Henry Magumo wa ITV huko Zanzibar

NyaniMzee

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
396
727
Nasikiliza radio one yanayojiri Zanzibar namsikiliza huyu mtangazaji anavyojiumauma. ITV fanyeni substitution haraka anaharibu taaluma za waandishi. Huenda ana tatizo fulani yaani anatetemeka tu.
 
Unaweza kuwa unamlaumu bure anaripoti huku pembeni kuna vifaru na defender za FFU unadhani atakuwa na amani.

Waandishi huwa ndio wapiga kelele kuomba wawe wanapewa ulinzi wa kutosha wanapofanya kazi zao! vifaru kama vipo, vipo kwa kuitikia kilio cha waandishi wa habari cha kupewa ulinzi wa kutosha.Hayo ya kuripoti hayawahusu madereva wa vifaru..Kazi ya dereva wa kifaru kuendesha kifaru na mtangazaji kutangaza.Hamna mgongano hapo.
 
Kumlaumu mtangazaji huyo ni kumuonea tu!Kama unashuka leo Mji Mkongwe haina tofauti yyt na Ukanda wa Gaza tena enzi za utawala wa PM Yitzhak Rabin

Mtu yeyote ukiona anaogopa askari wakiwa wametanda ni jambazi-by Suleiman kova aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam
 
Katika mji wa Chakechake, Pemba mitaa yote imejaa vifaru na wanajeshi, hakuna raia anayethubutu kutoka nje. Yaani ni kama ilivyokuwa Baghdad enzi za mapigano ya Marehemu Saadam Hussein na Wamarekani.
 
Mtu yeyote ukiona anaogopa askari wakiwa wametanda ni jambazi-by Suleiman kova aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam
Kwa hiyo Zanzibar kutakuwa na majambazi wengi sana ndiyo maana polisi wamejazwa huko na majambazi yameshindwa kutoka ndani kabisa
 
Waandishi huwa ndio wapiga kelele kuomba wawe wanapewa ulinzi wa kutosha wanapofanya kazi zao! vifaru kama vipo, vipo kwa kuitikia kilio cha waandishi wa habari cha kupewa ulinzi wa kutosha.Hayo ya kuripoti hayawahusu madereva wa vifaru..Kazi ya dereva wa kifaru kuendesha kifaru na mtangazaji kutangaza.Hamna mgongano hapo.
Ulinzi uliopo sasa ni kuhakikisha mapenzi yanatimizwa na si ukweli unaripotiwa
 
Mtu yeyote ukiona anaogopa askari wakiwa wametanda ni jambazi-by Suleiman kova aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam
Mhmm mkuu wa mkoa?! acha kupotosha hakunaga mkuu wa mkoa aliyewahi kuteuliwa kwa jina hilo nadhani hizo ofisi za lumumba wamewadanganya. Anyway lumumba ndio eneo la kupika majungu na fitina.
 
Achana naye anaandika kama kakalia kitu butu
 
Unaweza kuwa unamlaumu bure anaripoti huku pembeni kuna vifaru na defender za FFU unadhani atakuwa na amani.
Kwa sasa uhuru wa habari haupo, kila kitu kinaminywa ili kufanikisha jambo la watu wachache wenye maslahi binafsi wasiopenda maendeleo ..."tuombe sana Mungu huu ya amani ya taifa"
 
Back
Top Bottom