Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 375,749
- 870,527
Mwalimu Christian akiwa Iramba huko Singida akakuta wanafunzi wa shule moja wakiwa wanafanya mtihani uwanjani tena bila madawati... Akiona hii ni habari ya kufaa akapiga picha na kuweka maelezo yake...
Picha ikasambaa Mitandaoni na wahusika wakaiona... Sasa hivi Mwalimu Christian hajulikani alipo na kama yuko hai ama la... Alichukuliwa na wasiojulikana
Tuko kwenye zama ambazo hakuna uhuru wa habari tena.. Na ukosoaji wowote hauvumiliki hata kwa asilimia chache kabisa... Zamani ilikuwa ni ishu kubwa sana kukamatwa na polisi... Siku hizi ni afadhali mara mia ukamatwe na polisi kwakuwa kuna pa kuanzia na at least usalama wako hautakuwa shakani.....
Wengi waliochukuliwa, kutekwa ama kukamatwa na watu wasiojulikana hawakuwahi kuonekana tena na kama walionekana basi aidha watakuwa hoi kwa kipigo mateso na hawajitambui au miili yao wakiwa tayari ni marehemu... Wanakopelekwa hakujulikani, wanachofanywa hakijulikani... Lakini mkifanikiwa kumpata mmoja... Mnajua tu kuwa huyu alikuwa jehanum
Ngoma ikivuma sana hupasuka... Kutekwa kwa mwalimu Christian kunazidi kutoa taswira ya wale wasiojulikana waliokuwa wamejificha kwenye ukuta mnene...
Sasa mabingwa wa kuchora picha habari wanaweza kwa uwazi kabisa kubainisha pasi na shaka ni nani wako nyuma ya utekaji unaoendelea nchini....