Hembu Mnukuu GodBless Lema Hapa!

Hembu Mnukuu GodBless Lema Hapa!

Fungeni milango tupigane.

mkuu hv mzigo huwa unapiga saa ngapi? Au hapa jf ndio kibaruan kwako nn?
Nimeulza kwa nia njema tu mkuu usinimaindi ukizingatia mie ni ccm mwezako
 
lema hana akili timamu

ndugu amani kwa wote..pole sana kwa watu wengine kutokukuelewa ulichokisema hapo juu...

Ni kweli kabisaaaa...maneno aliyoyasema lema sio ya mtu mwenye akili timamu...

Hasa ukilinganisha na sie tulio wengi tumehitimu elimu isiyokuwa na waalimu wala vitabu...

Lema hana akili timamu kwa sababu hazijatimia katika kiwango cha wanadamu wengi wa kawaida kama sisi...lema anazo akili zilizozidi kipimo kama alizokuwa nazo nyerere, che guevara, patrice lumumba kwame nkrumah, malcolm x and the likes...kina plato, kina newton isack, kina albert einsten...

huu ni mfano wa watu wachache ambao dunia tunayoishi ilipata kuwashuhudia na kuwaita hawana akili timamu...ila sio kwa mapunguvu bali kwa kuzidi upeo wa kufikiri ikilinganishwa na watu walio wengi duniani.

lema hana akili timamu coz he is a genius
 
“Mimi ni bora nikapigwe risasi lakini mchungaji akija kusoma risala aseme marehemu amekufa akipigania haki, kifo kwangu kimeshapoteza kumbukumbu na uoga kwangu umeshapoteza kumbukumbu, siogopi kufa siogopi jela ila naogopa kwenda jela kwa wizi wa kompyuta, Tv au kubaka mwanamke lakini siogopi kwenda jela kwa kupigania haki za watu, wanaoleta vitisho ninawakaribisha.. ni vingi na vingine tunavifanyia utafiti sisi wenyewe tujue chanzo ni nini, hata muundo wa serikali ulivyo dhidi ya wapinzani ni kitisho namba moja, kwamba wewe ni mbunge wa Chadema na unafanya kazi na DC ama na mkuu wa mkoa ambae ni mjumbe wa kamati ya siasa ya CCM wilaya.

”Kauli nyingine aliyoitoa Lema ni kuhusu kesi yake kwa sasa kwa kusema “sitaki mahakama ya rufaa inipendelee sitaki hata kidogo, ikinipendelea nitalia, nitaogopa nitasikitika nikijua nilifanya makosa ya kuua alafu nikaachiwa huru, niko tayari kurudi kwenye uchaguzi na nitashinda kuliko mbunge yeyote Afrika Mashariki kwa kura za kubeba na Canter ila ninachotaka ni haki itendeke, ila nimepata faraja kwamba anaeiongoza kesi yangu ni jaji mkuu wa Tanzania nikiamini atapitia vipengele vya kisheria vizuri kabisa”

Pamoja na hayo yote, Godbless Lema amesema hajawahi kujuta kuwa nje ya bunge ila anajuta kwa nini Mahakama iliingiliwa na kumfanya ajue matokeo ya kesi siku 14 kabla ambapo namkariri akisema “Halima Mdee alinipa matokeo ya kesi mpaka kifungu kinachokwenda kunibana, Dr Slaa anaingia mahakamani ananiamba mwanangu unakwenda mahakamani lakini hukumu yako itakua hivi, ile kesi hukumu ilivuja kwa hiyo maana yake ilikua ni mpango, ni kitu kimepangwa”

“Kilichoniumiza sio mimi kutokua mbunge, ninaweza kuishi nje ya Ubunge ninaweza kuuza mitumba, ninaweza kuwa dereva wa daladala, ninaweza kucheza soka.. ubunge kwangu sio ajira naweza kuishi maisha mazuri kuliko kuwa mbunge, nimekua mfanyabiashara siku za nyuma sijakwenda Ulaya nikiwa mbunge, nimekwenda ulaya kabla sijawa mbunge nimekwenda karibu nchi 16 na nimefanya biashara lakini nilipopata ubunge nikasema nimepata nafasi ya kutumikia watu”

Souce:
By Millard Ayo with GodBless Lema kwenye exclusive interview!

Amma kweli, wajinga ndio waliwao!

Huyu Lema hajui hiyo Serikali iliyopo madarakani ndiyo iliyoanzisha muundo wa vyama vingi? Huyu Lema hajui hiyo Serikali iliyopo madarakani ndiyo inayotoa ruzuku kwa vyama vya upinzani?

Muundo mzuri kwake yeye ndiyo upi?

Viwanda vingine hutoa bidhaa mbovu.
 
"ktk watu ambao hawaitaki mema tz we ni namba moja,kabla ya kuweka ujumbe wako jaribu kuchunguza akili na fikra zako kuwa zipo timamu,usikurupuke"
 
Ccm wamempa likizo tu lem. Yeye ni mbunge wa arusha daima dumu.
 
i rather die like a man than live like a coward.......inaskitisha sana hali ya siasa humu nchin mahakama zimeingiliwa hazina meno hata mapengo hazina....
 
lema nashindwa kusema..neno gani kukusifia..but keep it up..ipo siku wataelewa tu...waziba haki..pamoja na wanaoshabikia
 
Huyu chizi kwanza tapeli ars Ina Watu wengi na akili zao jamii forum
 
zomba said:
Amma kweli, wajinga ndio waliwao! Huyu Lema hajui hiyo Serikali iliyopo madarakani ndiyo iliyoanzisha muundo wa vyama vingi? Huyu Lema hajui hiyo Serikali iliyopo madarakani ndiyo inayotoa ruzuku kwa vyama vya upinzani? Muundo mzuri kwake yeye ndiyo upi? Viwanda vingine hutoa bidhaa mbovu....| | Nyani haoni Kundule,huona la mwenziwe...Aliyekwambia vyama vingi vilianzishwa na Magamba ni nani? Kwa multipartism ilianzia Tanzania? Ama kweli,kichwa cha kuku hakibebi mzigo...nenda ukasome source of multipartism and forces behind its implementation! Kama ccm ndiyo chanzo cha vyama vingi,mngekuwa mnatumia nguvu kubwa na propaganda za kila aina kuhujumu upinzani ili muendelee kutawala kwa uroho wenu wa madaraka? Eti,serikali anayoilaumu Lema ndo inayotoa ruzuku,hivi hizo hela zinatoka kwenye mifuko ya Nape,Mukama,Jakaya au ni fedha za kodi za watanzania wote toka vyama vyote,zingine zinatokana na uuzaji wa rasilimali zetu .Kuna haki gani,DC au RC kuwa mjumbe wa kamati ya siasa ya ccm?
 
Back
Top Bottom