Herdroth - Sehemu 1

Herdroth - Sehemu 1

HERDROTH

SEHEMU YA 08

Miaka 1000 iliyopita kulikuwa na mfalme aitwaye Kal alitawala falme zote kumi na mbili kabla hakujatokea matengano na kila falme kuanza kujitegemea.

Utawala wa mfalme Kal ulikuwa ni utawala wenye nguvu, heshima na weledi wa hali ya juu kutokana na akili za kipekee alizokuwa nazo Kal, Kal alikuwa ni Teez. Pia katika utawala wake alikuwa anamiliki dragons saba na pia alikuwa ni mchawi wa hali ya juu wa dini ya kizamani na alikuwa mungu wa dragon, uchawi ulikuwa unaruhusiwa, watu waliishi kwa raha mustarehe isipokuwa watu walikuwa wanamhofu kwa uwezo wake wa kumiliki dragons. Pia hao dragons walikuwa wamefundishwa uchawi wa hali ya juu, kama Herdroth alivyo fanya kwa hawa dragons wake wawili wa nyakati hizi

Mfalme Kal ndiye aliyeziunganisha falme hizi 12 na kuzitawala, aliweka viongozi katika kila falme, wawe chini yake na ndiye aliyedumisha umoja wa falme hizi kwa kipindi chote alichotawala na aliheshimika sana.

Miaka hiyo hiyo katika jimbo la Tardosen la mfalme Kal, kulikuwa na kijana mmoja mwanaharakati aitwaye Trosphontere, kijana huyu alijaribu kushawishi watu wajitenge na utawala wa Kal, akidai kwamba Kal anawatawala kimabavu na matisho na kwa uchawi. Kijana huyu kwa jitihada zake za muda mrefu, alifanikiwa kupata wafuasi mia nne walioungana naye kwa lengo la kumng'oa Kal kwenye utawala.

Kutokana na mfalme Kal kuwa na uwezo wa hali ya juu, Trosphontere alitumia mbinu ya kutaka kumwua mfalme peke yake kwa sababu alifahamu fika kwamba kwa vita asingemweza.

Hivyo Trosphontere akajichagulia watu 14 watakao kuwa naye mstari wa mbele katika mchakato mzima wa kumwangamiza mfalme Kal. Waliingia kwa siri usiku na kuwapulizia dawa ya usingizi walinzi waliolinda kuelekea kwa mfalme hatimaye wakafanikiwa kuingia ndani mfalme Kal akiwa amelala na Trosphontere akamchoma kisu kifuani na kufanikiwa kuuondoa uhai wa mfalme Kal.

Usiku huo huo, wakati Trosphontere na wenzake wakikimbia baada ya kufanya tukio la mauaji ya mfalme, dragons walikuwa wamekwisha kutambua ya kuwa mtu wao kwa vyovyote vile atakuwa ameuawa, hawakuhisi muunaganiko wowote kati yao na Kal. Hazikupita dakika nyingi dragons wakawa wamewasili na kufanya mashambulizi ya nguvu, like kundi la watu mia nne wengi wao waliteketezwa kwa moto usiku huo huo na dragons, na bado hatimaye waliendelea kufanya mashambulizi jumla waliangamiza watu elfu moja na mia tano ndani ya siku moja, kwa kipindi hicho watu elfu moja na mia tano ni idadi kubwa mno.

Trosphontere hatimaye alichukuwa ufalme na kutawala falme zote kumi na mbili, hakuruhusu uchawi na alianzisha utaratibu wa kuwaua waliotumia uchawi, hii yote alifanya ili kujikinga asilipizwe kisasi.

Utawala wa Trosphontere ulikuwa wa mabavu mno na alipenda kujilimbikizia utajiri, na kutokana na jimbo la Tardosen kuwa ndiyo jimbo lililoendelea kwa miaka ile, Trosphontere alilichagua kuwa makao yake makuu, na huyuhuyu Trosphontere ndiye aliyekuwa mwanzilishi wa ukoo wa Trosphontere, kwa sababu alijizolea sifa stahiki za kuwa kama mwanzilishi wa ukoo.

