Hela zimesharudi mtaani?

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,231
113,598
Moja ya malalamiko ya kipumbavu kabisa yaliyokuwepo enzi za utawala wa Rais Magufuli ni kuwa eti hela hazikuwepo mtaani.

Sijui ni lini hasa Tanzania hii ambapo hela zilikuwepo bwerere mtaani! Kwa sababu, Tanzania ni nchi maskini. Ni nchi ya ulimwengu wa tatu.

Vipato vya wananchi wake ni vya chini sana. Si nchi nyingi ambazo nchi yetu imezipita kwa vipato vya wananchi.

Na tumekuwa nchi ambayo wananchi wake ni wa kipato cha chini tokea tuwe taifa na nina uhakika kabla hata ya kuwa taifa.

Lakini katika utawala uliopita tuliaminishwa mzunguko wa hela umebanwa na hivyo kupelekea kutokea upungufu wake mtaani/ mitaani.

Baada ya kumpata huyu Rais wetu mpya, aliye mpole na msikivu, mwenye kuongea Kiingereza kizuri kabisa 😉, tukaambiwa sasa mzunguko wa hela utarudi na hela zitakuwepo mtaani kama ilivyokuwa kabla ya kuja kwa dikteta Magufuli!

Sasa niaje raia? Mama kesharudisha hayo mahela mitaani?

Kama hayo mahela yamesharudi mitaani kwa nini mnalialia kuhusu vijitozo vya shilingi 100 mtumapo hela kwenye Em Pesa?

Kwa mnaojua hayo mahela yalipo, msiwe wachoyo. Tauambieni na sie wengine tuje tuyaokote bana.

Vilivyo vizuri kuleni na sie ndugu zenu.

Tuendelee kuupiga mwingi 😉.
 
Hata chanjo wameanza wenye connections kwanza, raia wengine tunarubiri zitakazobaki kuanzia kesho.
 
Ukweli ni kuwa, mzunguko umekuwa mdogo zaidi kuliko hata kipindi cha JPM.

Hii ni kutokana na kupanda kwa bei ya bidhaa na huduma. Mambo yamekuwa magumu zaidi.

Hakuna hela yeyote.
Wow! Shocker!!!
 
Magufuli anatekeleza sera za Chadema .....huyu hafai hela zote anapeleka kwenye miradi, miradi yenyewe hasara tupu! Sasa ndege nani atapanda! Alafu analipa cash, si angekopa tu! Stendi ya mbezi ni ovyo italeta foleni kubwa! Magufuli ni dikteta amekataza siasa! Flyovers zipo Kenya zile za Magufuli hamna kitu!

Haya mzee wa watu kapumzika, shangwe likaibuka, kwisha Mataga, Sukuma gang watakoma! Mama achana na miradi ya Magufuli haina maana! Mama anaupiga mwingi! Mama anafungua uchumi! Sasa nchi inapumua, tuko huru kukosoa na kufanya siasa.

Sasa hivi, tuone mataga na sukuma gang wakisema Mama anaupiga mwingi ni block tu, Mama ni dikteta wa kike! Hata Magufuli hakuwahi kutufungulia mashtaka ya ugaidi! Huyu Mama ndio atakuwa the worst President ever!

Dah! Haya maneno yote yanasemwa na watu wale wale!
 
Kwa sisi wapiga deal mambo yetu yanatunyookea taratibu...

Ngoja mama aendelee kuupiga mwingi kwa kutalii kwa majirani ili sisi tuendelee kuzichangisha...

Tumeanza kwa kujenga vituo vya mafuta kila baada ya kilometa 2.
 
Back
Top Bottom