Heri tukose haki, hewa, na maji lakini tuwe na amani

Heri tukose haki, hewa, na maji lakini tuwe na amani

The Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
10,959
Reaction score
13,426
Wengi wanawalaumu bure watawala wetu kwa kusisitiza amani bila haki.

Wanawalaumu watawala bure kwa kushindwa kutatua matatizo ya kijamii kama vile upatikanaji wa maji.

Wanawalaumu kwa kutunyima haki lakini wakatupa amani huku tukisota na wao wakiishi kwa amani.
Tunababana kwenye misururu barabarani lakini tuna amani.

Heri kuwa na imani ya amani hata bila amani ya kweli lakini kukawa na amani.

Amani kwanza mengine baadaye.

Amani inaweza kuleta kila kitu hata kama ni ndotoni.

Adui wa amani ni mbaya kuliko adui wa haki.

Kukiwa na amani, kuna haki ila kukiwa na haki, amani itapotea.

Kwanini hatuwaelewi watawala wetu ambao sijui kama wanatuelewa?

Kukiwa na amani, mwenye njaa itamuuma kwa amani.

Kukiwa na amani mwenye chakula atakula kwa amani.

Amani ikosekana na haki ikatawala watu watakuwa na kiburi kama cha watawala ambao wana amani wanayosisitiza.

Kwa vile watawala wetu wanatuwakilisha, wakila na kushiba kwa amani, sisi pia tunaishi kwa amani.
Ukidai haki, ujue. Unatishia na kuvuruga amani.

Swali kuu, je, amani yetu ni ya nani na kwa ajili ya nani?
Napiga kelele kimya kimya na kuwaza kwa kutowaza.

Yote tukose ila si amani. Kwani, amani inaliwa, inavaliwa, inawekwa benki, na yote katika yote, amani ni uhai.
 
Individualism ni jambo la msingi sana. Hadi siku tukianza kuitazama amani at individual level ndio mtajua Tanzania sio nchi ya amani.

Tafsiri yetu ya amani it's in a collective way kwamba the atmosphere iko shwari ndio amani which is not.

Tukiwa individualistic lazima tutaanza kujali mimi binafsi najisikiaje? Hakuna maji, miudnombinu mibovu, usafiri shida, umasikini umekithiri najisikiaje mimi kama mimi. If we start thinking like this trust me hata hawa machawa hawatoiona hiyo amani.

Mapepari (US/Europe) wanatuzidi hapa.
 
Chawa wanalipwa kwahiyo wana maisha mazuri
 
Cosmas CHIDUMULE anakwambia ile wizara ya Vijana ijazwe Wazee wa kutosha yaan ni Wizara ya Vijana halafu ijazwe wazee? Ianzishwe wizara ya Wazee huko wawajaze wazee
 
Hiyo hiyo ya mawenge ya watawala wetu watulao kila uchao kwa kuteuana na kupendeleana. Kwa ufupi, ni amani yao na siyo yetu.
Kuna Zee linakwambia likiambiwa lichague kati ya Uhuru na Utumwa linachagua Utumwa.. halafu zee nilikua naliheshimu sana linaturudisha miaka 200 nyuma
 
Kuna Zee linakwambia likiambiwa lichague kati ya Uhuru na Utumwa linachagua Utumwa.. halafu zee nilikua naliheshimu sana linaturudisha miaka 200 nyuma
Hilo, kwa Kiswahili cha mjini, huitwa mtu mzima hovyo
 
Hivyo ulivyotaja ukivikosa,huwezi kuwa na amani.Mwenzetu kwako amani ni nini ?
 
Back
Top Bottom