Dragons hawakuacha kuwa tishio kipindi chote cha utawala wa mfalme Trosphontere Denassia, na kipindi cha utawala wa mwanaye Rudiger Trosphonere, na kipindi chote cha utawala wa mjukuu wake Castor Trosphontere, hadi kilipofika kipindi cha kitukuu wake, mfalme Sidha Trosphontere ambaye mtawala huyu alifanikiwa kuwaangamiza dragons wote saba waliokuwa tishio na akajizolea umaarufu mwingi usio na kifani na utawala wake ulikuwa na nguvu, mithili ya chuma, hakutikisika, ila baada ya yeye kufariki ndipo majimbo yakaanza harakati za kujitafutia uhuru wao ili kuwa falme zinazojitegemea.

Majimbo hayo kumi na mbili, ambayo kwa sasa ni falme zinazojitegemea ni kama ifuatavyo:
Falme ya Tardosen, falme ya Drusulito, falme ya Rodrino, falme ya Green Land, falme ya Trethe, falme ya Brondon, falme ya Kinthor, falme ya Quasta, falme ya Pengelino, falme ya Costiniapho, falme ya Sixphe, na falme ya Ostinazo.

Baada ya mfalme Kal, kwa kipindi chote cha miaka 1000 katika utawala wa wafalme toka katika ukoo wa Trosphontere mpaka sasa ni wafalme 19, mfalme Strodgan Trosphontere wa Tardosen akiwa ni mfalme wa 19.

Majina ya wafalme hao 19 ni kama ifuatavyo;
Trosphontere Denassia, huyu alitawala falme 12.
Rudiger Trosphontere, huyu alitawala falme 12.
Castor Trosphontere, huyu alitawala falme 12.
Sidha Trosphontere, huyu alitawala falme 12.

Baada ya Sidha falme zingine zikaanza kupata uhuru wao kama ifuatavyo:
Rinetha Trosphontere, huyu alitawala falme 10 isipokuwa Rodrino na Pengelino.
Mandizu Trosphontere, huyu alitawala falme 8, Trethe na Brondon walijitoa na kupata uhuru wao katika utawala wake.

Damintha Trosphontere, huyu alitawala falme 5, Green Land, Drusulito na Quasta walijitoa.
Kamishiz Trosphontere, huyu alitawala falme 4, Kinthor ilijitoa.
Tamidunn Trosphontere, huyu alitawala Tardosen pekee, Costiniapho, Sixphe, na Ostinazo walijitoa.

Wafalme waliofuata baada ya Tamidunn waliendelea kuitawala Tardosen, kama ifuatavyo:
Emmir Trosphontere, Padropin Trosphontere, Shekky Trosphontere, Minna Trosphontere, Hellepha Trosphontere, Stephiza Trosphontere, Komayya Trosphontere, Linotho Trosphontere, Strodigee Trosphontere na Strodgan Trosphontere.

Katika utawala wa nne, wa mfalme Sidha Trosphontere, kipindi hichi ndipo alipozaliwa binti aitwaye Elibetha, binti huyu ni Teez, binti huyu alipewa dhamana ya kutunza mayai ya dragons mawili yaliyosalia. Huyu Elibetha ndiye yule bibi ambaye tulimsoma Episode ya 4 ambaye hakufa hadi alipomkabidhi Herdroth mayai. Ndiyo hawa dragons tulio nao sasa, yaani Drementa na Krozdunn waliowashangaza watu walivyojitokeza na kumwokoa Janvrey alipotaka kuuawa na kuondoka naye.

Elibetha alipoona hafi na waliokuwa marafiki zake wote wameisha aliamua kwenda kuyahifadhi mayai Crystal Land, chumbuko la uchawi na aliyahifadhi kwa spell maalum.
"Dosh puth das puth da dragala eggzronth kal es das pool". Kisha naye alibaki huko huko Crystal Land akimsubiri yule ajaye ili afe, nafsi yake ikapumzike kwa amani.

ITAENDELEA.
 
Back
Top Bottom