plan z
JF-Expert Member
- Jun 10, 2019
- 1,395
- 1,439
FB Group: STORIES
SEHEMU YA 01.
Katika falme ya Tardosen alikuja mtu kutoka falme ya mbali sana akiwa na farasi mweusi. Knights of Tardosen wakiwa juu ya minara ya ulinzi katika falme hiyo ya Tardosen walimwona mtu huyo akiwa anakuja kwa kasi akiwa amempanda farasi wake mweusi akiwa na ngao na upanga wake mkononi.(Knight ni majina waliyoitwa walinzi au mashujaa wa nyakati za kifalme, walikuwa hodari wa kupigana wakiwa wamepanda farasi)
Tardosen ilijengwa ndani ya jengo moja kubwa sana la kifalme, watu wote wa falme hiyo walienea ndani ya jengo hilo kubwa sana. Tardosen ilikuwa ni ghorofa kubwa sana yenye pande tatu, upande wa juu ndipo alipokaa mfalme na wakuu wake na watu wenye vyeo katika ufalme. Upande wa kati wa jengo hilo walikaa watu wa kati, na wafanyabiashara na matajiri, watu wa upande wa kati walikuwa ni watu wenye uwezo kiuchumi lakini hawakuwa viongozi. Upande wa chini ndipo walikaa masikini na watu wasiojiweza na tegemezi.
Tardosen ilikuwa ni falme tajiri na yenye kuheshimika kuliko falme zingine zote kwani ilikuwa na nguvu na mamlaka kubwa kutokana na nguvu ya kiuchumi na nguvu ya jeshi iliyokuwa katika falme hiyo ya Tardosen.
Mfalme "Strodgan Trosphontere" wa Tardosen alikuwa ni mfalme mwenye dharau kwa watu wake hata falme zingine alizidharau, na aliwabagua maskini na kuwaona hawana thamani.
Knights of Tardosen baada ya kumwona mtu huyo akielekea kulikabili lango ya mbele la kuingilia Tardosen walijipanga kupigana naye ili kumzulia. Mtu huyo alifanikiwa kuwaua wale walinzi na kuwashinda mpaka kuingia ndani kabisa hadi ilipokuwa ikulu ya mfalme.
"Wewe ni nani?", mfalme alimuuliza.
"Knight of Rodrino", alimjibu mfalme kisha akaitupa arm yake ya kivita akimaanisha anaomba mpambano. Mara moja knight mmojawapo wa Tardosen aliiokota arm hiyo akiashiria amekubali mpambano na mtu huyo.
"Lini?",mfalme alimuuliza mtu huyo.
"Kesho mchana", alijibiwa.
Rodrino ni falme ya mbali sana kutokea Tardosen. Miaka zaidi ya ishirini iliyopita, mfalme Strodgan Trosphontere aliishambulia falme hiyo ya Rodrino na kuangamiza jeshi lote katika falme hiyo na kujizolea utajiri mwingi wa falme hiyo. Watu waliosalia walikuwa wachache sana wale dhaifu.
"Mercuset" alikuwa mwana mama wa Rodrino mchawi. Wakati Tardosen ilipoivamia Rodrino alipoteza familia yake, waliuawa wakati wa vita akabaki yeye peke yake hali ya upweke huku akiwa na msiba wa wanawe pamoja na mumewe.
Mwana mama huyu alikuwa akitumia uchawi wa dini ya kizamani. Mercuset alikwenda katika makaburi ya mashujaa wa kizamani yaani Knights of Rodrino akamwamsha shujaa mmojawapo kwa maneno ya kichawi kwa lengo la kulipiza kisasi.
Wakati wa usiku watu wa Tardosen walishangaa kumwona Knight of Rodrino akiwa kwenye uwanja wa vita akusubiri mpambano wa kesho. Amesimama tu amechomeka mkuki wake chini akiwa amevalia koti jeusi refu mpaka miguuni. Hakai, halali, wala hali. Watu walimwogopa sana.
Wakati wa mpambano ulifika knight of Rodrino alimshinda knight of Tardosen na kutupa tena arm yake ya kivita kuomba mpambano mwingine. Alibaki pale pale uwanjani akisimama vile vile kusubiri mpaka kesho mchana. Hali, hakai wala halali. Na aliwashinda wote aliopambana nao. Lengo lake lilikuwa ni mpaka amuue mfalme Strodgan Trosphontere.
