari wanaweza kwa uwazi kabisa kubainisha pasi na shaka ni nani wako nyuma ya utekaji unaoendelea nchini....
1e4e1526b07ae79fae8e3484c213b28c.jpg
Wasiojulikana ndo haohao
 
Haki huinua Taifa. Mwigulu Nchemba usikae kimya yanapotokea matukio kama Haya. Mtu mzima anapoteaje?
 
tatizo mwalimu kajisahau akaanza kuitaja chama cha majitu manene,badala ya kujikita ktk hoja ya msingi.

mahaba ya wanainji na chama lao havihusiani na umasikini walionao.

any way labda yuko millimani kwa maombi maalum,kwaresma hii bana.
 
Back
Top Bottom