HELSB yawaburuza kortini 18 kwa kutorejesha mikopo

engineerm

Senior Member
Aug 30, 2011
106
19
Wanafunzi 18 wa vyuo vikuu nchini wameburuzwa mahakamani baada ya kubainika kushindwa kerejesha mkopo uliowawezesha kupata elimu ya juu kutoka Bodi ya Mikopo (HELSB).

Washitakiwa hao walioshitakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam wanadaiwa zaidi ya Sh. milioni 148.

Wanadaiwa fedha hizo ambazo walikopa kati ya mwaka 1994 na 2009 na kukubali kurejesha kwa muda ambao walikubaliana na masharti ya bodi hiyo.

Inadaiwa kwamba kwa mujibu wa kifungu cha 6 C na H cha sheria ya Bodi ya Mikopo namba 9 ya mwaka 2004, inatamka kwamba bodi iliaminiwa kusimamia utaratibu mzima wa kutoa na urejeshaji wa mikopo iliyotolewa na serikali tangu Julai 1994.

“Kwa mujibu wa kifungu namba 19 cha sheria ya bodi na miongozo yake, inatamka kwamba kila aliyefaidika na mkopo baada ya kukamilisha elimu yake atarejesha mkopo wa Serikali kupitia Bodi. Wadaiwa walikumbushwa kurejesha madeni kupitia vyombo vya habari, lakini walikaa kimya, hivyo bodi inaomba waamuliwe kulipa,” ilisema hati ya madai.


Bodi ya Mikopo inaomba kila mdaiwa alipe fedha alizokopa na adhabu asilimi 10 ya mkopo, alipe fidia kama mahakama itakavyoona inafaa na pia walipe gharama za kesi.

Wadaiwa katika kesi hiyo wanatakiwa kulipa jumla ya Sh. 135,132,275 ambazo ni madeni waliyokopa kwa ajili ya kuwawezesha kupata elimu ya juu na Sh. 13,513,227 ni adhabu ya kuchelewesha malipo.

Walioburutwa mahakamani ni Adam Coresh, Ally Mwenda, Anna Lymo, Hasma Tullango, Catherine Mhina, Clement Kihamia, Dorin Lyatuu, Farida Zuku na Felix Mosha. Wengine ni Flora Peter, Frank Daniel, Harieth Mazengo, Happynes Saria, Hollo Ngeme, Mwanahamisi Abood, Ndebemeye Philipo, Ndeni Anande na Turphina Matereke.

CHANZO: NIPASHE
 
Mmmh....nina maswali mengi! Ina maana ni hao 18 tu ndio hawajalipa?
 
....Nasikilizia mwenendo mzima wa kesi utakavyokwenda... kama wanafanya kweli au longolongo maana idadi ya wanaodaiwa ni maelfu....
 
Wanafunzi 18 wa vyuo vikuu nchini wameburuzwa mahakamani baada yakubainika kushindwa kerejesha mkopo uliowawezesha kupata elimu ya juu kutoka Bodi ya Mikopo (HELSB).
engineerm, ni 'wanafunzi' au 'waliokuwa wanafunzi'?
 
Last edited by a moderator:
Wanarudisha pesa hiyo kutokea wapi, jee walishapata ajira baada ya masomo?. Maana mimi nimelipa baada ya mwajiri wangu kuletewa jina toka Bodi na ndio akaanza kunikata kwenye mshahara. Nchi za Ulaya waliopewa mikopo huwa wanatafutiwa kazi na serikali ili warejeshe huo mkopo au huwa wanaambiwa waede kutoa huduma ya kujitolea kwa muda fulani nchi za nje ambazo hizo nchi huilipa serikali ya anayejitolea (voluntire) halafu baadae unaruhusiwa kurudi nchini kwako na kupatiwa kazi. Hata kama sio nchi za nje hata hapa Tanzania wangepewa nafasi hiyo mpaka deni litakapoisha
 
uonevu tu!! mbona wako wengi sana wanaodaiwa tena na wengine hata kazi hawajapata?
 