Safari hii mtoto wa mfalme ambaye ndiye mtarajiwa atakirithi kiti cha ufalme wa Tardosen aliamua kuiokota arm ile ya kivita kuashiria kukubali mpambano na mtu yule.
"Mimi Strodgento Trosphontere, nitapambana na wewe kesho", alisema maneno hayo huku akiokota arm ile. Mfalme alishtushwa sana na kitendo cha mwanaye kuchukua uamuzi ule. Ikumbukwe kwamba mpambano ni hadi kifo, kwani knight of Rodrino aliwaua wote aliokwisha kupambana nao. Ndiyo sheria za mpambano zilivyokuwa. Sasa wasiwasi ulikuwepo mtoto wa mfalme anakwenda kuuliwa na ni nani sasa atakuwa mfalme hapo baadaye.
Katika falme ya Tardosen kulikuwa na tabibu aitwaye Jaiden, alikuwa akitibu watu wote wa Tardosen na kutoa ufumbuzi wa matatizo mbalimbali yanayoikubwa Tardosen na amedumu kwa kipindi kirefu hivyo ni mtu wa makamo. Jaiden ni mtu wa busara sana.
Jaiden anaishi kwenye maabara yake pamoja na kijana aliyezaliwa na kipaji alichorithi kutokana na mama yake kuwa na asili hiyo. Yaani mama yake ametokana na "Teez".(Teez ni aina flani ya watu wenye uchawi wa asili. Kijana huyo anaitwa "Herdoth".
Usiku huo mfalme Strodgan Trosphontere alimwita Jaiden na kumuuliza kama ana lolote la kusema.
"Hii ni elimu ya dini ya zamani ya kichawi, huyu knight of Rodrino ni shujaa wa zamani ameamshwa kichawi naona anakuja kulipa kisasi", Jaiden alikuwa akitoa maelezo kwa mfalme.
"Ni kweli nilimuua, umepata wapi hizi taarifa?", mfalme aliuliza.
"Nimezipata maktaba", alijibiwa.
Tardosen kulikuwa na maktaba kubwa sana tangu enzi na enzi, tangu ufalme na ufalme. Kila tukio lililotukia lilikuwa likiandikwa na kuhifadhiwa katika maktaba hiyo pamoja na picha mbalimbali zilichorwa ndani ya vitabu hivyo.
Knight of Rodrino alikuwa na mkuki wenye pembe tatu zilizochongoka huku upande wa katikati wa mkuki huo ulikuwa mrefu zaidi.
Jaiden na Herdoth walipouona mkuki huo walienda maktaba na kugundua kuwa knight of Rodrino aliamshwa kichawi kwa lengo la kulipiza kisasi. Wakampa taarifa mfalme Strodgan Trosphontere.
Mfalme alimwita Jaiden peke yake na kumweleza kwamba kesho yeye ndiye atakayepigana ili kumnusuru mwanawe, Tardosen isije ikakosa mfalme hapo baadaye. Hivyo alimwambia ampe dawa ya usingizi mwanaye itakayomfanya alale kupitiliza mpaka pambano litakapoisha, ili mwanaye asife kwa ajili ya jambo alilolitenda mfalme. Kwani Strodgento Trosphontere, mtoto wa mfalme alikuwa mtu asiyekubali kushindwa. Hivyo waliamua watumie njia hiyo mwanaye asiende kupigana akauawa.
"Chukua hii dawa unywe, itakuondolea uchovu katika mwili wako", Jaiden alimpa dawa ile Strodgento.
Wakati wa pambano, mfalme alivaa mavazi ya kivita kupambana na knight of Rodrino huku watu wote wakiwa wanatizama. Jaiden na Herdoth pia walikuwemo. Mpambano ulikuwa mkali mfalme alimtoboa knight of Rodrino tumboni na upanga, lakini knight huyo hafi, hana tofauti na mizimu.
Mpambano uliendelea hatimaye mfalme aliangushwa chini. Knight of Rodrino akaunyanyua upanga wake akijiandaa kumuua kabisa Strodgan.
Hedroth alipoona hayo akabadilika macho yakawa ya dhahabu akatamka matamshi ya kichawi ya kuharibu nguvu ya uchawi aliyokuwa nayo Rodrino na kumwangamiza kabisa.
"Waan-ros dran patro swan hurto", Hedroth alitamka ndipo knight huyo akalipuka kama bomu akateketea pale pale ikawa ushindi kwa Strodgan Trosphontere.
ITAENDELEA.
Sent using Jamii Forums mobile app