Hembu Mnukuu GodBless Lema Hapa!

Hembu Mnukuu GodBless Lema Hapa!

Watanzania wanapiga kura kama vipofu, halafu wanalalama kama vichaa! (Generali Ulimwengu 2011)
 
Hawa ndo viongozi tunaowataka, viongozi wanaojua nini maana ya watanzani nini maana ya watu wa chini nini maana ya uzalendo na nini maana ya kutumikia watu. si propaganda ambazo hazisaidii watu. Tuombe Mungu tupate wabunge kama Lema nchi itasonga mbele. Hata wakufanyie hila miaka miwili tuu imebakia lazima urudi mjengoni. Wanaairisha mazishi ila lazima marehemu atazikwa tu.
 
Huyu chizi kwanza tapeli ars Ina Watu wengi na akili zao jamii forum

..........kuna kiumbe mmoja wa huko huko kwenu akiitwa A.L.Mrema, hivi Lema anaweza kupita umaarufu wake ? naye atapita tuu !
 
Amma kweli, wajinga ndio waliwao!

Huyu Lema hajui hiyo Serikali iliyopo madarakani ndiyo iliyoanzisha muundo wa vyama vingi? Huyu Lema hajui hiyo Serikali iliyopo madarakani ndiyo inayotoa ruzuku kwa vyama vya upinzani?

Muundo mzuri kwake yeye ndiyo upi?

Viwanda vingine hutoa bidhaa mbovu.
Hiki nacho ni kituko!! Serikali iliyoko madarakani ndiyo iliyoanzisha muundo wa vyama vingi? Demokrasia ya vyama vingi katika nchi nyingi duniani imeanzishwa na serikali zilizoko madarakani? - Utumbo!!!
 
“Mimi ni bora nikapigwe risasi lakini mchungaji akija kusoma risala aseme marehemu amekufa akipigania haki, kifo kwangu kimeshapoteza kumbukumbu na uoga kwangu umeshapoteza kumbukumbu, siogopi kufa siogopi jela ila naogopa kwenda jela kwa wizi wa kompyuta, Tv au kubaka mwanamke lakini siogopi kwenda jela kwa kupigania haki za watu, wanaoleta vitisho ninawakaribisha.. ni vingi na vingine tunavifanyia utafiti sisi wenyewe tujue chanzo ni nini, hata muundo wa serikali ulivyo dhidi ya wapinzani ni kitisho namba moja, kwamba wewe ni mbunge wa Chadema na unafanya kazi na DC ama na mkuu wa mkoa ambae ni mjumbe wa kamati ya siasa ya CCM wilaya.

”Kauli nyingine aliyoitoa Lema ni kuhusu kesi yake kwa sasa kwa kusema “sitaki mahakama ya rufaa inipendelee sitaki hata kidogo, ikinipendelea nitalia, nitaogopa nitasikitika nikijua nilifanya makosa ya kuua alafu nikaachiwa huru, niko tayari kurudi kwenye uchaguzi na nitashinda kuliko mbunge yeyote Afrika Mashariki kwa kura za kubeba na Canter ila ninachotaka ni haki itendeke, ila nimepata faraja kwamba anaeiongoza kesi yangu ni jaji mkuu wa Tanzania nikiamini atapitia vipengele vya kisheria vizuri kabisa”

Pamoja na hayo yote, Godbless Lema amesema hajawahi kujuta kuwa nje ya bunge ila anajuta kwa nini Mahakama iliingiliwa na kumfanya ajue matokeo ya kesi siku 14 kabla ambapo namkariri akisema “Halima Mdee alinipa matokeo ya kesi mpaka kifungu kinachokwenda kunibana, Dr Slaa anaingia mahakamani ananiamba mwanangu unakwenda mahakamani lakini hukumu yako itakua hivi, ile kesi hukumu ilivuja kwa hiyo maana yake ilikua ni mpango, ni kitu kimepangwa”

“Kilichoniumiza sio mimi kutokua mbunge, ninaweza kuishi nje ya Ubunge ninaweza kuuza mitumba, ninaweza kuwa dereva wa daladala, ninaweza kucheza soka.. ubunge kwangu sio ajira naweza kuishi maisha mazuri kuliko kuwa mbunge, nimekua mfanyabiashara siku za nyuma sijakwenda Ulaya nikiwa mbunge, nimekwenda ulaya kabla sijawa mbunge nimekwenda karibu nchi 16 na nimefanya biashara lakini nilipopata ubunge nikasema nimepata nafasi ya kutumikia watu”

Souce:
By Millard Ayo with GodBless Lema kwenye exclusive interview!

Hapo kwa red,
hivi huyu dogo anajua anacho kisema? anajua maana ya kifo kweli? Yesu pamaja na kuwa na uhakika na safari yake baada ya kifo anaenda kwa Mungu, hakuwahi tamka maneno hayo hata siku moja! dogo, hamna shujaa katika kifo! nafikiri angeenda hospital aone jinsi watu wanao kata roho wakati bado wanapenda kuishi asinge sema hayo yote.
kwa matamshi yake hayo, kama hadhamini uhai wake mwenyewe ni vipi adai kuwapigania wengine? yaani yupo kama wale wafuasi wa Alqaeda ambao maisha kwao hayana maana badala ya kujilipua wafie mbali wenyewe wanalipua watu wengine. in short lema aseme ni kitu gani kina dhamani kwake zaidi ya maisha? well Mungu amemsikia siku akiomba roho yake asilalamike!!.
 
Back
Top Bottom