wameaonea watu hawana kazi watarudishaje huo mkopo halafu 1994 elimu ilikuwa buree vijana fungueni kesi ya madai mtalipwa donge nono kwa usumbufu wa bodi nitafteni niwasimamie hiyo kesi buureee:target:
 
wameaonea watu hawana kazi watarudishaje huo mkopo halafu 1994 elimu ilikuwa buree vijana fungueni kesi ya madai mtalipwa donge nono kwa usumbufu wa bodi nitafteni niwasimamie hiyo kesi buureee:target:
Umesoma wapi kuwa hawana kazi? Elimu ilikuwa bure 1994 iweje hawa wapelekwe mahakamani?Ndugu hivi umesoma kweli taarifa yoyote au umesoma kichwa na kurukia kuchangia?
 
mbona na mimi nina deni miaka kibao! wahajawai kunidai ata siku moja !ila madogo sikuhizi wakiajiriwa makato yanaanza hapohapo!
 
Kama bodi haitaishia kwa hao tu itakuwa jambo jema, naamini kuwa wapo wengi sana tena wenye uwezo wa kulipa lakini hawajalipa. Hatuna budi kujenga utamaduni wa kulipa madeni otherwise kelele za kutaka mabadiliko ya uongozi wa siasa bila sisi wenyewe kubadilisha mindset kuwa mkopo lazima ulipwe ni kupoteza muda.
 
Bodi ya mikopo haina hata record kamili ya majina ya watu waliowahi kukopa na kusomeshwa na kwa hela za bodi. Nina jamaa zangu kibao ambao tulimaliza wote UDSM, na tumeajiriwa pamoja kwenye seckta tofautitofuati, hawakuwahi kudaiwa na bodi hiyo hela ya mkopo. Mimi nililetewa barua kazini kuanza kukatwa deni langu, na nimekatwa hadi nimelimaliza mwaka jana. Cha ajabu majina ya wadaiwa wa bodi ya mikopo yaliyotoka mwaka jana, langu likawemo katika wanaodaiwa, halafu watano kati ya hawa rafiki zangu ambao hawakuwahi kulipa majina yao hayamo kati ya wadaiwa. Inashangaza sana, aliyelipa anaendelea kudaiwa halafu ambaye hakuwahi kulipa hayupo kwenye record zozote.

Yaani utendaji wa vyombo vya serikali nchini ni mbovu haujawahi kuwapo duniani. Wafanyakazi wa bodi ya mikopo wanalipwa mishahara mikubwa na mrupurupu kibao lakini umakini wao ni mdogo mno. Wanashindwa hata kuwa na record kamili ya waliokopa, waliolipa na wanaodaiwa. Sasa utajiuliza katika malaki ya waliokopeshwa, ni hawa 18 tu ambao hawajalipa? Na katika haya majina yaliyotajwa hapa, sijaona hata jina moja la hao jamaa zangu.
 
mbona na mimi nina deni miaka kibao! wahajawai kunidai ata siku moja !ila madogo sikuhizi wakiajiriwa makato yanaanza hapohapo!

Kulipa deni si lazima udaiwe,kuna mtu hakudai deni lake,hakusumbui, lakini tayari unakuwa umejiweka katika kapu fulani la watu...Halafu tunaongoza kupiga kelele kwenye jukwaa la siasa kutaka mabadiliko...man in the mirror.
 
Upumbavu mwingine wa serikali ya magamba, mkiambiwa kuna watu WASENEnyaji mnakataa, bodi yenyewe viongozi wake wanatuhumiwa kwa ufisadi, hivi moyo wa kurudisha madeni unapatikana wapi? Kwanza ni wangap wanadaiwa? Nilisikia wakisema urejeshaji haujali kama aliyefaidi mkopo amepata ajira au la, manake wanategemea watu walipe kwa kuuza masaburi au? Inakasirisha sana!
 
Back
Top Bottom