BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,015
Helikopta za CCM na Chadema zaleta maafa
Makubo Haruni, Tarime
Daily News; Thursday,October 09, 2008 @20:02
WATU watano wamelazwa baada ya kukatwa mapanga katika ugomvi wa kugombea uwanja wa mpira mjini hapa kwa ajili ya kutua helikopta za kampeni za Chadema na CCM jana.
Vyama hivyo vinatumia helikopta katika hatua za mwisho za kampeni, Chadema ikiwa imeanza kuitumia kuanzia juzi, wakati ya CCM iliwasili kwa mara ya kwanza jana.
Watu waliokatwa mapanga ni Masanda Edward, Athuman Selemani, Mahende Daniel, Genya Sabai na Modesta Mwita ambao wamelazwa katika Zahanati ya Tarime mjini hapa.
Ugomvi huo ulitokea majira ya saa nne asubuhi uwanjani hapo baada ya wafuasi wa Chadema kutinga uwanjani kwa ajili ya kusubiri helikopta yao maarufu kama ya Mbowe, iliyokuwa itue kwa ajili ya kuwachukua viongozi kwenda kufanya kampeni. Habari kutoka uwanjani hapo zilizothibitishwa na Katibu Mwenezi wa CCM wilayani Tarime, Samwel Kiboye,
zilieleza kuwa uwanja huo ulikuwa umeombwa kwenye Tume kwa ajili ya shughuli maalumu kupokea helikopta ya CCM, na kwamba ugomvi ulitokea baina ya pande hizo mbili kutokana na wafuasi wa Chadema kugawa uwanja huo makundi mawili kwa ajili ya kutua helikopta hizo.
Hata hivyo muda mfupi kabla ya kufika kwa helikopta ya Chadema, kulitokea majibizano kati ya wafuasi hao na wanaodaiwa kuwa ni wa CCM, kuchomoa mapanga na kuanza kuwashambulia wenzao na kuwajeruhi.
Kitendo hicho kiliwavuta watu wengi na kufanya helikopta ya Mbowe isitue uwanjani hapo na rubani wake kulazimika kutafuta eneo jingine katika uwanja wa Kanisa la Anglikana ambako ilitua na kumchukua Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na mgombea ubunge, Charles Mwera, kwenda kwenye kampeni. V
iongozi wa Chadema akiwamo Mkurugenzi wa Vijana na Mambo ya Nje, John Mnyika na mgombea udiwani wa chama hicho waliijia juu Polisi kwa kutowakamata watuhumiwa hao, licha ya wao kuwataarifu waliohusika na gari walilokimbizwa nalo.
Wakati hayo yakitokea katika kampeni za kumsaka Mbunge wa Tarime kumrithi Chacha Wangwe, aliyekuwa kada wa CCM aliyehamia Chadema amesema kuwa alifanya hivyo badala ya kusubiri kufukuzwa.
Kada huyo, Chacha Mwikwabe, ambaye aligombea ubunge wakati wa kura za maoni CCM, ameeleza kuwa kitendo cha kumtoa uongozi wa Katibu wa Umoja wa Vijana wa Mkoa na kwenda kuwa karani wa Mwenyekiti wa Taifa wa jumuiya hiyo, kingemfanya kuwa mpika chai.
Amesema ubaguzi aliofanyiwa na kuandamwa kutokana na kukemea mafisadi ndani ya CCM, kulisababisha kuchukiwa na Nchimbi na Yusuf Mkamba, hali iliyomfanya apatwe na wasiwasi na kuamua kutimka kabla ya kutimuliwa.
Ameiponda CCM kwa kile alichokieleza, kuiga Chadema kutumia helikopta katika kampeni huku akiapa kuongoza vijana wa Chadema kudai ushindi iwapo CCM itatangazwa mshindi hata ikibidi kumwaga damu.