Help please!

Kuna moment katika maisha no point of return unaweza sema mungu huypo kumbe he's just there watch'n you until the last point that you say its over now, then he showed up huwezi amini na sio kwamba anapenda unavyoteseka No anakupima imani je wakati wa raha utaweza kumkumbuka kama wakati wa shida??
 

namuomba na atengeneze njia kwa wakati huu maana hiki ndo kipindi kigumu zaidi kuwahi kutokea katika maisha yangu,nashukuru mnanitia nguvu na baadhi wanaonyesha nia ya kutaka kunisaidia,mungu aendelee kufungua mioyo yenu ili kupitia nyie niweze kupata majibu ya matatizo yangu
 
  • Ndugu , usirudi nyuma, usichoke kutafuta, wenye nazo hawakuzaliwa nazo, ipo siku utafanikiwa.
  • Tanguliza sala kwa kila ulipangalo na kulifanya.
  • Toa sadaka ya sehemu ya kidogo mungu alichokupatia .
  • Hakika utafanikiwa, na yanayokukabili leo yatabaki kuwa historia. Jipe moyo unaweza.
pia nawaomba ndugu zangu humu jamvini mnipe japo neno tu la kunifanya niendelee kutamani kuishi,sina mtu yoyote wa karibu mda huu wa kunifarij hata usingizi sina!!
 

asante kwa ushauri mzuri mwalimu,nipo karibu na mungu na huwa namuomba kila uchao,wacha niendelee kuwa na subira
 
asante sana pia kwa hili,kuna mengine yanasikitisha,nakaribia kufukuzwa nilipopanga mda wa kulipa kodi umefka sina hata senti,ajira nazo ndo hazipatkani,mungu naomba anibariki anifungulie njia!

Aisee daah, kuna watu mnapitia majaribu hadi huruma, Mungu aepushie mbali.... Pole sana ukiona mambo yamekuelemea tafuta hata washkaji wakupige tafu au urudi home kwanza ujipange upya jamani.
 
Aisee daah, kuna watu mnapitia majaribu hadi huruma, Mungu aepushie mbali.... Pole sana ukiona mambo yamekuelemea tafuta hata washkaji wakupige tafu au urudi home kwanza ujipange upya jamani.

kwetu mkoani,hapa dar natafuta tu maisha,hali tete sana ila nashukuru jaman kwa ushauri wenu mnanitia nguvu,naomba mungu njia yangu ifunguke kupitia kwenu
 
...pole sana ndugu yangu. Ila kumbuka kuwa unapoona una tatizo hadi kufukia hatua kwamba unaona labda limekushinda, hapo ndipo Mwenyezi Mungu anapima imani yako kwake, na ukifaulu hapo tu basi ujue umefanikiwa na tatizo litakwisha huku ikibaki kuwa historia tu. Kumbuka pia kuwa hapo ni kwamba unatengeneza historia ya maisha yako na kwamba siku moja mambo yako yakiwa mazuri utabaki kuwa unakumbuka 'duh, nilipitia wakati mgumu sana kipindi Fulani huko nyuma'....ninakuomba umshukuru Mwenyezi Mungu kwa zawadi ya uhai na afya aliyokujaalia kwani kuna wengi wanakosa hata hali hiyo ambayo wewe unayo.....tupo pamoja nami nitakuweka ktk dua zangu ili mambo yako yawe vile unavyotamani Inshaallah! usikate tamaa kumuomba Mwenyezi Mungu na uhangaike kujikwamua kutoka ktk hali hiyo.
 
kwetu mkoani,hapa dar natafuta tu maisha,hali tete sana ila nashukuru jaman kwa ushauri wenu mnanitia nguvu,naomba mungu njia yangu ifunguke kupitia kwenu

Mungu ni mwema hakika atasikia kilio chako na hitaji la moyo wako.
Usikate tamaa ndugu!
 

asante sana
 
Usikate tamaa kila kitu kinawezekana hasa unapokua na Imani,kuwa mtu wa kujichanganya ila epuka makundi mabaya...Mungu akusaidie
 
Usikate tamaa kila kitu kinawezekana hasa unapokua na Imani,kuwa mtu wa kujichanganya ila epuka makundi mabaya...Mungu akusaidie

najitahd sana kutokufanya matendo mabaya kama wizi,utumiaji madawa,ulevi na vinginevyo nna imani hvyo ndo vitafanya nichukie zaidi maisha,pia najipa moyo kuendelea kuhangaika,ila kwa point niliyofikia ni pagumu sana,ni kama mtu akiwa anaendesha gari,mafuta yakiisha kama pesa huna safari yako inakuwa mashakani!
 

usiogope wewe sio wa kwanza wapo wanaopitia magumu zaidi yako..take it as a challenge na usonge mbele
 
I BELIEVE HARDSHIP PUSHES SOMEONE TO SUCCESS...AS LONG AS YOU ARE PHYSICALLY AND MENTALLY FIT..be positive mindedno matter what...I CAN FEEL WHAT YOU ARE GOING THROUGH....NEVER LATE SUICIDE CROSS YOUR MIND....
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…